Sendeka amesimama kuhesabiwa kuhusu Tanganyika

hoja ya utanganyika, uzanzibari na utanzania tunaweza iweka kapuni for some time, kwani inapoteza dira na malengo ya mtanzania wa chini kabisa ambaye mahitaji yake muhimu ni chakula, mavazi, elimu, mahala pa kulala n.k. matatizo ni mengi sana tz yetu hii, hatuwezi fanya kila kitu ni priority, nadhani tungekomaa na mambo machache then mengine yatakuja baadaye, hapa ufisadi, hapa katiba mpya, hapa kilimo kwanza hakitekelezeki, hapa elimu duni, hapa uongozi mbaya, hapa kila kila kitu. yani ambacho si kizuri ndio kipo hapa. muda umefika wananchi tuamue priority ni nini kwetu na tuanze mapigano hadi kieleweke..

Hoja yako hapo kwenye nyekundu kwa kifupi ni RASILIMALI. Huwezi ukazungumzia rasilimali kama katiba haijakaa vizuri na katiba ina historia yake. Na mojawapo ya historia ya Katiba ya Tanzania ni suala la muungano ambalo halijakaa vizuri. Juzi juzi jamaa wamenusa mafuta huko Zenj wakasema hilo litolewe kwenye mambo ya muungano maana rasilimali hiyo ya mafuta itawafaidia wazenj tu. Mimi naamini matazizo ya watanzania siyo hayo uliyoyaorodhesha hapo juu pekee. Ni pamoja na misingi ya utawala ambayo ni ya kikatiba ambayo inawafanya watawala wetu wawe miungu watu wakijigawia mali zetu wapendavyo nasi tukiendelea kukosa hayo mambo muhimu uliyoyaorodhesha.
 
Hongera mh. Sendeka, huu ni wakati muafaka wa kuelezana ukweli, siasa za vitisho vina mwisho, lazima tuwe na serikali yetu kamili Tanganyika hao wanaopigania muungano kwa maslahi binafsi zao zipo ukingoni, hawana cha kuwaeleza wananchi zaidi kusifia muungano ambao hauna maana yoyote ile kwa watanzania wa kawaida, wazinazibar wengi wanadhana ya kuwa watanganyika tunanufaika na muungano, binafsi sijui nimenufaika nini hadi sasa hawajui kama tumewabeba kwa muda mrefu bila ridhaa yetu, muungano nia yake kubwa ilikuwa ni kuleta umoja kamili kati yetu kama wao hawautaki tunawalazimisha nini?
Chama
Gongo la Mboto DSM
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwa mbali naiona Mamlaka ya Watu wa Pemba inanukia chini ya P.L.O(Pemba Liberatio Organization).
Sijui kama Jamhuri ya Watu wa Unguja itawavumilia hawa P.L.O.
 
Tupo pamoja.

Kuanza kulipia makaratasi na document upya ni kasheshe.......

Kama UNGUJA hawataki Muungano na Pemba wanataka, basi fukuza Unguja na walete Wapemba hapa.....

Tanzania is here to stay hata kama haitakuwa Jamhuri ya MUUNGANO na ibaki Jamhuri ya Tanzania....
Hapa hatudai Tanganyika, tunataka muungano uvunjwe
 
Mwanzo wa G55 nyingine?

MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, wamezozana hadharani wakipishana maneno kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Katiba. Mzozo huo ulizuka juzi kwenye mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat) uliofanyika Kunduchi, Dar es Salaam juu ya mada ya Mabadiliko ya Katiba.

Baada ya Masaju kumaliza kuelezea madhumuni ya muswada huo, Sendeka alisimama na kuhoji kuhusu kauli iliyotolewa awali kwenye mkutano huo na Waziri Kombani kuwa, moja ya sababu za kuandikwa kwa Katiba mpya ni mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar iliyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Sendeka alisema mabadiliko hayo yameifanya Zanzibar kuwa nchi kamili, hivyo ni muhimu sasa kwa Watanganyika nao wadai serikali yao. “Waziri amesema moja kati ya mambo yaliyosababisha mabadiliko ya Katiba, ni mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Mabadiliko yale yameifanya Zanzibar kuwa nchi kamili. Na sisi tudai Serikali ya Tanganyika. Mwambieni Rais (Jakaya) Kikwete hivyo,” alisema Sendeka.

Hata hivyo, wakati wa kujibu maswali, Masaju alisema Zanzibar siyo nchi kwa maana ya dola, bali ni kwa maana ya mipaka.
“Siyo kweli kwamba Zanzibar ni nchi kwa maana ya dola, bali ni nchi kutokana na mipaka yake,” alisema Masaju kwa hasira huku akinukuu baadhi ya vifungu vya Katiba ya Zanzibar na kuongeza:“Someni Katiba ya Zanzibar na hati za muungano.”

Baada ya Masaju kukaa, Sendeka alisimama tena na kusema: “Sawa, yaani unatujibu kwa hasira hivyo? Katiba ya Zanzibar imetoa madaraka makubwa. Zamani kwa kesi za Mahakama ya Rufaa walikuwa wakija huku (Tanzania Bara), lakini siku hizi mahakama yao ina mamlaka ya mwisho. Wewe si umesoma sheria na sisi hatujui sheria, basi tunakwenda kutunga sheria na wewe utaitumia tu. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.”

Kauli hiyo ya Sendeka iliibua shangwe kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo.

My take:

Kauli ya Sendeka kuwa yeye(Masaju) ni mwanasheria lakini wao(kina Sendeka) ni watunga sheria watatunga na Masaju lazima ataitumia tu inaacha maswali mengi badala ya majibu kuwa wakati wa kujadili muswada huu kutakuwa na mvutato mkubwa sana baina ya wabunge wa pande zote.


Tangia tumekuwa na huu Muungano tumefaidika na kitu gani. Hebu tupime kati ya Faida na hasara tulizopata hadi sasa kisha tuamue keundelea ma kuuvunjilia mbali
 
Hapa hatudai Tanganyika, tunataka muungano uvunjwe
muungano uvuvnjwe na tanzania indelee kuwa tz na capital yake dom. visiwa tunavyo vingi ie mafia, ukerewe
kwa hivo kama visiwa viwili vinata kutoka tz viache vitoke
 
muungano uvuvnjwe na tanzania indelee kuwa tz na capital yake dom. visiwa tunavyo vingi ie mafia, ukerewe
kwa hivo kama visiwa viwili vinata kutoka tz viache vitoke

Unafahamu mipaka ya Zanzibar inaishia wapi wewe?
 
Unafahamu mipaka ya Zanzibar inaishia wapi wewe?

Hebu niambie inaishia wapi sifahamu lakini sio zile habari 10 mile strip ya coast ambayo sultan aliachiwa atawale na mkoloni! Sisi tunachotaka ni Tanganyika yetu muungano utavunjika, utabaki sisi hatutaki kujua tunataka Tanganyika yetu irudi. Mungu ibariki Jamhuri ya watu wa Tanganyika
 
Wangapi wanaitaka Tanganyika?

Kama wapo nani kawanyima?

Hivi kudai Tanganyika kwasababu eti Zanzibar imepewa madaraka zaidi kikatiba ni akili au tope?

Tudai Tanganyika kwakuwa ikiwa tuna sababu za msingi bila kuwanyima haki ya msingi wazanzibar waishi wapendavyo...

Tropical your just a joke,yaani Wazanzibar waishi wapendavyo na wabara waishi kwa hofu ndani ya muungano ,how?
 
Viva Ole Sendeka,watu wako tuko nyuma yako tukikusuport!lazima tuwe nchi tuachane na choko choko za muungano,hazina msaada
 
Hongera Sendeka umesema yaliyoko moyoni mwako sio kufuta upepo.

MOD. TUWEKEE KURA YA MAONI HAPA KUHUSU HUU MUUNGANO WETU
 
hahaa!

ivi unajua uwa najiulizaga kila nikitizama vituko, midomo na sharubu za sendeka.

ivi atumii majani kweli?

Ole Sendeka (Mzee Sendeka) havuti wala kuitumia bangi a.k.a. ngambo kali a.k.a. majani.

Ila wewe inaonyesha unatumia bangi kama si sembe ya afghani. Kwasababu ni mvivu wa kuelewa na mgumu wa kujifunza tena mzito wa kujikosoa/kuliona kosa lako. Ila ni hodari wa ubishi. Hebu angalia kiswahili chako kilivyo kibovu na uj**** wa kushindwa kuandika maneno vizuri. [wana-jF ingie kwenye profile yake halafu angalia kiswahili alichotumia kilivyo kibovu)
 
we lazima mwaka huu mbivu na mbichi za utanganyika na uzanzibar zijulikane
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom