Sekretariet ya ajira wizi mtupu

Usilalamike, next time cha kufanya uki-apply nafasi ya watu 3 wakaita 100 usiende, kama ndiyo unafikiri ni kupotezeana muda. Uwezo wako wa kufikiri na kuchambua mambo ndio unaokufanya ulalamike. na kama hutabadili namna ya kuchambua mambo, interview zote utakuwa unabigwa chini. Ningekuwa natafuta nafasi yoyote ya kuajiri nisingekuajiri kwa kuwa unaonyesha uwezo mdogo wa kuchanganua mambo.

Anaogopa competition!
 
Binafsi sina tatizo kabisa na utaratibu wa kuita watu wengi katika interview kwakuwa hiyo inawasaidia kudistinguish wenye GPA genuine na za kimagumashi, unaweza kukuta mtu ana GPA Kali sana lakini kichwani hakuna kitu, ama uelewa wake hauendani na GPA aliyonayo kwenye makaratasi yake.

Ugomvi wangu na sekretarieti ya ajira ni kitu kimoja tu, wameshindwa kusimamia vizuri nafasi za ajira kwa watu wanaowapeleka katika mashirika ya umma. Kumekuwa na tabia ya uchakachuzi wa waajiriwa katika baadhi ya mashirika ya umma na baadhi ya idara za serikali. Nina mifano hai mitatu ya watu waliochakachuliwa ajira zao. Mmoja alipelekwa Ofisi ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali(NAOT), mwingine alipelekwa halmashauri ya manispaa ya Ilala na mwingine alipelekwa Tume ya takwimu ya Taifa (National Burea of Statistics).

Sekretarieti ya ajira iliwapelekea watumishi (Transport Officers wenye ordinary diploma) katika mashirikana na manispaa kama nilivyotaja juu, kama ambavyo walikuwa wameombwa na taasisi husika. Mmoja aliyepelekwa NAOT alikwenda kufanyiwa induction programme iliyofanyikia hoteli ya Girraffe kwa muda wa wiki tatu pamoja na waajiriwa wengine. Lakini baada ya kumaliza induction na kusaini mkataba wa kazi HR Manager akamueleza kwamba wao NAOT walikuwa wanataka mtu mwenye Advanced Diploma, kwahiyo akatakiwa asianze kazi kwanza hadi watakapowasiliana na sekretarieti ya ajira. Yule mtu akaamua kwenda kutoa taarifa katika sekretarieti na akajibiwa kwamba NAOT walitaka mtu mwenye ordinary diploma na ndiye ameombewa kibali cha ajira kutoka utumishi na kibali kimetoka. Baada ya kuendelea kufuatilia NAOT na sekretarieti ghafla sekretarieti wakageuka na kumwambia NAOT wametuma maombi ya kutaka waajiri mwenye advanced diploma kwahiyo ajira yake haipo tena.

Mwingine walimpeleka Ofisi ya statistics kuwa transport officer, baada ya kuripoti na kukaa wiki moja akaambiwa nafasi ya TO imefutwa kwahiyo hawahitaji tena transport officer, aliporudi kutoa taarifa sekretarieti wakasema watafuatilia, lakini hakuwahi kupata jibu lolote hadi leo hii.

Mwingine tena walimpeleka manispaa ya ilala kuwa transport officer, baada ya wiki mbili tangu alipoti kazini akaanza kufanyiwa mizengwe kwamba nafsi yake imebadilishwa kwahiyo hawatamuhitaji tena, wakamrudisha sekretarieti ya ajira na hajawahi kupangiwa kazi mahali pengine tena.

Katika matukio yote haya matatu baada ya kuyafuatilia, wahusika wamegundua mambo yafuatayo;

1.NAOT wameajiri transport officer mwingine mwenye ordinary diploma kama waliyemkataa, lakini aliyeajiriwa ni mtoto mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dsm, na ni kabila moja na HR Manager wa NAOT.

2. National Bureau Of Statistics waliajiri transport officer mwingine ambaye ni mtoto wa mhadhiri mmoja mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

3. Manispaa ya Ilala nayo inasemekana kuajiri mtu mwingine lakini details zake hazijapatikana kikamilifu.

Baada ya mambo haya yote kutokea wahusika walikwenda kulalamika sekretarieti ya ajira juu ya uchakachuzi wa nafasi zao za ajira waliofanyiwa, bahati mbaya sana hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa zaidi ya kuwapa matumaini tu kwamba wanalifuatilia. Na bahati mbaaya sana yule HR Manager wa NAOT naye ni mjumbe katika panel ya sekretarieti ya ajira inayoketi kusahili waombaji wa ajira kwahiyo anaweza kuwa anatumia nafsi yake kufanya mambo kinyume na taratibu ili kutoa favour kwa watu wake.

Kama sekretarieti hawatobadilika bado siamini kwamba ajira zitakuwa za haki bali utakuwa ni muendelezo wa kujuana, kama huko nyuma tulikotoka.
 
Dogo Kikomelo kuhusu ratio hapo umechemka rudi shule ukajifunze hesabu, ratio ya 3:1 ndy nini? sahihi ni 1:3
 
Watanzania kuweni makini na kulalamika, sijui mnataka mfanyiwe zuri lipi? hawajamaa wanapotangaza kazi, wanapokea maombi kibao! nafasi tuseme wametangaza mbili, wanapokea maombi 600! wanachokifanya nikuchagua waombaji wenye sifa na kuwaita kwenye usahili! wanataita wote wenye minimum qualification ili kuondoa malalamiko ya kudai wanashortlist kwa upendeleo! wanataka kila mtu awe na nafasi sawa ya kushindana! Kama kati ya maombi 600 waliyopokea, watu 400 wanasifa, basi wataitwa wote! Na wanatoa mtihan wa mchujo ili kupata watu bora! kwenye mchujo huo uwa wanabakiza ratio ya 3:1, kila nafasi moja inagombaniwa na watu watatu! kwa mfano kama wanatakiwa watu 2 basi wanaoenda kwenye oral watakuwa ni 6 tu, wale waliofaulu juu kuliko wote! Jamaa wako fair, kama ilibidi wabaki watu 6 ila matokeo yakawa kawa ivi, nimepanga kutokana na max kubwa, 90 ,87,86,85,84,83,83,83,83,83,82 na kuendelea...basi watakaoienda oral ni 10! kwa kuwa wa sita wamefungana! na kama watatu tu ndo wamevuka 50, na wengine wakapata chini ya 50 basi watakao piga oral ni watatu tu mana serikali haichukui chini ya 50.
Nina iman tumeelewana! wanaita watu wengi ili kuwa na uwanja mpana wa kupata watu wazur! kitu cha maana ni kujiandaa vyema kabla ya kwenda kwenye writen interview! hachen kulalamika, vilaza nyie!!!

Mkuu,
Umesema vema sana. Shughuli zangu kiasili zinaingiliana sana na Sekretariet ya Ajira. Hivyo najua kwa ukaribu namna jamaa wanavyofanya kazi. Wako fair sana. Wanawapa watu fursa sawa ya kupata nafasi ya ajira. Mliosoma Samoling mtatusaidia ni aina gani ya sampling method ambayo kila mtu/sampuli ina equal chance ya kuchaguliwa.

Kama unaulizwa maswali na unashindwa, then unalaumu, basi wewe ndo una matatizo. Nimeona majuzi wametangaza nafasi mbali mbali za kazi. Nimeomba. Kuna ambazo nina sifa. Na kuna ambazo sina sifa. Nataka nione itakuwaje.

Bwana Daudi na timu yake wanajitahidi kadiri wanavyoweza kwa kweli. Tatizo tulishazoea zamani ajira za Vimemo au kuibiwa maswali na kupewa. Jamaa wana Idara kabisa ya Quality Assurance ambayo inashughulika na kutunga mitihani. Wako makini sana. Hawacheki na mtu.
 
Tuwe makini tunapochangia mada, kiuhalisia kubali usikubali katika hizi interview ukiangalia kwa kina hakuna fair play waungwana, funguka! nlikua napita tu.
 
Back
Top Bottom