Sensa: Ponda, wenzake wahesabiwa

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
Kwa mjibu wa taarifa ya habari ya saa moja leo asubuhi Kamishna wa Sensa amesema sheikh Ponda pamoja na makeke ya kupinga zoezi la sensa alisalimu amri na kukubali kuhesabiwa.

Kwanini hakutumia jukwaa lilelile kuwambia wafuasi wake wakahesabiwe ili kuwaepushia karaha na kadhia za kukumatwa na kufunguliwa kesi na wengine kuwapiga wake zao walikubali kuhesabiwa achilia mbali waliokimbilia porini kuwakimbia makarani wa sensa?

>>>>>>>>>>>>>>>>>
Habari kamili hii:

Chanzo: Mtanzania | JUMAPILI, SEPTEMBA 02, 2012 | Mwandishi - ELIZABETH MJATTA

VINARA waliokuwa wakihamasisha waumini wa dini ya Kiislamu wasishiriki Sensa ya Watu na Makazi, akiwamo Sheikh Issa Ponda wamehesabiwa. Kauli hiyo, imetolewa na Kamishna Mkuu wa Sensa, Amina Mrisho mjini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema hadi jana mchana idadi ya watu ambao walikuwa hawajahesabiwa walikuwa chini ya asilimia tano.

Aliwataka watu ambao hawajahesabiwa wajitokeze kuanzia leo hadi Septemba 8.

"Tulianza kuhesabu watu Jumapili na ilipofika Jumatatu asubuhi vinara wote waliokuwa wakipinga Sensa walikuwa wamehesabiwa akiwamo Sheikh Ponda.

Alisema makarani walifika nyumbani kwake ambako walikuta hayupo lakini walielezwa kuwa amekwenda katika Msikiti wa Mtambani.

"Lakini katika jambo la kufurahisha mke wake alitoa ushirikiano wote kwa makarani, baada ya kutoa taarifa zote za familia yake.

"Lakini baada ya wakarani kumaliza kuihesabu familia yake, alirudi kuungana na familia yake…kwa hiyo yeye alihesabiwa sasa wale wengine ambao walikuwa wanalishwa kaa la moto wajue wamepotoshwa,wapo ambao tayari wamekamatwa na jeshi la polisi.

"Sina takwimu sahihi ni wangapi, lakini mkoani Kagera watu 15 walikamatwa, Kiteto watano ambao wanaume ni wanne na mwanamke mmoja, mkoa wa Kilimanjaro ambao wamekataa kuhesabiwa ni wengi mno… lakini mkoa kwa kushirikiana na jeshi la polisi, wanafahamu ni hatua gani wanazochukua,"alisema.

Alisema mkoani Kagara, ndiko kulikuwa na vituko vingi kwa sababu wanaume walikuwa wakifanya mañosa makusudi kwa nia ya kutaka kutelekeza familia zao.

Mrisho alisema pia kuwa ili kuondoa migongano katika suala la kipengele cha dini, taasisi hiyo iko katika mchakato wa kupeleka bungeni Sheria ya Takwimu Sura ya 351 ifanyiwe marekebisho.

"Novemba tutaipeleka bungeni ifanyiwe marekebisho kusiwe na sheria inayoruhusu mtu kutoa takwimu bila kupitia kwetu kwa sababu kuruhusu vitu kama hivi ndiyo vinaleta mkanganyiko.

"Katika nchi ambazo zimeruhusu suala la dini na kabila kuingia kwenye Sensa, kumetokea machafuko makubwa na hata watu kupoteza maisha, hatutakia haya yafike kwetu," alisema.

Akizungumzia malipo kwa makarani na wasimamizi wa Sensa, alisema fedha kwa ajili ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ziliwasilishwa katika mikoa na wilaya siku nyingi na yalitolewa maelekezo ya jinsi ya kuzigawa.

"Natumia fursa hii kutoa tahadhari kwa wale wenye mpango wa kuchakachua malipo haya sheria itachukua mkondo wake na tutamhusisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwapata wachakachuaji," alisema.
 
Hizo ni propoganda!ukweli ni kwamba zoezi la sensa limekua hovyo.viongozi ngazi za chini hawakushirikishwa
 
Tbc hamuwajui? hawa jamaa waongo sn madaktar waligoma wao wakasema huduma znaendelea,walimu wamegoma wao wakasema hakuna mwalim aliegoma hawa jamaa wababaishaj sn .
 
Kama ni unafiki basi ni unafik wa kutupwa. Mbona mimi hivi sasa nasikiliza Radio Imani na akina Ponda wanakanusha kuwasaliti wenzao na kwenda kuhesabiwa.

Nimesikiliza sana Radio hiyo kuna mada inayosema "Vyombo vya Habari vinavyotumika kuwafarakanisha Waislamu" Kuna maneno mengi humo ikiwemo hukumu kwa wazandiki, wanafiq na watu wenye husda. Hukumu ni kali ikiwemo kichwa cha mzandik kuletwa mezani.

Sasa Ponda aangalie kama kweli kawasaliti wenzake asije akapewa fwatwa inayomsitahili toka kwa Maulamaa.
 
kupitia redio imani leo asubuhi kwenye kipindi kinachoitwa mwaangaza,shekhe ponda kakanusha habari hizo na kusisitiza kuwa hizo ni propaganda na msimamo wa waislam kususia sensa upo palepele.
 
Hukumu ni kali ikiwemo kichwa cha mzandik kuletwa mezani. Sasa Ponda aangalie kama kweli kawasaliti wenzake asije akapewa fwatwa inayomsitahili toka kwa Maulamaa.
Mkuu with all due respect kama hicho ulichokiandika hapo kwenye red ni kweli ni mafundisho ya Uislamu, basi with no doubt Uislamu kamwe hauwezi kuwa dini ya kweli, Mungu huyu wangu mimi wa Isaka na Yakobo kamwe hawezi kutufundisha mafundisho haya maana hukumu ni kazi ya Mungu.
 
Ni kweli kabisa Sheikh Ponda alishahesabiwa na mimi ndiye niliyekwenda nyumbani kwake kama msimamizi wa makarani wa sensa kuhakikisha kuwa yeye na familia yake wanahesabiwa. Hakuleta ubishi wala usumbufu wowote kama ilivyotarajiwa zaidi ya kunisihi sana tusiweke hadharani taarifa za yeye na familia yake kuhesabiwa.

Kwa mjibu wa taarifa ya habari ya saa moja leo asubuhi Kamishna wa Sensa amesema sheikh Ponda pamoja na makeke ya kupinga zoezi la sensa alisalimu amri na kukubali kuhesabiwa.
Kwa nini hakutumia jukwaa lilelile kuwambia wafuasi wake wakahesabiwe ili kuwaepushia karaha na kadhia za kukumatwa na kufunguliwa kesi na wengine kuwapiga wake zao walikubali kuhesabiwa achilia mbali waliokimbilia porini kuwakimbia makarani wa sensa.
 
somji juma
Jumuiya za Kiislamu kama OIC zitapata msg kwamba Wislamu wanadhulumiwa Tanzania na misaada ya tende na pesa itaongezeka kwenye taasisi za kiislamu ili kueneza Uislamu, maana tangu asset za AlQaeda ziwe freezied hawa wachochea chuki za kidini wamekosa ufadhili.
 
Last edited by a moderator:
Leo TBC na Gazeti la uhuru linaaminika habari zake!! Kweli bana 'hawatakuwa radhi mpaka tufate ila zao'. Wajiulize kwanza pamoja na Propaganda mbona zoezi limeshindwa? Uzuri tulisha shauriwa na Anna Makinda tukisoma magazet haya tusome kama vile ni barua za kirafiki.
Hata Meles Zenawi alipokuwa Kwenye Koma hospital kule Ubelgiji 'TBC' yao ilisema Mzee ni mzima kabisa kaenda kwenye mapumziko katika 'utaratibu alojipangia' mara kwa mara!
 
Ni kweli kabisa Sheikh Ponda alishahesabiwa na mimi ndiye niliyekwenda nyumbani kwake kama msimamizi wa makarani wa sensa kuhakikisha kuwa yeye na familia yake wanahesabiwa. Hakuleta ubishi wala usumbufu wowote kama ilivyotarajiwa zaidi ya kunisihi sana tusiweke hadharani taarifa za yeye na familia yake kuhesabiwa.

Akina 'Mwa' mnavisa nyie!!! Baada ya soko la Ngozi za binadamu kushuka kule Zambia sasa mmeanza ukuwadi wa kisiasa,muda si mrefu mtaanza kuuza 'Vibogoyo' vyenu vya mgongoni kujikimu!!!
 
Ndugu zangu wana jamii kumekuwa na upotoshaji wa dhahir kuwa sheikh ponda kahesabiwa, huu ni uongo wa dhahir waandashi wanasema uongo juu ya kiongozi wetu wa waisilamu wanaandika habari zisizo na uchunguzi leo redio imani imempigia simu ana ameongea live hii redio ni redio ya haki na inatowa taarifa kwa haki bila ya kupendelea upande wowote na mwenyezi mungu awalinde kwa hilo pole sana sheikh kwa kusingiziwa uongo MUSLIM LOVE YOU SO MUCH WEWE NDIO KIONGOZI WA KAHI UPO UPANDE WA WAISILAMU ALLAH AKULINDE
 
Ndugu zangu wana jamii kumekuwa na upotoshaji wa dhahir kuwa sheikh ponda kahesabiwa, huu ni uongo wa dhahir waandashi wanasema uongo juu ya kiongozi wetu wa waisilamu wanaandika habari zisizo na uchunguzi leo redio imani imempigia simu ana ameongea live hii redio ni redio ya haki na inatowa taarifa kwa haki bila ya kupendelea upande wowote na mwenyezi mungu awalinde kwa hilo pole sana sheikh kwa kusingiziwa uongo MUSLIM LOVE YOU SO MUCH WEWE NDIO KIONGOZI WA KAHI UPO UPANDE WA WAISILAMU ALLAH AKULINDE

Hivi kuwa kiongozi wa haki ni kuwa upande wa waislamu eeeeenh? Ooooooh kumbe! Nilikuwa sijui......
 
Unanijibu kwa kutumia masala niliyo kuuliza ....

Let me relax .... it seems ignorance is your daily bread
adai hajawahi kuhesabiwa, na kama aliwahi kuhesabiwa auliza wapi na kwanini vyombo vya habari vimeshindwa kuonyesha picha yake? adai jinsi ya vyombo vya habari vilivyokuwa vikimfatilia kama anagalihesabiwa coverage ya habari ingalikuwa hiyo.
lkn hadi vyombo habari kungojea tume ya sensa kutoa habari ni wazi hiyo ni propaganda.
asema atayafungulia kesi magazeti yliochapisha haabri hiyo bila ya yeye kama Mtuhumiwa kutopigiwa simu ya kuulizwa.
Mahojiano na redio Imaan leo asubuhi kipindi cha mwangaza wa Jamii

my take:
hata tzdaima leo hii lipo upande wa CCM kwa hili? nchi hii ipo mashakani kwa mandeleo
 
Back
Top Bottom