Sensa/Faini

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,398
8,885
Nimekuwa nikisikia kila kukicha kuhusu baadhi ya watu kugomea Sensa, hivi ni kwa nini Serikali isiwapige faini wale wote ambao hawatataka kuhesabiwa badala ya kupoteza muda sijui kukamata shehe huyu sijui mwenyekiti wa kijiji yule.

Naona imefika wakati sasa Serikali iwe Serikali hamna kubembelezana tena, tunakuja nyumbani kwako hutaki kuhesabiwa faini na ni lazima ulipe usipolipa tunataifisha mali tunaendelea mbele.

Haiwezekani watu kugomea Sensa ikimbukwe serikali inatumia pesa nyingi sana kwa zoezi hili na watu hao hao wanaolia umaskini kila siku ndio wa kwanza kuhujumu rasilimali zetu!
 
....wakati huo huo tukijiandaa kwa machafuko yanayoweza kutokea...hayakuanza hivi hivi tu ila yalianzishwa na watu, tukachekelea na matokeo yake ndio haya kila mtu kuwa na ndevu kama kambale..
 
Mawazo yako ni dhaifu sana, na ayaendani na level ya JF.
Kama kawaida kwa kuwa hukubaliani na jinsi mwingine anavyofikiria unaamua kutoa kashfa, sasa sijui unatumia kigezo gani kuita mawazo ya mtu mwingine dhaifu hayafai kuwekwa hapa kama uko sahihi kwa nini sasa mods hawajaitoa au unashauri na mods wa JF nao dhaifu kwa maana wameshindwa kuona udhaifu wa mawazo yangu? Inabidi ukue (kiakili) sio lazima wote tukubaliane, nchi tuko mill 40 hivyo haiwezekani wote tukawa na mawazo sawa!
 
Kwa maoni yako mwenyewe umesema sio lazima watu wote wakubaliane kwa kila kitu humu,hivyo ulipaswa kukubali kupokea opposition pia na muhimu ni kuvumiliana kimawazo,haya ni maoni yangu unapaswa kuyaheshimu pia
 
Aiseee baba yangu hakuna kipengele chochote kinacho sema nikikataa kuhesabiwa nipigwe fain,,cha msingi serekali itowe somo la kutosha kuhusu kuhesabiwa,,,mi nafananisha sensa kama kupiga kura ni si lizima kupiga kura hata kama umejiandikisha

ngoja nikate kiu na mbege
 
Kwa maoni yako mwenyewe umesema sio lazima watu wote wakubaliane kwa kila kitu humu,hivyo ulipaswa kukubali kupokea opposition pia na muhimu ni kuvumiliana kimawazo,haya ni maoni yangu unapaswa kuyaheshimu pia

Sawa kabisa, ila kuna tofauti kati ya kutokukubaliana na mtu na kumkashifu yule usiyekubaliana naye, na ndio hoja yangu, kama hukubaliani kile mwingine alichosema aidha umjibu kwa kumwambia kwa nini hukubaliani nae au vinginevyo unampotezea hautapungukiwa na chochote nafikiri kuna tofauti hapo!

Enzi za NYERERE wasinge thubutu kwani wote wangeishia kizuizini. kila mtu anaona yeye ndio serikali.nini faini tandika fimbo adabu ipatikane.
 
Nimekuwa nikisikia kila kukicha kuhusu baadhi ya watu kugomea Sensa, hivi ni kwa nini Serikali isiwapige faini wale wote ambao hawatataka kuhesabiwa badala ya kupoteza muda sijui kukamata shehe huyu sijui mwenyekiti wa kijiji yule.

Naona imefika wakati sasa Serikali iwe Serikali hamna kubembelezana tena, tunakuja nyumbani kwako hutaki kuhesabiwa faini na ni lazima ulipe usipolipa tunataifisha mali tunaendelea mbele.

Haiwezekani watu kugomea Sensa ikimbukwe serikali inatumia pesa nyingi sana kwa zoezi hili na watu hao hao wanaolia umaskini kila siku ndio wa kwanza kuhujumu rasilimali zetu!

Yaani hapa ndo mwisho wa upeo wako wa kufikiri? sasa faini hiyo kwa kosa gani? kwani mtu asipohesabiwa ni kosa,
mbona hamna uhusiano wowote kati ya sensa na faini, jitahidi kuuliza na kupata mawazo kabla hujapost hizi pumba zako humu jf.
 
Nyie na serikali yenu dhaifu endeleeni kutapatapa bt waislam msimamo uleule hakuna kipengele cha dini hakuna muislam kuhesabiwa,chezea waislam ww!
 
hebu nipe namna ya kuwatoza hiyo faini

Hiyo yote ni katika kutaka kuwaeleza watu kwamba hivi vitu kama sensa au uchaguzi haviji bure, ni vya gharama kubwa sana, Serikali inatumia pesa nyingi (pesa zetu walipa kodi), sasa kuona mtu au kikundi cha watu kinajaribu kuzuia sensa isifanyike ni kama kuchukua hela na kutupa chooni wakati mtu huyo huyo anataka Serikali hiyo hiyo impe huduma mbalimbali zinatoka wapi?

Sensa au upigaji kura havijagunduliwa Tz, Dunia nzima wanafanya hata UN wanatambua hilo, kwa hiyo mimi naamini kabisa kwamba Serilkali kuna wakati inapaswa kutumia nguvu kama pale inaona kabisa hili jambo lina manufaa kwa jamii kwa ujumla!

Kuhusu namna ya kutoza faini ziko nyingi, Serikali ni kuamua, kwa mfano wanakuja Nyumbani hutaki kuhesabiwa wanaamrisha kule unakofanyia kazi kukata 1/4 ya mshahara kulipia gharama, mpaka utakapo kubali, kama mkulima bei ya pamba wanakata kufidia gharama, njia ziko nyingi sana kama Serikali haitashindwa, ikiamua!

Yaani hapa ndo mwisho wa upeo wako wa kufikiri? sasa faini hiyo kwa kosa gani? kwani mtu asipohesabiwa ni kosa,
mbona hamna uhusiano wowote kati ya sensa na faini, jitahidi kuuliza na kupata mawazo kabla hujapost hizi pumba zako humu jf.
Sina haja ya kujibizana na wewe kwani wewe ndio wale wanaosema mtoto ni wangu naamua mwenyewe kama aende shule au akae nyumbani na serikali haipaswi kuniuliza!

nguvu, mabavu hayawezi kuleta takwimu sahihi, ukumbuke kuwa ni wananchi ndio wanaotoa taarifa na hao makarani wanajaza kulingana na kinachosemwa na muhojiwa. Katika kanuni za kitafiti, ili upate takwimu sahihi hutakiwi kumlazimisha au kumrubuni kwa vitu ama pesa unayemuhoji. Kwa hili siri kali sikivu imekula kwao.
 
Mi nazani Elimu ndo inatakiwa kutolewa kuhusu sensa na sio mabavu..

Vyovote vile ambavyo itaonekana inafaa, ila mwisho wa siku Sensa lazima ifanyike na kuokoa tu fedha kupotea bure, kama wakitumia Elimu na sensa ifanyike sawa, kama ni faini pia sawa lakini mwisho wa siku zoezi lisishindwe na kupoteza pesa zetu bure!

Back
Top Bottom