send off

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,399
Naomba kujuzwa siku ya send off kama mwanaume muoaji anatakiwa ajpange kwenda na vitu gani kwa maana nasikia huwa kunafaine za hovyo hovyo sana..
 
we nenda mwenyewe ukiona wanataka hela kimbia uone kama bibi harusi hajatoka haitebo kukukimbiza.

Huwa wanawaonea mabozo
 
Naomba kujuzwa siku ya send off kama mwanaume muoaji anatakiwa ajpange kwenda na vitu gani kwa maana nasikia huwa kunafaine za hovyo hovyo sana..

Hakuna chochote cha kupeleka...we vaa pendeza,uwe nadhifu...pale unakuwa kama unatambulishwa kwa ndugu wa upande wa kike ambao wanamuaga binti yao.
 
Begi la nguo za harusi za mkewe

ila na wewe si unandugu zako wanajua kawaulize ukifuata ya hapa it will eat your side.

Hakuna chochote cha kupeleka...we vaa pendeza,uwe nadhifu...pale unakuwa kama unatambulishwa kwa ndugu wa upande wa kike ambao wanamuaga binti yao.
 
Jamii hio inategemea saana na kabila ambalo umechumbia na kuoa. Pamoja na kusema kua mambo mengi yamechakachuliwa katika tamaduni za kuendesha mambo mbali mbali katika makabila; areas kama misiba na harusi hizo taratibu za kitamaduni bado zinatawala. Kuna makabila mengine wastaarabu na mengine mmmh! Mpaka utoke hapo kijasho kimekutoka! Hata hivo swali lako ungejibiwa kwa ufasaha kwa kumshirikisha mchumba wako ili akupe taratibu na kukudokeza yalo ya muhimu....
 
kongosho umenifurahisha kweli...yaani nimebaki nimecheka mpaka basi........bibi arusi atakavyonikmbilia mbona ni balaa..hahahahahaha
 
Inategemea na kabila la Mke Mtarajiwa, mfano kama ni Mchaga, andaa Blanketi la Bibi. Kuna makabila ambayo huwa wanakuvizia mlangoni wakati unaingia ukumbini ili wakutoe upepo, so andaa Dolari mfukoni mwako siku hio.
 
Hizi tunaita internal technic, sijui imekuwaje hata nikakuibia hii siri

kongosho umenifurahisha kweli...yaani nimebaki nimecheka mpaka basi........bibi arusi atakavyonikmbilia mbona ni balaa..hahahahahaha
 
inategemea na kabila,ongea na mwenzio atakwambia yote,all in all andaa vijisenti kidogo sana,kuwa na mia tano tano kama elfu kumi tu,vifaini unatoa mia tano tano na utarudi na chenji kibao
 
Back
Top Bottom