Selelii awazima Lowassa na Rostam

Nafikiri hapa tukubali tumeguke.

Vyama vingi vya upinzani au wapigania uhuru walikuwa wanagawanyika katika makundi mawili. Moja ni lle la military wings na jingine ni Political Wings.

Kuna wengine mnaona kuwa mabadiliko ya kweli yataletwa kwa KUPIGA sana kelele. Haya makele wengine yametuchosha na tunasema sasa inabidi kubadilisha mwelekeo wa mapambano. Nyie mnaamini kuwa hii njia inafanya kazi ila wengine tunaona kama vile Fisi anaumezea na kuupigia makelele mkono wa binadamu ukatike.

Inawezekana mko sawa, na endeleeni kupiga kelele. Mie najipelekeka kwenye kundi la watu wanaosema 'imetosha' na sasa ni kuanza kupambana nao direct. Kama ni maandamo au chama cha upinzani. Hakuna haja ya wenyewe kwa wenyewe kuanza kutukanana. Kama unafanya hivyo basi uko kwenye pay roll ya RA.
Sikonge tunaweza kukufuata lakini inabidi utueleze jinsi gani ya kufuata hiyo njia yako, na imebidii nikuulize hivi kutokana na maandishi yako ya jana ambayo nilikueleza faida za kupigania tunachopigania ni Sikonge na maeneo mengine ya njii hii, tusije tukalaumiana ooh kwetu hakuna umeme, ohh hakuna barabara, umeme au investor or sisi tunalima tumbakuu , watu wamechongeka nk nk . hatuna wasomi nk nk.
So nasubiri mkakati wako ilinione unafaa au niendele kupiga kelele kwa sasa.
 
Kupiga kelele?? Kelele zitasaidia nini!! Nilidhani ungesema zichukuliwe hatua fulani ili kuzuia. Lakini kelele tu mtapiga wee usiku na mchana na hakuna kitachotendeka. Si umeona mwenyewe kelele za wabunge zilipolifikisha suala la Richmond!! Waliapa kuwa ikiwa serikali haitokuja na majibu ya kueleweka kwenye kikao cha Bunge lililopita wangepiga vote of no confidence kwa serikali. Mbonan hawakufanya hivyo na imo ndani ya uwezo wao? Wamebaki kulalamika tu.. Hebu jamani tuwe realistic for once..Watu wote wamo katika maslahi tu. Hakuna cha utaifa hapa..
tk
Hayo uliyosema ni kweli, Hatua zinahitajika dhidi ya haya yanayolalamikiwa, je unaweza kupendekeza hatua yoyote mbali na zile zinazogusiwa na baadhi ya Wachangiaji; za kuanzisha vurugu, Kuchukua Ikulu au Kuingia Msituni?
 
Hao Lowassa na papa fisadi ni wapambe wako maana wanakupamba kwa kila namna ili ukamuondoe mbaya wao kule Kyela.

Mimi sijakulink kabisa na hao mafisadi bali kilichokulink na hao mafisadi ni unachoandika hapa cha kuwatetea kwa nguvu zako zote bila kujali maslahi ya nchi yetu na kuthubutu kusema eti tufukie mashimo na kusonga mbele bila kutafutia ufumbuzi madudu chungu nzima ambayo yanaitafuna nchi yetu kila kukicha. Unayoyaandika yanaonyesha kabisa hufai kupewa wadhifa wowote ndani ya nchi yetu hata ujumbe wa nyumba 10 haukufai.

Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inapita katika wakati mgumu kuliko wowote ule hatuhitaji Wabunge wa kufukia mashimo ili tu tusonge mbele wakati huko mbele kuna kiza cha kutisha na nyuma pia kuna madudu ya kutisha. Hatuwahitaji kabisa ndani ya Bunge letu Wabunge wenye kutaka kufukia mashimo kama wewe utakavyo.

Mkuu BUBU ATAKA KUSEMA, achana na MTANZANIA, tumemwelewa! He is simply stupid! Anataka kutatua matatizo ya Tanzania kwa remote control, akiwa London na kwa maelekezo ya mafisadi!
 
Mkuu BUBU ATAKA KUSEMA, achana na MTANZANIA, tumemwelewa! He is simply stupid! Anataka kutatua matatizo ya Tanzania kwa remote control, akiwa London na kwa maelekezo ya mafisadi!

Mwanakijiji,

Niliposema tumegeke, nilikuwa nina maan sisi Wapinzani wa Ufisadi. Kuna makundi mawili au matatu hapa kwa sasa. Moja linataka tubaki tukipiga kelele. Jingine tuache na tuendelee na mengine na ambalo mie nipo karibu nalo. Ila mie si kuwa tuache YAISHE, la hasha. Mie niko upande wa tukae tujadili jinsi gani ya kubadilisha mashambuli. Sisemi tuache, la khasa. Tubadili tu njia za ku-solve hili swali. Ni sawa na hesabu, mwingine anaweza kutumia njia ya Finit-Element-Method na mwingine akatumia Integration equastions ila majibu yatakuwa yanakaribiana sana.

Wengi hapa wanataka Mafisadi wakamatwe, washitakiwe na wahukumiwe. Ila kuna wengine wanapiga kelele tu bila kufahamu hali halisi ya nchi yetu. Inabidi katiba zibadilike, wananchi wabadilike, miiko ya uongozi, mihimili ya dola nk iwe inafanya kazi barabara bila ya kuingiliana.

Ndiyo maana nilishangilia sana kigazeti cha Cheche. Juzi Kishoka kaja na mawazo ya chama kipya, nimesema wazi kabisa kama kitakuwa chama cha wananchi na si NGO au Chama cha Watu, basi mie nimejiunga.

August:

Kuna thread juu ya chama kipya anataka kuanzisha Rev. Kishoka. Unaweza ukaja kujiunga nacho mara kikianza. Pia tunaweza kumobilise Sallim A. Sallim achukue form nje ya CCM na sanasana ningelipenda achukue kwa kofia ya CHADEMA. Hana anachoweza ku-loose. Na akitoka, ataweza kuchukua CCM kadhaa na yeye.

Hilo ni wazo langu kwa sasa. Inawezekana siko sahihi. Ila naona CCM imekuwa kikwazo kikubwa katika kubadili katiba na kuweka miiko ya viongozi.

Tuendelee na mashambulizi yote bila ya watu kuanza kuitana STUPID na FISADI. Wewe mtu hajawahi kufanya kazi Tanzania hata siku moja. Hajawahi kufanya kazi ya serikali ya Tanzania wala shirika lolote (kupata mshahara wa Tanzania) leo unamwita FISADI? Hivi kwa nini watu wengine hawawezi kujadili bila ya kuweka matusi?

Ninakubaliana na mwalimu mmoja wa secondary aliyesema kuwa 'kumfukuza mwanafunze shule, ni kukubali umeshindwa kazi'. Leo nasema mtu akianza kurusha matusi, basi huyo ni MUFILISI wa majadiliano. Yaani ni MWEUPE wa point na anachoweza kukimbilia ni MATUSI na kutowa personal attack.
 
tk
Hayo uliyosema ni kweli, Hatua zinahitajika dhidi ya haya yanayolalamikiwa, je unaweza kupendekeza hatua yoyote mbali na zile zinazogusiwa na baadhi ya Wachangiaji; za kuanzisha vurugu, Kuchukua Ikulu au Kuingia Msituni?

Tungeenda hatua kwa hatua.

1. Kila mass action lazima iwe na maandalizi na uongozi. Kwa kawaida haya hufanywa na vyama vya upinzani. Kwa kuwa nchini kwetu vyama hivyo ni dhaifu sana na haviwezi kutoa uongozi huo, inabidi tutegemee muungano wa wana harakati na wasomi ambao watatakiwa waunde forum maalum kwa ajili ya kutekeleza mass action hizo. Njia hii itaondoa zile shutuma za kawaida kuwa chochote kitachofanyika ni kutokana na mbinu za wapinzani.

2. Baada ya kupata chombo hicho, yaanze kufanyanyika maandamano ya amani. Kila panapotokea jambo ambalo linaenda kinyume na maslahi ya taifa watu washawishiwe kujitokeza na kuandama. Hatua hii itatatanguliwa na intensive education campaing kuuelimisha umma kuhusu haki zao za msingi na jinsi ya kuzidai.

3. Ikiwa serikali itajaribu kupinga au kuzuia maandamano hayo, au ikiwa yatafanyika kwa muda mrefu bila kutoa results, hapo ndio gear ya pili itatumika ya maandamano yatayoambatana na kuingia mitaani.

4. Ikiwa mpaka hapo bado mambo yatakuwa si shwari basi yaanze mapambano ya dhahiri. Kwa hali ilivyo sasa hata askari nao wanaweza kushawishiwa kuunga mkono umma kwani wengi wao pia nao wanakerwa na matokeo ya uhalifu unaoendelea.
 
Mkuu BUBU ATAKA KUSEMA, achana na MTANZANIA, tumemwelewa! He is simply stupid! Anataka kutatua matatizo ya Tanzania kwa remote control, akiwa London na kwa maelekezo ya mafisadi!

Angalia usije ambiwa una wivu wa kijinga! Mafisadi wananguvu za ajabu....RA amekuja na mpya hataki tena majaji ila uchunguzi mpya kama yeye ni Fisadi ama sio......RichMonduli. Naanza kumwelewa Obama Africa tuna kosa strong institutions, sheria hakuna, mahakama ndiyo hivyo tena, mtu mmoja mwenye pesa za wizi anauwezo wa kufanya chochote. Wengine tuliowategemea wanakuja na idea tufukie mashimo tusonge mbele jamani....!

Mungu ibariki Tanzania.
 
Duh leo tangu asubuhi nilikuwa naipitia hii thread kwa makini sana sikupenda kuchangia ila kufyonza elimu taratibu.
Napenda kuwapongeza wachangiaji wafuatao.
[1] Bubu Ataka kusema
[2] Masanilo
[3] mzee Mwanakijiji
[4] Mkandara
[5] Steve D

Naomba tusikate tamaa tuendelee kupiga kelele kwa nguvu zetu zote hadi kieleweke.

Hebu nami niungane nawe ila namuongeza FME; nina siku nyingi bila kuingia jamvini na nikutokana na utumbo wa baadhi ya mafundi ucungo humu ndani
 
Alichokifanya Selelii ni kutuwekea hadharani mgogoro wa mafahali wawili, JK na Lowasa. Ina maana JK alimtosa rafikiye Lowasa kukubali ripoti iwekwe hadharani ili kummaliza kisiasa maana alishaanza kumfunika. Lowasa awali hakufahamu kuwa mwenzie alikuwa na ripoti ile mwezi mmoja kabla, hapo ndipo senema yetu ilipo, tungoje na kuona
 
Tungeenda hatua kwa hatua.

1. Kila mass action lazima iwe na maandalizi na uongozi. Kwa kawaida haya hufanywa na vyama vya upinzani. Kwa kuwa nchini kwetu vyama hivyo ni dhaifu sana na haviwezi kutoa uongozi huo, inabidi tutegemee muungano wa wana harakati na wasomi ambao watatakiwa waunde forum maalum kwa ajili ya kutekeleza mass action hizo. Njia hii itaondoa zile shutuma za kawaida kuwa chochote kitachofanyika ni kutokana na mbinu za wapinzani.

tk umegusa mojawapo ya ukosoaji wangu wa Chadema; kwamba kama chama cha upinzani kimeshindwa kutoa uongozi kwenye mass action zaidi ya kutumwagia namba za matatizo ya nchi yetu na kutushawishi akili kwa kitu ambacho tayari tumeshashawishika!
2. Baada ya kupata chombo hicho, yaanze kufanyanyika maandamano ya amani. Kila panapotokea jambo ambalo linaenda kinyume na maslahi ya taifa watu washawishiwe kujitokeza na kuandama. Hatua hii itatatanguliwa na intensive education campaing kuuelimisha umma kuhusu haki zao za msingi na jinsi ya kuzidai.

Hapa unazungumza; lakini siyo Chadema wala CUF vyenye ubavu huo; wote wanaamini kuwa Watanzania hawapendi confrontational politics hivyo wanazungumza majukwaani kama wahubiri! Angalau wahubiri hutoa nafasi mwishoni za "kukata shauri".
3. Ikiwa serikali itajaribu kupinga au kuzuia maandamano hayo, au ikiwa yatafanyika kwa muda mrefu bila kutoa results, hapo ndio gear ya pili itatumika ya maandamano yatayoambatana na kuingia mitaani.

I love you for this; Chadema hawawezi haya ndio maana wameanza kugeuka na wataendelea kuwa irrelevant. CCM ingetikisika na nchi ingeamka kama kungekuwa na uongozi wa namna hiyo. Kwani ulimsikia Zitto, Mbowe au Slaa lini wamepanga maandamano ya kuishinikiza serikali zaidi ya kuwaita waandishi wa habari na kuwamwagia Data!?

4. Ikiwa mpaka hapo bado mambo yatakuwa si shwari basi yaanze mapambano ya dhahiri. Kwa hali ilivyo sasa hata askari nao wanaweza kushawishiwa kuunga mkono umma kwani wengi wao pia nao wanakerwa na matokeo ya uhalifu unaoendelea.

Wananchi wanayo haki ya msingi ya kuikataa serikali dhalimu hata kwa nguvu! Ndivyo yalivyotokea South Africa. Thanks for this ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom