Sehemu nzuri duniani

Hapa tunagandamiza siasa tu ,sasa hii habari labda ukaipeleke kunakohusika ,hali zetu kwa upande wangu ni hoi bin taaban ukiniletea sehemu hizo naona kama unanizalilisha na umasikini wangu ,samahanai lakini inabidi niseme ili dongo liondoke rohoni ,ngoja mpaka ukisikia tunachimba mafuta ndio utuletee labda tutaweza kupanda hata zile meli za kitalii na kuzurura nazo.
 
Wameweka The Statue of Liberty, Big Ben, the Petrona Towers na Burj al Arab lakini hawajaweka The Imperial Gardens (Tokyo) ?
 
Last edited:
Hapa tunagandamiza siasa tu ,sasa hii habari labda ukaipeleke kunakohusika ,hali zetu kwa upande wangu ni hoi bin taaban ukiniletea sehemu hizo naona kama unanizalilisha na umasikini wangu ,samahanai lakini inabidi niseme ili dongo liondoke rohoni ,ngoja mpaka ukisikia tunachimba mafuta ndio utuletee labda tutaweza kupanda hata zile meli za kitalii na kuzurura nazo.

Pole Mwiba..ila sasa dunia haiko fair maana siyo wote wenye njaa kama wewe!

Tatizo masurufu ya hayo mafuta yatakufikia? au watafaidi wenyewe? uwe mwangalifu udai chako kabla wajanja hawajawahi..
 
Ndio maana yake, hapa ni siasa tu ,hayo matembezi na majumba anasa ambazo kwa Mtanzania anaepigana na maisha yake na ya watu wake ,hatoweza kupata wasaa wa kuzuru au kuangalia mambo ya watu ,kama ni uzuri basi hakuna sehemu nzuri kama Tz na wanajenga hapo katikati ya mbuga ,hivi waache yote hayo waje huku kusiko kuzuri unawafanya wao hawana akili ,waje waishi katikati ya mijinyama isiyotabirika ,si wangekaa huko kwenye mahoteli ,wacheni hizo ,watu wamesema na wanaendelea kusema kuzuri,kutamu ni nyumbani tu hakuna kwengine ndio maana hata kukitokea patashika mtu anakimbilia nyumbani na kujiona yupo safe ,japo nyumba ni mbavu za mbwa, tujitahidini kuepuka mawazo mtindi mafisadi watazidi kutuona tunalewa tende.

Hivi unaona huko kwenye hayo majumba ndio sehemu kuzuri kabisa duniani ,ama kweli tunatoka mbali.
 
Kuzuri ni nyumbani, lakini nyumbani wapi?
 
Vile wewe nio Mganda nyumbani kwenu ni Uganda ,maana hata wale wanaofanya kazi huko wanakokuita kuzuri siku wakigaiwa likizo utawasikia wakiaga wenziwao kuwa mwezi ujao wanaenda nyumbani .Kikwete akipita huko mnakokuona kuzuri anawambia vibaka wenzie warudi nyumbani ili kuekeza.
 
Back
Top Bottom