mkuu kumbuka ripoti ya Mwakyembe ilionyesha kuwa Rostam alikataa kutokea na alipuuza 'samansi'. Bila shaka Rostam alisha jiapiza kutohojiwa na Kamati ya Mwakyembe.
RA alikataa kutokea kwa hiari yake; kamati ya bunge ilikuwa na nguvu na uwezo wa kutumia njia zingine halali kisheria kuwalazimishiwa watuhumiwa kuhojiwa.
Kama wahusika wakubwa kwenye hili ni Lowassa na RA, ninashangaa kweli hii kamati ilishindwa kutumia nguvu zake kisheria kuwahoji hawa watu. Maneno ambayo wangeyasema mbele ya hicho kikao, yangelikuwa na nguvu na ingelikuwa hata rahisi kuwachukulia hatua za kisheria.