mnyanyaswaji
JF-Expert Member
- Nov 10, 2009
- 478
- 117
Wanajamvi habari zenu, leo baada ya swala ya Ijumaa waislamu ndio wametoa picha sensa hii itakuwa ya aina gani. Jibu ni kama kuchakachuliwa kwa matokeo ya uchaguzi na sio figure halisi. Tuwekeni ushabiki pembeni serikali ya sisiemu inavuna ilichopanda kwani propaganda zina ukomo wake. BAKWATA nao wakikaa kny Tv wanawahadaa watanzania kuwa hali ni shwari na waislamu wote watashiriki sensa, jamani eeh uongo uongo na tena uongo, kumbukeni bakwata inawakilisha wazee wachache sana wakiislamu tena wachache mnoo. Madhehebu ya kiislamu yote lao moja except bakwata. Swali linakuja je tunalazimisha ili kuleta ubabe kma ada yake ilivyo? Kwa nchi zilizo serious wananchi wangeingilia kati kuokoa Billion 141 zisipotee za sensa. Kwa walio karibu na misikiti leo watakubaliana na mie nini ninachosema. Tutarajie uchakachuaji wa matokeo na sio idadi halisi. Au hii plan imewekwa ili ipatikane pesa za kampeni hizi billion huku wakijua zoezi litafeli?? Nawakilisha wadau