Sekretarieti ya chadema na wanapotoka

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
Nilikuwa napitia tovuti ya CHADEMA leo hii. Nikawa nataka niijue Sekretariati ya CHADEMA nikakuta majina ya wajumbe wa Sekretariati ila cha kushangaza nikakuta wajumbe John Mnyika (mbunge wa Ubungo) na Halima Mdee (Mbunge wangu wa Kawe) wanaonyeshwa kama ifuatavyo:

Mkurugenzi Mambo ya Nje
John John Mnyika (31)
Kutoka Mwanza
Afisa Mwandamizi Sheria

Halima James Mdee (33)
Kutoka Same, Kilimanjaro
halima@chadema.or.tz

Mimi najua kwamba Mnyika anatoka Ubungo na Mdee anatokea Kawe sasa inakuwaje inaonyeshwa kwamba Mnyika anatoka Mwanza na Mdee anatoka Same, Kilimanjaro? Kuna mantiki gani au ni kuonyesha wajumbe wametoka sehemu gani ya kuzaliwa?

Naomba msaada tafadhali

Mambo mengine ni kutumia akili kidogo tu! Hili halihitaji kuvua gamba
 
Hiyo akili ya kutumia hapa sina ndio maana nikaomba wenye akili kama wewe mnisaidie. Ubaya wenu ni kwamba mtu akiulizia tu jambo lolote la CHADEMA humu ndani mnamuona kama ametumwa ama ni mpinzani. Sisi wengine hatuna ushabiki wa chama ila tunajaribu kuangalia umakini wa hivyo vyama ili tupate vyama bora na siyo bora vyama.
 
Ha ha ha Mchungaji Bwana! Umenifurahisha sana. Ni sawa na Makongoro Mahanga akikwambia anatoka Mara utabisha? Au Eugen Mwaiposa akikwambia anatoka Mbeya wakti ni mbunge wa Ukonga au Mpendazoe kutoka kisha halafu kuwa Mgombea wa Segerea, Hussein Mwinyi kuwa Mkuranga baadae Zanzibar n.k ni common sense
 
Nilikuwa napitia tovuti ya CHADEMA leo hii. Nikawa nataka niijue Sekretariati ya CHADEMA nikakuta majina ya wajumbe wa Sekretariati ila cha kushangaza nikakuta wajumbe John Mnyika (mbunge wa Ubungo) na Halima Mdee (Mbunge wangu wa Kawe) wanaonyeshwa kama ifuatavyo:

Mkurugenzi Mambo ya Nje
John John Mnyika (31)
Kutoka Mwanza
Afisa Mwandamizi Sheria

Halima James Mdee (33)
Kutoka Same, Kilimanjaro
halima@chadema.or.tz

Mimi najua kwamba Mnyika anatoka Ubungo na Mdee anatokea Kawe sasa inakuwaje inaonyeshwa kwamba Mnyika anatoka Mwanza na Mdee anatoka Same, Kilimanjaro? Kuna mantiki gani au ni kuonyesha wajumbe wametoka sehemu gani ya kuzaliwa?

Naomba msaada tafadhali

Wewe haujui kuwa DSM tumekuja kutafuta hela tu na ndio maana tukifa wengine tunarudishwa makwetu.
 
Jijini sote tumekuja tu KUCHUMA ila kila mmoja wetu tunavyo vijiji vyetu kulikozaliwa Mababu zetu. Labda wewe mwenzetu ambaye kijijini kwenu ni kwa Aziz Ali Mbagala.

Nilikuwa napitia tovuti ya CHADEMA leo hii. Nikawa nataka niijue Sekretariati ya CHADEMA nikakuta majina ya wajumbe wa Sekretariati ila cha kushangaza nikakuta wajumbe John Mnyika (mbunge wa Ubungo) na Halima Mdee (Mbunge wangu wa Kawe) wanaonyeshwa kama ifuatavyo:

Mkurugenzi Mambo ya Nje
John John Mnyika (31)
Kutoka Mwanza
Afisa Mwandamizi Sheria

Halima James Mdee (33)
Kutoka Same, Kilimanjaro
halima@chadema.or.tz

Mimi najua kwamba Mnyika anatoka Ubungo na Mdee anatokea Kawe sasa inakuwaje inaonyeshwa kwamba Mnyika anatoka Mwanza na Mdee anatoka Same, Kilimanjaro? Kuna mantiki gani au ni kuonyesha wajumbe wametoka sehemu gani ya kuzaliwa?

Naomba msaada tafadhali

Unaulizia kuhusu Mnyika kutoka Mwanza na si Ubungo anakowakilisha,mbona hauulizi juu ya Mdee kutoka Same angali yeye anaiwakilisha Kawe,na je unajua ni nini kimezingatiwa hapa?uzawa,kabila ama uwakilisha?maana waweza kuwa mchaga lakini umezaliwa na familia imehamia sehemu nyingine tofauti,hujawahi ona?
 
Hiyo akili ya kutumia hapa sina ndio maana nikaomba wenye akili kama wewe mnisaidie. Ubaya wenu ni kwamba mtu akiulizia tu jambo lolote la CHADEMA humu ndani mnamuona kama ametumwa ama ni mpinzani. Sisi wengine hatuna ushabiki wa chama ila tunajaribu kuangalia umakini wa hivyo vyama ili tupate vyama bora na siyo bora vyama.

Mkuu, mbona unamjibia mtu kwa maelezo marefu katika swali fupi?
 
Kimbunga naona kama jibu la swali lako liko kwenye title ya hii thread. naomba kunukuu..."Sekretarieti ya chadema na wanapotoka". Hata hivyo nikutoe wasiwasi kwamba both Mwanza na Kilimanjaro zimo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Labda mantiki na muktadha wa swali langu haukueleweka vizuri. Nimepitia sekretariat za vyama vingine kama CCM na CUF sikukuta wajumbe wake wakionyeshwa sehemu wanazotoka lakini kwa CHADEMA nikakuta wanaonyesha sehemu wanakotoka yaani sehemu walikozaliwa (ambapo unaweza ku guess makabila yao) kwa hiyo nikashangaa. Sikujua mantiki ya kuonyesha wanakotoka au ina maana Sekretariat ya CHADEMA ina uwakilishi wa mikoa au ni kuonyesha tu kwamba sekretariat inaundwa na wajumbe toka mikoa mbalimbali ili kuondoa dhana ya ukabila au ukaskazini ambao huwa unaongelewa kuhusu CHADEMA? Kwa maana hiyo nilitaka kujua tu mantiki ya kuonyesha kuwa wajumbe wanatoka wapi. Nadhani walikuwa na mantiki yao kwani vinginevyo wangeweza tu kuandika majina na vyeo vyao bila kuonyesha wanakotoka.
 
Kwa hiyo umestusthwa na makabila, sio?

Siwezi kustushwa na makabila kwa kuwa kwa kuandika walikotoka siwezi kujua exactly makabila yao ni yapi ila naweza tu ku guess kwa mfano kwa kuwa Mdee anatoka same basi anaweza kuwa Mpare au kwa kuwa Mnyika anatoka Mwanza anaweza kuwa Msukuma. Lakini guess yangu inaweza kuwa totally wrong Mdee anaweza kuwa mchaga, Mtaita au hata Mmasai na Mnyika akawa Mkurya, Mzinza ama Mkerewe!! Mantiki yangu nilitaka tu kujua kama wameweka mahala wanapotoka kwa kuwa sekretariat in uwakilishi wa kimkoa ama ni kuonyesha tu kwamba wanachama wanatoka maeneo mbalimbali ya nchi na haina uhusiano wa uwiano wa kiuwakilishi wa kimkoa. Basi. Ningejua ofisi za CHADEMA ziko wapi ningeenda kuulizia kimyakimya na kusingekuwa na haja ya kuulizia kupitia humu
 
crap crapist:evil: we afande vipiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Unashangaa nini? Hujui maana ya uwakilishi? Uwakilishi sio ukabila. Kamanda DR. Slaa anaweza kuwa mbunge wa shy, kitu hicho nakiombea sana.
 
Labda mantiki na muktadha wa swali langu haukueleweka vizuri. Nimepitia sekretariat za vyama vingine kama CCM na CUF sikukuta wajumbe wake wakionyeshwa sehemu wanazotoka lakini kwa CHADEMA nikakuta wanaonyesha sehemu wanakotoka yaani sehemu walikozaliwa (ambapo unaweza ku guess makabila yao) kwa hiyo nikashangaa. Sikujua mantiki ya kuonyesha wanakotoka au ina maana Sekretariat ya CHADEMA ina uwakilishi wa mikoa au ni kuonyesha tu kwamba sekretariat inaundwa na wajumbe toka mikoa mbalimbali ili kuondoa dhana ya ukabila au ukaskazini ambao huwa unaongelewa kuhusu CHADEMA? Kwa maana hiyo nilitaka kujua tu mantiki ya kuonyesha kuwa wajumbe wanatoka wapi. Nadhani walikuwa na mantiki yao kwani vinginevyo wangeweza tu kuandika majina na vyeo vyao bila kuonyesha wanakotoka.
Duh! nilikuwa nacheka sana ila hapo kuna pointi
 
Hiyo akili ya kutumia hapa sina ndio maana nikaomba wenye akili kama wewe mnisaidie. Ubaya wenu ni kwamba mtu akiulizia tu jambo lolote la CHADEMA humu ndani mnamuona kama ametumwa ama ni mpinzani. Sisi wengine hatuna ushabiki wa chama ila tunajaribu kuangalia umakini wa hivyo vyama ili tupate vyama bora na siyo bora vyama.

unapotoka ni pale ulipozaliwa sio unapofanyia kazi. hao wanaishi DSM LAKINI WAMETOKA MWANZA NA kILIMANJARO. Nini kigumu hapa?
 
It doesnt make sense kusema Mnyika anatoka Mwanza kwani anawakilisha Mwanza si angegombea huko Mwanza mwanza basi?
 
Mi ninavyoona tayari umeshamaliza wew mwenyewe,sina la ziada.
 
Nilikuwa napitia tovuti ya CHADEMA leo hii. Nikawa nataka niijue Sekretariati ya CHADEMA nikakuta majina ya wajumbe wa Sekretariati ila cha kushangaza nikakuta wajumbe John Mnyika (mbunge wa Ubungo) na Halima Mdee (Mbunge wangu wa Kawe) wanaonyeshwa kama ifuatavyo:

Mkurugenzi Mambo ya Nje
John John Mnyika (31)
Kutoka Mwanza
Afisa Mwandamizi Sheria

Halima James Mdee (33)
Kutoka Same, Kilimanjaro
halima@chadema.or.tz

Mimi najua kwamba Mnyika anatoka Ubungo na Mdee anatokea Kawe sasa inakuwaje inaonyeshwa kwamba Mnyika anatoka Mwanza na Mdee anatoka Same, Kilimanjaro? Kuna mantiki gani au ni kuonyesha wajumbe wametoka sehemu gani ya kuzaliwa?

Naomba msaada tafadhali

.
Kwani hao wajumbe wa sekretarieti wanatakiwa kuwa wangapi ili labda wawakilishe ama ukanda, mkoa, wilaya jimbo la ubunge au kata?
.
 
Back
Top Bottom