Seif Khatib: Kuzomewa Ni Gharama Ya Siasa

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Seif Khatib yuko Iringa. Yeye na msafara wake wamekuja Iringa katika kile kinachoitwa mkakati wa chama tawala kuwatuma makada wake nchi nzima kuondoa sumu waliyopewa wananchi kutokana na ziara za viongozi wa vyama vinne vya upinzani nchi nzima wakiongozwa na Mbunge Zitto Kabwe ambayhe hoja yake ya Mkataba wa Madini wa Buzwagi ilimwacha akionyeshwa mlango wa kutokea nje ya Bunge na hatimaye kumpa umaarufu mkubwa kama mwanasiasa.

Jioni ya jana pale Ukumbi wa Siasa ni Kilimo, Waziri Khatib aliongea na Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa, Wajumbe wa Halmashauri Kuu na watendaji wa kata.

Mh. Seif Khatib anasema:

-Kiongozi kuzomewa ni gharama ya siasa. Ukiingia kwenye mchezo wa siasa hujiandae kwa hilo.
-Sisi tuna kazi ya kufanya, wapinzani hawana kazi
-Sisi tuna maswali ya kujibu 2010, wapinzani hawana
-Wapinzani hawapendi tufanikiwe
-Msiingie kwenye mtego wa wapinzani
-Wapinzani wapuuzeni, simamieni ilani ya chama
-Tuna ilani inayotekelezeka

Kwa habari zaidi katika picha, tembelea; http://mjengwa.blogspot.com
 
siasa inafurahisha sana,ni kweli hilo wanalijua lakini halikuzoeleka kwa waziri kuzomewa.

ila nadhani wanajifanya wanapenda kuzomewa sasa.nilipata kuhudhuria mkutano mmoja wa CCM mjumbe fulani aliposimama wananchi wakaanza kumzomea kwa sauti,alichofanya badala ya kuendelea na hotuba akasema"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZIIIIIIIIIIII,WANAINCHI WAKAITIKIA KIDUMUUUUUUUUUUUU LAKINI HATUKUTAKIIIIIIIIIIII.
sasa huko ndiko tulikofikia,yaani baada ya kuzoea kuwazomea maofisa wa chini wa chama,wabunge,sasa ni mawaziri,next PM,mwisho ni Rais,na hapo tukifika just imagine!!!!!!!!!!
 
Mh. Seif Khatib anasema:

-Kiongozi kuzomewa ni gharama ya siasa. Ukiingia kwenye mchezo wa siasa ujiandae kwa hilo.
Loud and clear. Lakini daima utambue anayekupinga ana hoja, msikilize na jaribu kudadafua nini pumba na nini mchele.
-Sisi tuna kazi ya kufanya, wapinzani hawana kazi
This might be a joke? Kila mtanzania ana kazi ya kufanya! Labda kama ni tafsiri ya kisiasa zaidi ya hivi inavyosomeka. Muhimu ni kutimiza ahadi za 2005 ili baadae kieleweke kwao (serikali iliyo madarakani).

-Sisi tuna maswali ya kujibu 2010, wapinzani hawana
Self explanatory! Na kinachohitajika ni hekima badala ya kupoteza muda kukimbilia mahakamani kusafisha majina. Mnaweza kuibua mengine na mwisho mkajikuta 2010 inafika hakuna kilichofanyika hivyo umma wa watanzania kuwahukumu sawa na matendo yenu. Muhimu sana kuzingatia muda na kusoma alama za nyakati! Ushauri mzuri sana mheshimiwa katoa.
-Wapinzani hawapendi tufanikiwe
Ndiyo siasa yenyewe! Kushindwa kwa mpinzani wako ni baraka kwako ukiingia naye ulingoni. Penda usipende halikwepeki hilo. Sidhani kama CCM pia ingefurahi kwa wapinzani kufanikiwa kupata wabunge zaidi ifikapo 2010. Ndiyo raha ya upinzani!
-Msiingie kwenye mtego wa wapinzani
Labda awachomoe walioshaingia kichwa kichwa bila kujua kuwa wanajilengesha kubaya zaidi. Mtego umetegwa na njiwa kadhaa washanasika, kujinasua kazi kubwa kwao na inaweza kupelekea kuanguka kwao zaidi. Waache walionasika waliwe au wajinasue wenyewe au ikiwezekana wape mbinu za kuwawezesha!
-Wapinzani wapuuzeni, simamieni ilani ya chama
Hilo ni kosa... Wasipuuzwe wapinzani! Wana hoja na badala ya kujibizana nao jaribuni kupitia hoja moja baada ya nyingine kimya kimya huku mkitoa majibu kwa vitendo. Ndiyo njia nzuri na mbadala ya kuweza kumshinda anayekaribia kukumaliza politically. Maneno matupu yatawafikisha kusiko!
-Tuna ilani inayotekelezeka
Basi Nyerere/Mkapa alikuwa mwongo!
 
siasa inafurahisha sana,ni kweli hilo wanalijua lakini halikuzoeleka kwa waziri kuzomewa.

ila nadhani wanajifanya wanapenda kuzomewa sasa.nilipata kuhudhuria mkutano mmoja wa CCM mjumbe fulani aliposimama wananchi wakaanza kumzomea kwa sauti,alichofanya badala ya kuendelea na hotuba akasema"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZIIIIIIIIIIII,WANAINCHI WAKAITIKIA KIDUMUUUUUUUUUUUU LAKINI HATUKUTAKIIIIIIIIIIII.
sasa huko ndiko tulikofikia,yaani baada ya kuzoea kuwazomea maofisa wa chini wa chama,wabunge,sasa ni mawaziri,next PM,mwisho ni Rais,na hapo tukifika just imagine!!!!!!!!!!

Rais tayari wananchi walishambebea mabango na walishawahi kumgomea uzinduzi wa mradi wa maji. Next time watamzomea. Huwa nasuma tuu kwa matandao lakini ianipa raha sana kuona wananchi wamebadilika.

Ulishawahi huaangalia Movie ya The death of President? jamaa wanamzomea Bush Chicago hates Bushi! Chikago hates Bush! Karamagi akienda mgodini nadhani wananchi watamwimbia hivyo hivyo.
 
sasa huko ndiko tulikofikia,yaani baada ya kuzoea kuwazomea maofisa wa chini wa chama,wabunge,sasa ni mawaziri,next PM,mwisho ni Rais,na hapo tukifika just imagine!!!!!!!!!!

Tatizo watanzania hawakuzoea hali hii... Kuna kinachosababisha na kiko wazi. Mheshimiwa Rais alichotakiwa kukifanya ni kuhakikisha walau maisha ya watanzania yanarejea hata kwa kiwango alichotuacha nacho BWM.

Hali ya mtanzania wa chini usiisome kwenye magazeti ama vyombo vingine vya habari ukaachia hapo. Wasiliana moja kwa moja na jamaa yako yeyote aliye kijijini au hata Dar tu mwulize vipi maisha yamependeza eh? Jibu linaweza kukusababishia ukate simu ghafla.

Inawezekana bado! JK can do it...
 
Wao ndio wamewafundisha wananchi kuzomea kwani kule bungeni huwa wanawazomea watetezi wa wananchi, kila wanapowatetea.

wabunge wa CCM huwa wanawazomea wabunge wenye hoja za kujenga taifa na wananchi wameiga toka kwao wacha waipate fresh.
 
Wapinzani hawapendi tufanikiwe..
Katika lipi? Ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma? maana hilo ndilo linalopigiwa kelele na Wapinzani na wananchi wote kwa jumla,na silaha waliyonayo kwa sasa kabla ya uchaguzi ni KUZOMEA.
Na kwa vile hilo la kuzomewa hakulizoea zaidi ya kusifiwa,tuwahamasishe wananchi WAWAZOMEE SAAAANA
 
Zitto apinga ziara za Mawaziri mikoani

Na Joseph Mwendapole

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe, amepinga uamuzi wa serikali wa kuwapeleka Mawaziri na manaibu wao mikoani kuelezea bajeti akidai kuwa huo ni ubadhirifu wa fedha za umma.

Akizungumza na Nipashe jana, Bw. Kabwe alisema hakuna sababu ya msingi ya kuwapeleka mawaziri hao kuelezea masuala ya bajeti kwa kuwa hiyo ni kazi ya wabunge.

`Kila jimbo lina mbunge wake na kazi kubwa aliyonayo Mbunge ni kuwaeleza wananchi jimbo lake limetengewa kiasi gani katika bajeti....mimi naona ni kupoteza muda na fedha za umma,` alisema.

Alisema muda wa siku kumi ambao viongozi hao watakaa mikoani ni mwingi na kwamba maamuzi mengi ambayo yangetolewa wakiwa maofisini mwao yatasimama kwa wakati huo.

Bw. Kabwe alidai kuwa mawaziri na manaibu hao wametumwa kumpigia debe kigogo mmoja anayegombea ujumbe wa Halmashari Kuu ya Taifa NEC kwa kisingizio cha kuwaeleza wananchi kuhusu bajeti.

`Huo ni ujanja wa kutumia fedha za umma kuendesha kampeni zao za siasa, lakini inafahamika kabisa kuwa wametumwa na kigogo mmoja kumsaidia kampeni,` alisema.

Mwenyekiti wa TLP, Bw. Lyatonga Mrema, alisema huo ni ubadhirifu na ufisadi mwingine kwa kuwa fedha za kuwazungusha mawaziri 60 mikoa yote ni nyingi na zinatokana na kodi za wananchi.

`Watu hawataki kusikia tena porojo za viongozi, Watanzania wana matatizo mengi na wanataka kuona matatizo hayo yanatatuliwa, na mimi kwa maoni yangu naona kama huo ni uzururaji tu,` alisema Bw. Mrema.

Aliongeza kuwa Watanzania wamechoka kulaghaiwa kama ilivyokuwa zamani na kwamba wasipokuwa makini viongozi hao wanaweza kujikuta wakizomewa kila watakapopita.

Alisema Watanzania wamechoka kuona rasilimali za nchi yao zikiporwa na wachache huku wao, wakiendelea kupewa porojo za siasa na kubaki mikono mitupu.

Aliongeza kuwa kutokana na wananchi kuchoshwa na ukandamizaji na udhalimu, viongozi hao hawataeleweka kwa wananchi hata wangeenda na vitu vya kuwafurahisha na kuwachekesha.

`Hiyo bendi watakayokwenda nayo haitoshi labda waende na Ze Comedy, na kama wanataka waje niwakodishe nyani wangu maana wanataka kwenda kuwachekesha wananchi badala ya kuwaletea maendeleo,`alisema Mrema.

Aliongeza kuwa wananchi wana njaa, na baadhi yao wanashindwa kumudu hata kula milo mitatu kwa siku, hivyo hawana haja ya kusikia maneno matupu.

Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam, Bw. Ibrahim Mtei, alisema watu wanataka kuona zahanati, hospitali, shule za msingi na sekondari, barabara na dawa za kutosha na wala si maneno.

SOURCE: Nipashe
 
Mi naona kwa wao kwenda mikoani 'kusafisha sumu ya wapinzani' tayari wanafanya kosa lingine la kiufundi na kama ni mtego wameshaingia tena!
 
Huyu Khatibu katumwa Iringa kwa gharama za nani? Za sisiem ama za 'sirikali'? Hili liwekwe wazi tujue tafadhali. Kama ametumwa Iringa na chama chake tafadhali tusione gari lolote lenye namba za uwaziri, kwani hilo ni la kwetu sie walipa kodi. Kama katumwa na mwajiri wake asiongelee masuala ya chama chake.
 
hii ya Mrema kuwakodishia nyani wake imeniacha hoi,
 
nadhani kuna watu watapiga walau picha tuone anatembelea gari gani?
 
hii ya Mrema kuwakodishia nyani wake imeniacha hoi,

Mrema katika lile fuso lake kuna tumbili flani hivi huwa anatembea naye kila mahali...so ni kweli anaye na nishawahi kumwona...sijawahi kuona anavomtumia lakininadhani ni sehemu ya jinsi anavokusanya watu kwenye mikutano
 
Mie nina hakika wananchi walishaanza kuwazomea viongozi wetu siku nyingi ila ukweli nikuwa walikuwa hawadiriki kutoa sauti.Sasa hivi wananchi nadhani wamekuwa na courage ya kutoa sauti baada ya kubanwa kwenye kona.Watu husema ukimkimbiza paka ukambana kwenye kona akakosa mahala pa kutokea,basi atakugeukia wewe.
Wananchi wa Tanzania walikuwa na kila aina ya uvumilivu kusubiri maisha bora ya kesho ambayo yaliahidiwa na CCM,tangu enzi hizo. Lakini badala yake wamekuwa wakiona maisha yao yanazidi kuwa hoi kila kukicha. Sasa wameamua kuwaface CCM za the only solution.
 
'Hiyo bendi watakayo kwenda nayo haitoshi labda waende na Ze Comedy,na kama haitoshi niwakodishe nyani wangu maana wanataka kwenda kuwachekesha wananchi badala ya kuwaletea maendeleo' alisema Mrema.
Tehe! tehe! Mrema usinichekeshe wakati nina machungu,...watumie nyani tena katika mikakati yao?hiyo kali.
Hata hivyo kwa vile lengo lao siku zote ni kuona wingi wa watu mkutanoni wawaite Ze comedy kama ilivyokuwa Mnazi mmoja ambapo watu walijaa sana Lakini wakati wa hotuba ya Dr.S walipiga kelele "inatoshaaa,tunataka comedy" Lakini wenyewe wanakuambia mkutano ulifana sana wakati hakuna ujumbe wowote uliopokelewa na walengwa,
 
Hizi ziara zinanichanganya, wanaenda kumweleza nani juu ya huo ubora wa bajeti? Wananchi wote au viongozi wa CCM?

Khatibu alikuwa anaongea na Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa, Wajumbe wa Halmashauri Kuu na watendaji wa kata. Jana pia kwenye TV(TVT) niliwaona kina Malima na Sofia Simba wakiongea na viongozi wa CCM, ndo hapo nachanganyikiwa.

Wakisema wananchi wanamaanisha viongozi wa chama? Hivi wale walio nje ya chama hawapaswi kuelewa ubora wa bajeti?

Na suala la kutofautisha kazi za chama na serikali, viongozi wetu washashindwa kutambua utofauti, na ndo maana wabunge wa CCM hujiona sawa na mawaziri katika kutetea kila kitu cha serikali bungeni.

Labda wanahitaji semina elekezi ili watambue tofauti hizo, kama zipo anyway.
 
Mawaziri wazomewa

na Christopher Nyenyembe, Mbeya

MAWAZIRI wa Serikali ya Awamu ya Nne walio mkoani Mbeya kwa lengo la kukisafisha chama hicho tawala dhidi ya sumu iliyosambazwa na wapinzani, jana walijikuta wakiwa katika wakati mgumu kisiasa, baada ya mkutano wao wa hadhara kutawaliwa na miguno ya wananchi na baadaye kuzomewa.

Hali ya wananchi kutokubaliana na hoja za mawaziri hao walioandamana na makada wengine wa chama hicho wakiwamo wale waliotoka katika vyama vya upinzani ilianza kujionyesha tangu mapema kabisa.

Hata hivyo kelele za “hao hao, wamekosa hoja, tunataka Karamagi ajibu hoja” ndizo zilizotawala eneo ulipofanyika mkutano huo wa hadhara kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Ruanda eneo la Nzovwe, nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

Hali hiyo ya kuzomea iliendelea hata wakati viongozi hao wakiwa ndani ya magari yao wakiondoka katika mkutano huo jana jioni baada ya wananchi wengi kujipanga kando ya barabara wakipiga mayowe ya ‘hao…haoo, haoo.’
Viongozi hao wa juu serikalini na ndani ya CCM waliokuwa wakiongozwa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Taifa, Aggrey Mwanri, walitumia muda mwingi wa hotuba zao kukipamba chama hicho tawala, Ilani yake ya uchaguzi na kuwaponda viongozi wa kambi ya upinzani.

Hata hivyo miguno na kuzomea kwa wananchi wakati wote wa mkutano wakati fulani ilisababisha mhamasishaji mkuu wa chama hicho na mjumbe wa Halmashauri Kuu ambaye ni kiongozi wa kikundi cha uhamasishaji cha chama hicho cha Tanzania One Theatre (ToT), John Komba, kuwataka wale wote waliokuwa hawataki kupunga mikono kuondoka.

Hatua hiyo ya Komba ambaye alikuwa ameongozana na kikundi chake kizima cha TOT ilikuja baada ya kuwataka watu kupunga mikono kuitikia nyimbo zake, hatua ambayo haikuungwa mkono na baadhi ya watu, tukio lililosababisha ajikute akitoa maneno hayo.

“Huu ni mkutano wa CCM kwa hiyo kama kuna watu hapa hawataki kupunga mikono waondoke,” alisema Komba.

Katika mkutano huo, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chilligati, hakupata nafasi ya kuhutubia mkutano huo kutokana na wenzake waliomtangulia kutumia muda mwingi kukanusha tuhuma zinazotolewa na wapinzani dhidi ya chama hicho tawala.

Mwana CCM pekee aliyeonyesha kuungwa mkono moja kwa moja katika mkutano huo alikuwa ni Mbunge wa Kyela, moja ya majimbo ya mkoani Mbeya, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye alipopewa nafasi ya kuzungumza alizungumzia kuhusu utekelezaji wa sera za chama hicho katika maendeleo ya nchi.

Dk. Mwakyembe alisema kuwa mtaji pekee wa CCM walionao kwa wananchi ni kutekeleza ilani ya chama hicho ili kuweza kujihakikishia ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2010 na si vinginevyo, hatua ambayo ilisababisha ashangiliwe na watu.

Naye Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasirra, aliyetamba kwa jina la ‘Tyson’ alisifia juhudi zilizofanywa na serikali kuendeleza kilimo kwa kuingiza nchini kiasi kikubwa cha mbolea ya ruzuku.

Wassira aliyetumia muda mwingi kuziponda hoja za wapinzani kuhusu ufisadi, alisema miaka miwili kati ya mitano ambayo serikali imewekeana mkataba na wananchi, imefanya kazi kubwa ya kuboresha huduma za maji, miundombinu ya barabara, elimu na kilimo.

Huku baadhi ya watu wakionekana kutokubaliana naye kwa kutoa maneno ya; ‘siyo kweli’, Wasirra aliendelea kusema kuwa katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Marekani, Rais Jakaya Kikwete amepatiwa dola milioni 600 kwa ajili ya kilimo na ujenzi wa barabara kuwa hiyo ni hatua kubwa ya maendeleo.

Alidai kuwa ametumwa mkoani Mbeya kuja kuwabomoa wapinzani na hoja zao za ufisadi, ambao alisema wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kueneza uongo kwa wananchi bila kutoa ushahidi wa wazi, hali ambayo inapaswa kukomeshwa kwa kuwashikisha adabu.

Hoja hizo za Wasirra zilisababisha mkazi mmoja wa Mbeya kuingia mkutano akiwa na trekta lake kama ishara ya kuwataka viongozi hao kuachana na maneno ya jukwaani na kuhimiza vitendo.

Mbali ya viongozi hao wengine waliopata fursa ya kuhutubia ni makada wapya wa chama hicho waliojiunga kutoka upinzani, Shaibu Akwilombe, Tambwe Hiza na Salim Msabaha, ambao walitumia muda mwingi kuwaponda wapinzani na kuvifananisha vyama vinne vya upinzani vilivyoanzisha ushirikiano kuwa ni sawa na paka waliofungwa mikia pamoja.

“Hawa wapinzani walioungana ni sawa na paka waliofungwa mikia yao pamoja na nawaambia hawa hawajaungana, ukiwapelekea panya mbele yao kila mmoja atataka amkamate, wangojeni mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu utaona watakavyoachana,” alisema Akwilombe huku akipokewa na miguno ya dhahiri kutoka kwa wananchi.

Kwa upande wake, Tambwe aliwaambia wakazi wa Mbeya kuwa amekuja mkoani humu kuwaomba msamaha kwa kuwa alipokuwa upinzani ndiye alikuwa mpika majungu mkuu dhidi ya serikali na kwamba alikuwa akiungana na wenzake kupika uongo, sasa amerudi CCM.

Wananchi wengi waliozungumza na Tanzania Daima waliuelezea mkutano huo kuwa usio na jipya na wakasema kwa kiwango kikubwa walikuwa wameshindwa kujibu hoja zilizotolewa na wapinzani siku chache zilizopita.

Katika mazingira hayo na watu kushindwa kuishangilia CCM, kiongozi wa bendi ya TOT, Kapteni Komba, aliamua kuwalazimisha watu washangilie na kuwataka wale wasiofanya hivyo wageuke nyuma na kuondoka, hali iliyozusha minong’ono na wengine kuamua kuondoka. Baadhi ya watu walidai kuwa huu haukuwa muda muafaka kwa chama hicho tawala kufanya mkutano huo, kwani watu wanachotarajia zaidi ni kuona utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na chama hicho kwa mujibu wa ilani yao ya uchaguzi.
 
Huko tunakoelekea na jinsi hawa jamaa wajifanyavyo kuwa na roho ngumu isiyo chembe ya aibu mbele ya waTZ waliochoka,sitashangaa siku nikisoma gazetini 'Viongozi wa CCM wafurumishwa mkutanoni kwa mawe'
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom