Sekondari 17 Singida kupata mtandao wa Intaneti

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Gasper Andrew ,Singida

MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohamed Gullam Dewji, ameahidi kutumia zaidi ya Sh50 milioni kugharamia uwekaji wa mtandao wa intaneti (Internet) kwa shule zote 17 za sekondari za Serikali, jimboni humo ili kusaidia wanafunzi na walimu kujisomea zaidi.

Mpango huo wa aina yake,utaanzia na shule tano ambazo tayari zina umeme, shule hizo ambazo ni pamoja na Mitunduruni, Mwenge, Dk Salmini Amour, Chief Senge,na Kindai,kila moja itapewa kompyuta 20 ili kufungua darasa maalumu kwa ajili ya wanafunzi na walimu kujifunzia.
Dewji maarufu kwa jina la ‘MO’ alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye kikao cha pamoja na walimu wa shule za sekondari za Manispaa ya Singida uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kanisa la Katoliki Misuna mjini hapa.

Alisema amefikia uamuzi huo kutokana na ukweli kwamba kupitia mtandao wa intaneti wanafunzi au mtu ye yote utamsaidia kujifunza mambo mengi.Aidha, alisema uamuzi huo umesukumwa pia na shule nyingi za sekondari za Serikali kukabiliwa na matatizo mengi yakiwamo vitabu vya kujisomea/kujifunzia.

“Kutokana na upungufu/uhaba wa vitabu vya kujisomea na mengine mengi, mimi mbunge wenu, nimeleta wataalamu wa intaneti kutoka Marekani ili watufungulie mtambo utakaowezesha shule zote za sekondari za Serikali zilizo na umeme, ziweze kujiunga na mtandao wa intaneti.
Dewji alisema hapo ndipo walimu na wanafunzi wanaweza kupata mambo mengi yatakayowasaidia kwenye masomo yao .

Source Mwananchi Gazeti
 
Kwani hao wana Singida waliandamana hadi wapate hizo privaleji? sisi wa hapa Arusha tunasubiri ratiba ya maandamano sijui itatoka lini.
 
Kwani hao wana Singida waliandamana hadi wapate hizo privaleji? sisi wa hapa Arusha tunasubiri ratiba ya maandamano sijui itatoka lini.

Lema + AM = wanaweza wakafanya zaidi ya MO, wanasubiri nini?
 
Wao wanangoja unaa tu, mambo ya maendeleo kama haya huwa kimyaa, hata kusifia hawataki. Utawaona sasa hivi, hao...
 
Lema + AM = wanaweza wakafanya zaidi ya MO, wanasubiri nini?

Nchi haiwezi kuendelea kwa kuwapa komputa wakati maji wanayokunywa si salama komputa si basic need kwa watanzania walio wengi hasa vijijini.kama yeye ana nia ya kusaidia apeleke wanafunzi wanaomaliza f6 watatu kila kijiji wakapate mafunzo ya miaka 2 hiyo 50ml ingekuwa na maana zaidi.Lakini kwa sasa huo ni ulaghai tu asubiri kibano chake 2015 time will tell , after all where is Rostam now
 
tatizo ni Maslahi ya walimu. utapeleka kila kitu kwenye hizo shule lkn km maslahi yao nio madogo wataishia kuuza tu hizo computer. baada ya miaka 3 tembelea hizo shule km utakuta kuna PC hata moja!
 
Wao wanangoja unaa tu, mambo ya maendeleo kama haya huwa kimyaa, hata kusifia hawataki. Utawaona sasa hivi, hao...
Wekeni sheria basi tusiwe tunachangia kwenye thread zenu...kwanza wewe ushawahi kufika hata shule moja iliyotajwa hapo juu? Mimi nimefika Dr Salimin...shule ina maabara mbovu kwa upande wa masomo ya sayansi ni bora angekarabati hizo laboratories kwaza ili wanafunzi waelewe kimatendo zaidi...internet itawasaidia nini?, nani atakuwa analipia hizo package?,nani atamanage wanafunzi wafungue site zinazoendana na masomo yao au wataachiwa wenyewe? Any way amefanya jambo zuri kwa upande mwingine maana members wa jf wataongezeka tuiadabishe serikali ya magamba...
 
Wao wanangoja unaa tu, mambo ya maendeleo kama haya huwa kimyaa, hata kusifia hawataki. Utawaona sasa hivi, hao...

Hizi ni kiasi kidogo sana na zinatokana na ukwepaji kodi katika biashara zake. Hamna haja ya kumsifu. Ni hela zetu hizo.
 
Wekeni sheria basi tusiwe tunachangia kwenye thread zenu...kwanza wewe ushawahi kufika hata shule moja iliyotajwa hapo juu? Mimi nimefika Dr Salimin...shule ina maabara mbovu kwa upande wa masomo ya sayansi ni bora angekarabati hizo laboratories kwaza ili wanafunzi waelewe kimatendo zaidi...internet itawasaidia nini?, nani atakuwa analipia hizo package?,nani atamanage wanafunzi wafungue site zinazoendana na masomo yao au wataachiwa wenyewe? Any way amefanya jambo zuri kwa upande mwingine maana members wa jf wataongezeka tkkuiadabishe serikali ya magamba...
<br />
<br />
Kwa ninavyozifahamu shule za serikali, ambozo nyingi ni shule za shule za kata, sijaona kama Mo KAFANYA KITU KIKUBWA ZAIDI HAPO, BORA ANGEBORESHA lABS KWANI WATOTO WANAFELI SANA MASOMO YA SAYANSI, ZAIDI YA HAPO HAPO KUNA SHULE WATOTO WANATEMBEA KM 15 KUIFUATA HIYO SHULE DAILY, KWANINI ASIWAJENGEE HOSTELS WATOTO WAKAPATA MUDA ZAIDI WA KUSOMA NA KUEPUKA TAMAA NA MIMBA ZA MAPEMA???
tATIZO NI KAMATI ZILIZOKAA NAE KUJADILI HILO, WENGGINE WATAFANYA MITAJI HAPO... MAANA UNAPOPELEKA COMP KWENYE SHULE AMBAYO MFUMO WA UMEMEME NI TATIZO.. HAPO KUNA MASUALA YA MAINTANANCE, UPDADING NA MENGINE MENGI... HIYO GHARAMA YA NANI? SHULE ZENYEWE WALIMU HAZINA
 
Wao wanangoja unaa tu, mambo ya maendeleo kama haya huwa kimyaa, hata kusifia hawataki. Utawaona sasa hivi, hao...

Sio kama watu hawataki kusifia FaizaFoxy ila wanajaribu kuvumilia huu u-chief Mangungo! Internet connection kwa shule za jimbo kwake huyu Dewji ni kitu kizuri lakini nataka nikueleze kuwa formula ya huu msaada ni sawa na ile ya wamerakani kwamba wamepata Uranium na wao wakatupa vyandarua vya mbu!

Ni lini Dewji alisimama bungeni akatetea hoja yoyote ya kijimbo na taifa? Kama ilivyo kwa wabunge wengi ccm, Dewji yuko bungeni kutetea wanasingida? au anawahitaji wanasingida ili wamuweke bungeni kwa 'shughuli maalum'? Hivi vyandarua sorry internet connection ndio tatizo kubwa walilo nalo wanasingida? Kwanza hizi shule zina umeme?
 
Kwani hao wana Singida waliandamana hadi wapate hizo privaleji? sisi wa hapa Arusha tunasubiri ratiba ya maandamano sijui itatoka lini.
<br />
<br />
kwakupenda vya dezo wabongo tunahtaji maendeleo ya kweli kutoka kwenye mfumo mzuri wa udhibiti wa fedha za serikali kamwe hii nchi haiwezi kuendelea kwa fedha za mifukoni kutoka kwa wabunge ingawa sio jambo baya, hvyo basi tusiwalaumu wale wabunge ambao wao hawafanyi majitoleo kama huyo Dewji hyo inatokana na wao kutokuwa matajiri, na kama unamponda LEMA kwakuwa hawezi kutoa kumpyuta kwahyo unataka nchi hii UBUNGE tuwape MATAJIRI TU.
 
7302atSingida.jpg


Sin'gida hapo lol
 
Viongozi wa CCM huwa hawako focused, hivi huyo ameangalia vipaumbele hivi kwanza? Je,



1. shule hizo zina walimu wa kutosha? 2. Kuna maabara kwa kila shule tena za kisasa? 3. kuna walimu wangapi wenye uwezo na internet/computer? 4. kuna umeme? 5. Madarasa yako poa? 5. Kuna madawati?
 
Back
Top Bottom