Sekta binafsi iunge mkono upinzani waziwazi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
hili ni mojawapo ya maswali ambayo bado sijapata majibu yake kwa hakika. Mara nyingi tumeona jinsi sekta binafsi (makampuni kadha wa kadha na watu binafsi) wakiunga mkono chama tawala aidha kwa kukichangia au kwa kujiunga nacho au kushiriki katika miradi yake bila hofu yoyote ile wakiamini ni haki yao ya kidemokrasia.

Tumeona makampuni yakitoa misaada kwa wabunge wa chama tawala bila wasiwasi wowote wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wanatimiza jukumuu lao la kiraia (civic duty).

Hivyo utaona kampuni kama Zain inaenda kutoa misaada ya vitabu kwa mbunge wa CCM huko Mbozi, au kampuni nyingine ikitoa misaada inayohusisha wanasiasa wa chama tawala.

Lakini kitu kimoja kinachokosekana sana ni makampuni makubwa na yenye ujiko kuunga mkono upinzani au jitihada za wapinzani. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiangalia kuona kampuni kama Zain, Vodacom, IPP, Quality Group n.k zikienda kwenye majimbo ya wapinzani na wakisimama pamoja na wabunge wa upinzani kutoa misaada ya aina mbalimbali au kudhamini shughuli zao.

Sijaona kama CUF wakiandaa kongamano lao pale Arusha kampuni kama TBL itakuwa tayari kuzamini, au kampuni kama NSSF kujitangaza pale kibiashara au kuvutia wanachama zaidi.

Hivyo naanza kujiuliza kuna ubaya gani kwa makampuni makubwa kuonekana na wapinzani kama kwa kufanya hivyo kutatangaza makampuni hayo, kuwapatia wateja wengi na kuonesha kuwa hazina mlengo fulani wa kisiasa?

Je kampuni binafsi au mtu binafsi mwenye uwezo wa kifedha au kibiashara akionekana anaunga mkono chama cha upinzani waziwazi kuna tatizo gani katika utawala wakati tunajua wafanyabiashara wengi wakubwa tu wamekuwa wakiunga mkono CCM pasipo kificho?

Je ni kwanini hakuna wafanyabiashara wakubwa ambao wamejitokeza kujiunga na chama chochote cha upinzani kwa wazi (ukiondoa wachache ambao wamefanya hivyo hadi hivi sasa).

Kimsingi ninachouliza ni kuwa; je ni wazo zuri kwa sekta binafsi kuonekana wanasupport, kufagilia au kwa namna ya wazi kabisa kuunga mkono juhudi za upinzani kuibwaga CCM?
 
Watanzania waanze kukataa biashara ambazo wanaona haziwasaidii kimaisha. Economic boycot basi. Kama hawasaidii jamii yako usifamye biashara nao.
 
Mwanakijiji
Hoja yako ni nzuri sana na ina maana.
Hakuna ntu asiyetaka tufikie maturity hiyo uliyoisema kwenye hoja yako. Nafikiri pia kuwa wapo wafanyabiashara wengi sana wanaopenda kuwa wafuasi na supporters wa upinzani.
LAKINI
CCM ndiyo Tatizo!!!!!!!!!!!!!
CCM wanawatisha wafanyabiashara na wamiliki wa makampuni ya kibiashara kuwa wakionyesha kutokuiunga mkono, basi serikali itawabana na hata kuwafilisi.
Kumbuka Mhe. Fredrick Sumaye alikwenda Moshi wakati fulani akawaambia wafanyabiashara kuwa Mtu anayetaka biashara yake inyooke basi atundike Bendera ya CCM.
Wapo watu kadhaa ambao kwa kweli wameshindwa kabisa kuendesha biashara kutokana na kunyanyaswa kwa vile tu hawaifagilii CCM.

Hoja ya Pili ni kuwa upo upendeleo wa dhahiri kwa watu wanaoishabikia CCM. Watanzania wengi wanapenda sana kupendelewa. Hata kama upendeleo wanaopewa una thamani ndogo kuliko haki yake halali wao hawapotezi muda kupima between lines na kujua ukweli. Wale wote wanaopenda kupendelewa wanajilazimisha kuishabikia CCM ili waendelee kufaidi wanachokiona kuwa upendeleo.

All in all siasa za kistaarabu haziwezi kufanyika Tanzania kabla ya CCM kuondolewa madarakani ama labda sana waondokane na siasa za kihasama na ukale.
 
kwenye nchi ambayo chama kinatukuzwa kuliko TAIFA!!!!mambo haya sio ajabu. tumeaminishwa kuwa kuipinga CCM ni kuipinga TANZANIA!!na hili linasimamiwa na dola kwa nguvu zote sasa what do you expect? hata hoa wapinzani wenyewe wanaonekana WAASi, makampuni yanaogopa........na huo ndo ukweli huwezi ku risk biashara yako kwa kujiingiza kwenye ugomvi na serikali
 
Nadhani wapo wenye nia ya kusaidia upinzani waziwazi lakini historia inawaogopesha.Pengine kuna wanaokumbuka vizaazaa vilivyomwandama Bakhresa kwa support yake kwa CUF...bila kumsahau yule mchimba madini wa Arusha "Askofu".Kampuni ikionyesha tu dhamira yake ya kusaidia upinzani,next day TRA wanabisha hodi kutafuta sababu ya kukwamisha biashara hiyo.Nchi inaendeshwa kisiasa (isomeke ki-CCM) mno.

Lakini tunaweza kwenda mbali zaidi kuiangalia the so-called sekta binafsi.Mengi ya makampuni binafsi yanahusishwa na uharamia unaofanywa na viongozi wa chama tawala.It goes without saying kwamba makampuni ya aina hiyo hayawezi kamwe kuwasaidia wapinzani kwani yanaelewa bayana kuwa kuimarika kwa upinzani ndio kiama kwa makampuni hayo.Sitarajii kuona Zain (isomeke Celtel) inayotuhumiwa kuendeshwa kinyemela kwa mitambo ya TTCL,au Vodacom ya RA,nk wakitoa mchango kwa chama cha upinzani.

Safari bado ni ndefu sana kwani kuna wengi wanaotamani kuiona CCM ikitawala milele ili nao waendelee kufanya biashara zao kana kwamba nchi ni yao pekee.
 
Wengi wa wafanyabiashara wanaosupport CCM wanafanya hivyo wakiwania fursa fulani. Wanajua kuwa chengewe ndicho kimeshika mpini na kina uhuru wa kumkatia pande yeyote anayeonekana kuwa anafaa (siyo anastahili) kukatiwa.
Madaraka iliyonacho chama tawala kupitia serikali yake ni makubwa kiasi kwamba wakati mwingine yanawatisha wafanyabiashara ambao mioyo yao ipo kwa upinzani.
tassisi kama NSSF, zinajichukulia kama sehemu ya cahama tawala kwa sababu zipo chini ya serikali inayoongozwa na chama husika.
mwisho nikumbushe usemi wa Sumaye kwa wafanyabishara: Ukitaka mambo yako yanyooke...
 
Nadhani wapo wenye nia ya kusaidia upinzani waziwazi lakini historia inawaogopesha.Pengine kuna wanaokumbuka vizaazaa vilivyomwandama Bakhresa kwa support yake kwa CUF...bila kumsahau yule mchimba madini wa Arusha "Askofu".Kampuni ikionyesha tu dhamira yake ya kusaidia upinzani,next day TRA wanabisha hodi kutafuta sababu ya kukwamisha biashara hiyo.Nchi inaendeshwa kisiasa (isomeke ki-CCM) mno.

Lakini tunaweza kwenda mbali zaidi kuiangalia the so-called sekta binafsi.Mengi ya makampuni binafsi yanahusishwa na uharamia unaofanywa na viongozi wa chama tawala.It goes without saying kwamba makampuni ya aina hiyo hayawezi kamwe kuwasaidia wapinzani kwani yanaelewa bayana kuwa kuimarika kwa upinzani ndio kiama kwa makampuni hayo.Sitarajii kuona Zain (isomeke Celtel) inayotuhumiwa kuendeshwa kinyemela kwa mitambo ya TTCL,au Vodacom ya RA,nk wakitoa mchango kwa chama cha upinzani.

Safari bado ni ndefu sana kwani kuna wengi wanaotamani kuiona CCM ikitawala milele ili nao waendelee kufanya biashara zao kana kwamba nchi ni yao pekee.

nikweli kabisa kaka,
kwanza makampuni yenyewe yanamilikiwa(infull or partial) na viongozi wa CCM!!!katika hali hii huwezi kutegemea wasaidie upinzani. jiulize hivi kweli CASPIAN au TICTS au PRECISION za RA,Kara na Mramba au TANPOWER ya YONA na Mkapa zitasaidia upinzani kwa faida gani?? AU makampuni ya madini yanayopewa mikataba ya Chee na CCM kweli yataweza kusupport upinzani?????

kufika huko ni bado sana!!!!ila siku moja tutafika

Mungu Ibariki TZ
 
Heshima mbele.... Tatizo jingine ni wale majamaa wanaitwa TRA..... Tukumbuke kuwa sekta binafsi hapa nyumbani asilimia kubwa ni wakwepaji wazuri wa kulipa kodi!! Lakini ukiwa karibu na kutoa vijisenti kwa wenye nchi then unalindwa in kind, sasa pale utakapojifanya kuwapa upinzani vijisenti vyako then madudu yako yote wale jamaa wa TRA wanayaibua na wakati mwingine kuweka "extra watch" in your dealings!!

Ni ugonjwa ambao bahati mbaya sio rahisi kuutibu manake umejikita haswa!!
 
I do have different approach kwenye issue. Nadhani kuwaachagulia sector binafsi nani wamfund ni kuenforce ujamaa. Sector binafsi wana haki ya kutoa msaada (social responsibility) kwa mtu, watu, au kundi lolote walitakalo as long as it's with in their policy.

Kumbukeni ya kwamba sector binafsi inafahamu hatari ya kwenda different ways na chama tawala. Moja ya factor zinazo athiri Mcroenveronment ya kampuni ni Political Influance. Na Hii ni kwa nchi yoyote ile duniani. Corporate responsibility mara zote zina favor chama tawala sababu ya kurely kwenye payback. Unadhani wakianza kucheza na CCM kisha CCM wakaamu kupandisha tax kwa kupitia bunge undhani nani will be affected? Kampuni binafsi hazipo pale kufavor kundi la watu bali TO MAXIMIZE SHARE HOLDERS WEALTH. Hivyo kama mmoja ya njia ni kupet CCM back, guess what they will pet.

Nadhani kupoint fingure kwa kuwaambia Zain au Voda society gani waisaidie ni wrong, sababu wao wana policy and regulation zao.
 
Anzisheni fundrising ambayo haitabagua mwenye pesa na asiye na pesa, kila mwenye kidogo awachangie kwa uwezo wake.
 
Vilevile kuna ishu ya kupata tenda/kazi za serikali..... Manake ukishaonyesha kuwa wewe ni smahbiki/mtoa misaada kwa chama cha Morani ambacho ni cha upinzani hukawii kufunga biashara/ofisi manake utakuwa "black listed" na kila ukiweka tenda basi unajikuta unatupwa nje au kuwekwa kapuni!!!!

Ndiyo Bongo yetu hiyo wakulu.....
 
I do have different approach kwenye issue. Nadhani kuwaachagulia sector binafsi nani wamfund ni kuenforce ujamaa. Sector binafsi wana haki ya kutoa msaada (social responsibility) kwa mtu, watu, au kundi lolote walitakalo as long as it's with in their policy.

Kumbukeni ya kwamba sector binafsi inafahamu hatari ya kwenda different ways na chama tawala. Hii ni kwa nchi yoyote ile duniani. Corporate responsibility mara zote zina favor chama tawala zones.

Nadhani kupoint fingure kwa kuwaambia Zain au Voda society gani waisaidie ni wrong, sababu wao wana policy and regulation zao.

Pamoja na mchango wako mzuri sana, tatizo la Tanzania ni kuwa vyama vya siasa havijitofautishi kwa itikadi na hivyo wafuasi kimsingi hawafuati itikadi. Ni rahisi kujua nini watafanya dems madarakani na Reps pia. Ni rahisi kujua nini watafanya Cons UK na Lab na hata lib dems. Kwetu ni vigumu sana.

Hivyo CCM imekuwa kama kinyonga, inabadilika kutokana na inavyoona hali ilivyo. Leo watakuwa na rhetorics za kijamaa, kesho neo liberals nk. Hivyo sekta binafsi so far inaona CCM ndio chama chao kwani wanaweza kukipindisha misingi yake kwa kuwapa michango.
Lakini sekta binafsi wanalalamika sana kuwa ni ghali sana kibiashara kuwa na CCM kwani inawachangisha kwa lazima na wakibisha wanawasumbua katika mambo ya leseni nk.

MwanaKijiji katika sekta binafsi inabidi kuwe na wana CCM, wana CHADEMA na wana CUF na wote wawe huru kuchangia chama watakacho.

Vilevile sheria zetu za kuchangia vyama na kampeni ziwe wazi aina ya michango na kiwango cha juu cha michango kutoka kwa kampuni moja au mtu mmoja. Kuna muswada unakuja Januari kuhusu 'campaign financing' inabidi tuuchangie vizuri ili kuweka misingi mizuri ya kisheria.

Ifikie wakati, mfanyabiashara akionewa eti kwa kuchangia upinzani aweze kwenda mahakamani na kuishitaki serikali. Hii itaondoa woga wa wafanyabiashara wetu.
 
Kuna tofauti ( au panapaswa kua na tofauti) kati ya CCM, Serikali
na Private sector... a clear cut difference otherwise tutakua kama mbwa
kufukuza mkia.

Kama alivyosema mchangiaji mmoja, katika hali ilioko Tanzania, ni vigumu
kuona hii tofauti na kwa kweli haki haitoweza kutendeka under these circumstances.

CCM, which is a party, has usurped the powers of the Govt(which is supposed
to be democratically elected by the people to serve them) hence creating an
environment of 'look behind your back if you dont tow the party line'. Ndiposa
kama wewe ni mwanabiashara na hutoi michango kwao, basi wanakutumia
TRA kukandamiza shughuli zozote za kibiashara.

Kisha katika haya mazingira ya kutatanisha sekta binafsi haitothubutu kutoa
hata senti tano towards the opposition coz doing so will mean a demise of
their businnesses.Kwa hivyo kama ni kuunga mkono upinzani they have to do
their moves in utmost secrecy so as to stay above water so to speak.
 
Ifikie wakati, mfanyabiashara akionewa eti kwa kuchangia upinzani aweze kwenda mahakamani na kuishitaki serikali. Hii itaondoa woga wa wafanyabiashara wetu.

It will take a whole change of attitude by CCM to get to this.
 
Hili swali ni muhimu sana kwa sababu, wakati wananchi wa kawaida wanafanya protest kwa ajili ya mafao yao wananchi makampuni hayana wasiwasi kwa sababu kuna sera ambazo wanazipenda ndani ya CCM.

Swali ambalo binafsi ningependa kuwauliza watu wa sekta binafsi ni sera gani au maamuzi gani ya CCM ambayo yanafanya kazi zao kuwa ngumu, kupunguza faida au kuwabebesha mzigo mzito kuliko inavyostahili? Tukishajua hayo wapinzani au chama cha upinzani kinakuja na sera kinyume cha hizo.

Lakini zaidi sekta binafsi lazima ijue ina interest katika welfare ya taifa zima. Yawezekana ni vizuri kampuni kutoa msaada wa kujenga kisima, darasa au kutoa vitabu. Lakini kwa kadiri makampuni yanatoa vijimisaada hivi aidha kwa kuombwa na wana siasa au kwa kuona umuhimu wake wao wenyewe hawapushi serikali na wananchi kufanya vile vinavyotakiwa kufanywa nao.
 
Anzisheni fundrising ambayo haitabagua mwenye pesa na asiye na pesa, kila mwenye kidogo awachangie kwa uwezo wake.

Naam Mama,

Kuna jamaa amependekeza something similar .... Zitto, Mnyika na viongozi wengine wa vyama vya upinzani it's time to wake up and go to work ... binafsi nimebakia kuwa mwanachama wa CCM kwa jina tu, na kama uongozi uliopo hautarudi kwenye mstari nitakuwa tayari kuwa upande wenu (just being honest here) .... anyways kuna jamaa kapendekeza ifuatavyo:

It's time to capitalize on the euphoria.
CCM is our version of Republicans, and Kikwete is our George Bush.
We can build a grassroots movements here too.
Trust you can craft a moving central theme for change in Tanzania.
Tanzanians certainly want change.
Then use an SMS-based donations collection scheme.
And as people donate they become more hooked into the political process
Thus doing what they can to make sure their donation isn't in vain

We have 10,000,000 mobile users.
If you can motivate at least 1,000,000 mobile users to donate Tshs 1,000 per month that will be Tshs, 1,000,000,000/- per month.
I don't know campaign maths, but don't you think it will be enough to run a strong campaign against CCM?

As for CCM, I doubt if ordinary Tanzanians will be willing to donate to a party which is protecting thieves.

Time to do away with Big Donors. Big Donors are shy and worried of victimization from the state.
But SMS donors will never be afraid, because after all, they remain anonymous.

It's up to you guys to come up with a compeling message to fire people up.
 
Nakuunga mkono na mguu. Hii habari ya wafanyabiashara madhara yake ni kuwa wengi wao (wafanyabiashara) wanaangalia faida, isiwe ya leo basi iwe ya kesho au kesho kutwa. Na ndhio kinachowatokea puani sisiemu kwa sasa. MaEPA scandals zote nyuma yake wako wafanyabiashara walioidhamini.

Je mchango wetu sisi wananchi tusio na vipato vikubwa hauthaminiwi na wanasiasa? Lau wangejua haba na haba hujaza kibaba.

NB: kama kuna sekta binafsi kama wanaweza kuwa fair enough na kuwadhamini, it will be very well and also good.
 
The current position of opposition makes it a rather stupid move to openly support them, speaking from the businessman point of view, in particular because businesses tend to only care about the interests of their shareholders (as they should). This may be under the banner of social responsibility, corporate responsibility, what ever you might call it.. Big business does it only to ensure their image remains positive in the eyes of the public aka market.. Under CCM's dominance and almost negligible challenge ushered by the oposition, it makes little or no business sense to openly support the opposition.. And business sense is the chief concern of business entities, of course
 
don't you think it is the best interest of the business community to have a very good relationship with the opposition too just in case either a new party becomes the majority in the parliament or have unchecked power in the presidency?

Don't you think looking with the mentality of "right here, right now" is detrimental to the future or the success of the companies. They have to look beyond their own current levels of comfort?
 
The current position of opposition makes it a rather stupid move to openly support them, speaking from the businessman point of view, in particular because businesses tend to only care about the interests of their shareholders (as they should). This may be under the banner of social responsibility, corporate responsibility, what ever you might call it.. Big business does it only to ensure their image remains positive in the eyes of the public aka market.. Under CCM's dominance and almost negligible challenge ushered by the oposition, it makes little or no business sense to openly support the opposition.. And business sense is the chief concern of business entities, of course

You just nailed it! The only opposition we have in Tanzania is of parties that talk about policies they cant impliment and the one whose leaders leave constituencies just that they can acquire fame by running for the president. No reasonable company will invest their money in such parties.The opposition is unstrategic, selfish and naive in the eyes of any mentally-sound citizen. On top of that, companies have eyes - they see just like anyone would see that the chances any of the current opposition party in their current political approaches will ever acquire majority of sits in the parliament or even get close to the state house.so why inject their money in such vain mission?!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom