SENSA: Nini faida yake?

Sensa ni muhimu, matokeo ya sensa yatatumiwa na hii serikali kwa miaka mitatu ijayo yaani hadi 2015 ila matokeo hayohayo yatatumika hadi 2022.....Nina imani kubwa kwamba serikal itakayoingia madarakani 2015 na 2020 itatumia matokeo ya sensa yatakayopatikana mwaka huu kuleta maendeleo kusudiwa.
 
binafsi sipingi sensa ila nawapinga wanasiasa wanapoizungumzia sensa eti kwa ajili ya maendeleo!! sikubaliani kabisa na upuuzi huu.labda waniambie sensa ni kwa ajili ya nchi kufahamu tu idadi ya watu wake lakini si kwa kigezo cha kuwaletea maendeleo.

Tangu ifanyike sensa ya 2002 mpaka leo ni maendeleo yapi ambayo yamepatikana kwa sisi wananchi zaidi ya huduma za kijamii kuzidi kudorora? leo hii kuna wanachi ngozi za kuku'vichwa vya kuku hadi miguu ya kuku ndiyo wanavitumia kama vitoweo je mwaka 2002 yalikuepo haya? kama haya ndiyo maendeleo basi tumepiga hatuwa.

kama kuhesabiwa ni maendeleo vipi hospitali nyingi zikose huduma sitahiki kama madawa'vitanda vya wagonjwa' wahudumu nk? wanasiasa acheni upumbavu wa maneno yenu ya kipumbavu yasiokuwa na tija kwa watanzania.msifikiri maisha mnayoishi nyinyi basi na watanzania wote wapo hivyo.

sipingi sensa ila maneno ya wanasiasa wapumbavu na wengineo wanaosema eti sensa kwa maendeleo upumbavu mtupu.
 
Nadhani kwa serikali makini inabidi iweze kubuni aina nzuri ya kujua idadi ya watu wake kupitia mifumo bora zaidi ya kupita kila kaya...

Wakae chini na watu wazuri wa data na IT specialists waweze kuestablish National Database ambapo kila anayezaliwa au kufa information hiyo inakuwa available na kuhakikisha iyo database inakuwa up to date..

Hii ya kupita kila kaya haiko feasible tena ukizingatia life styles za sasa na watu wanavyohustle kujitafutia maisha..!!
 
SENSA inafaida gani kwa watu wa wilaya ya KONDOA? miaka 50 sasa hakuna High school, hakuna Hospitali, hakuna maji, hakuna Umeme,hakuna barabara n.k.

Binafsi yangu sioni faida ya sensa, kama hata maji bado watu wanachota mtoni, highschool mpaka twende moshi, songea, mwanza nk. KAMA BUDGET YA TAIFA HILI inazingatia idadi ya watu mbona kila mwaka budget haikidhi mahitaji ya wananchi?? na bado sehemu kibao zimesahaulika. NINI FAIDA YA SENSA KTK WILAYA YA KONDO?
 
mkuu mwigo mwezi wa sita nilibahatika kutembelea maeneo haya hamai, churuku, matui, ni hatari ukitaka maji lazima ukimbie km 8, km5, km2 sasa ukiangalia hayo maji kwa macho huwezi kunywa, labda umchukue mchungaji msigwa uyaombee,halafu ningeomba m4c waende maana wanajua kuna chama kimoja tu hapa tz.

KICHEKESHO kingine kipo stand ya mabasi hapo Dodoma hahahahaha eti makao makuu utafikiri stand ya koboko mwigo tujipe pole.
 
SENSA inafaida gani kwa watu wa wilaya ya KONDOA? miaka 50 sasa hakuna High school, hakuna Hospitali, hakuna maji, hakuna Umeme,hakuna barabara n.k. Binafsi yangu sioni faida ya sensa, kama hata maji bado watu wanachota mtoni, highschool mpaka twende moshi, songea, mwanza nk. KAMA BUDGET YA TAIFA HILI inazingatia idadi ya watu mbona kila mwaka budget haikidhi mahitaji ya wananchi?? na bado sehemu kibao zimesahaulika. NINI FAIDA YA SENSA KTK WILAYA YA KONDO??/

Uchawi mwingi sana pale.......huwezi pata maendeleo wakati uchawi umeshamiri!
 
kwa nini kondoa?

Kama mitume walihesabiwa kwenye sensa, tunapotafuta sababu za kuipinga, siuoni ubora wa akili tunaoutumia.

Angalieni watindiga wenye sababu za msingi walivyotekelezewa matakwa yao, wanapewa nyama pori ili wabaki home wasenswe!!!! Sasa ndugu zangu wa kondoa mnapima umoja wenu kwa reagent feki!!!!! Hesabiweni bwana, achaneni makinyongo.
 
Tuache ushabiki wa kisiasa...sio kwa sababu unashabikia upinzani au kwa sababu unachukia CCM ndio upinge kila kitu kinacholetwa na CCM.

Kwenye masuala muhimu yanayohusu maslahi ya kitaifa ninaomba tuache ushabiki na chuki. Mimi nadhani ni sahihi kama mtu atakuja na hoja kuhusu namna sensa inavyofanywa na sio hoja ya kuipinga sensa pasipo sababu za msingi.
 
Tuache ushabiki wa kisiasa...sio kwa sababu unashabikia upinzani au kwa sababu unachukia CCM ndio upinge kila kitu kinacholetwa na CCM. Kwenye masuala muhimu yanayohusu maslahi ya kitaifa ninaomba tuache ushabiki na chuki. Mimi nadhani ni sahihi kama mtu atakuja na hoja kuhusu namna sensa inavyofanywa na sio hoja ya kuipinga sensa pasipo sababu za msingi.

hoja ni hoja tu, usiipunguzie mvuto kwa kuiita haina msingi! Aliyeianzisha anajua msingi wake, waambie wanajamvi ni nini "maslahi ya taifa" sijaona chuki kwenye hii hoja, wala hapajashabikiwa lolote hapo, unaonekana mkuu umekariri jinsi ya kujitetea kwa staili ya kujihami. Hoja imejengwa kwenye kipambanuzi cha maendeleo!!!!

haya sasa changia ukiwa soba.
 
we upo kondoa gani? maana kuna kondoa ya ovada usandawe hadi kurio wao wanajijengea sekondari na kuchimba visima,na kujenga zahanati HALAFU kuna kondoa ya farkwa ,babayu , kondoa mjini na kule kwa kina nkamia juma wao kipaumbele chao ni kujenga madrasa! wewe upo kondoa ipi mkuu?
 
Mwinyi - Copy.JPG
Umenikumbusha shambani kwa huyu Mzee Bella hapo Kondoa, ambaye huweka kumbukumbu zake kwa kupanda miti....! Jamaa kwa majungu yao wakamshitaki mzee wa watu kuwa anaweka uchuro kwa kuweka vibao na kugeuza shamba kama makaburi!
 
we upo kondoa gani? maana kuna kondoa ya ovada usandawe hadi kurio wao wanajijengea sekondari na kuchimba visima,na kujenga zahanati HALAFU kuna kondoa ya farkwa ,babayu , kondoa mjini na kule kwa kina nkamia juma wao kipaumbele chao ni kujenga madrasa! wewe upo kondoa ipi mkuu?

Ila umeme upo Kondoa mjini, mondo, Goima, Jenjeluse na kuendelea..................
 
SENSA inafaida gani kwa watu wa wilaya ya KONDOA? miaka 50 sasa hakuna High school, hakuna Hospitali, hakuna maji, hakuna Umeme,hakuna barabara n.k. Binafsi yangu sioni faida ya sensa, kama hata maji bado watu wanachota mtoni, highschool mpaka twende moshi, songea, mwanza nk. KAMA BUDGET YA TAIFA HILI inazingatia idadi ya watu mbona kila mwaka budget haikidhi mahitaji ya wananchi?? na bado sehemu kibao zimesahaulika. NINI FAIDA YA SENSA KTK WILAYA YA KONDO??/
Hospitali ipo hapo pembeni ya ofisi za halmashauri na huko kwingine vijijini kuna vituo vya afya na zahanati labda useme habari ya uchache.............Umeme nao upo mjini, na vijiji vyote inakopita barabara ya kuelekea Kiteto. Barabara inajengwa toka babati mpaka dodoma tatizo ni kasi ya mkandarasi ama labda serikali haimlipi kwa wakati............Mengine ya maji na high school sina la kusema!
 
Ni kweli jamaa alitia sana chumvi,pamoja na kwamba sensa implementation ya datas zake kwenye kuwaletea wananchi maendeleo imekuwa too slow,, lkn alizidisha sana
 
sensa ni mbinu ya mafisadi kutufisadi fedha zetu......barabara mbovu zinaonekana si lazima sensa au kujua idadi ya watu watembeao juu ya barabara hiyo
 
Back
Top Bottom