Sept 11 ni tukio la kigaidi la kufikirika, wamarekani wana siri nzito

Ama kweli siasa za kitapeli na kupwaya kwa akili zetu kuujuwa ukweli ni kufilisika werevu ndani ya vichwa vyetu. Kila mpumbavu atazua lake na tukamfuata tukijivuna tunaelewa. Hakika wapumbuvu wataendelea kutupumbumbaza na kutuburuza kwa sababu kila tunachoambiwa tunaitikia kwa sauti kuu huu ndiyo ukweli.

Tuangalie tutaishia wapi na hili la Alkaeda - Osama na Wamerikani..........Who is who and why is who and for what was who?
 
mwanzoni walikuwa wanamsifia sana na kumuita SHEIKH OSAMA BIN LADEN hawezi kukamatwa kijinga ni mtu mjanja na ana akili na mbinu zote kajifunzia MAREKANI. na akawa anatoa video zake na wanamshangilia .na wakawasifia sana akina MULLA NA WENZAKE WA AFGHANSTAN. lakini baadae OSAMA akavamiwa kwake ameuawa mbele ya mkewe na wanawe na akazikwa baharini. kuna binadamu kutoka tanzania nchi ya tatu kwa umasikini duniani wananchi wanaishi chini ya dola moja . ANABISHA ANASEMA YULE ALIYEULIWA SI OSAMA NA HAKUNA OSAMA DUNIANI.hivi huyu mtu kweli ana akili timamu kweli . kweli nimeamini umasikini ni ugonjwa
 
Nakubaliana kwa asilimia nyingi na mtoa hoja,
kuna documentary niliwahi kuingalia kuhusu 9/11 conspiracy naamini kabisa ni plan ambayo waamerika waliisuka. Hata leo kwenye yahoo wametoa habari ya 9/11 jinsi gani Bush alivyokuwa aware na tukio zima wiki moja kabla.

Lakini ikiwa umeamua kuamini 9/11 ni kweli ni jambo la kawaida tu kwani hata ni sisi wananchi tunaoamini maneno ya uwongo ya wanasiasa na kuwapa kura au wanao amini muhubiri fulani ana miujiza japo voishiria vyote vyaonyesha ni mtafutaji wa fedha tu.
 
Back
Top Bottom