Secretariat kuu ya CCM chukueni hatua sasa...!

greenstar

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
390
53
Napenda kutoa rai yangu kwa SECRETARIAT KUU ya CCM ichukue hatua juu ya maazimio ya kujivua gamba yaliyoafikiwa mwezi wa sita!

Nyinyi ni watendaji wakuu ndani ya chama ambao mnatakiwa muwe wabunifu katika kuendesha chama, acheni kupambana na CHADEMA,tafuteni sera nzuri zinazoweza kutekelezwa ili wananchi wawe na imani na serikali ya CCM.

Acheni woga wakuwafukuza wanachama wezi na ambao si waaminifu kwa CHAMA.
MAFISADI wanapata kiburi kwa vile mnaweka maazimio ambayo hamuwezi kuyatekeleza.Kama ROSTAM alitii, kwa nini mnaacha mtandao wake?

Fukuzeni wakaanzishe CHAMA chao cha KIFIDI waone uchungu wakutunyonya badala yakulindana !
 
Sijapata kuona ushauri wa ajabu kama huu! Mkuu hebu nitajie hata mmoja msafi ndani ya hicho Chama sembuse Kamati Kuu. Unataka kukiua chama wewe.
 
ushauri wa maana na si wa kupuuzwa hata kidogo kwa mustakabali wa chama chetu but my note is that asifukuzwe mtu bila uthibisho wa dhahiri kuhusika kwenye ufisadi na sio kutumia shutuma za magazetini au kamati zenye watu ambao ni mahasimu wa watuhumiwa kisiasa.ccm juu
 
Mkuu, unamaanisha watafukuza chama chote? Kazi kweli kweli!
 
sektretariat yenyewe ina ufisadi mtupu sasa watajivuaje magamba wenyewe...we waache waendelee hivyo walivyo watavuliwa magamba na wananchi wenyewe 2015
 
Hivi unamwambia nani? Kwani hujui CCM ni chama sikivu kilichoweka pamba masikioni? wewe jitokee uwaachie wenye chama.
 
Sijapata kuona ushauri wa ajabu kama huu! Mkuu hebu nitajie hata mmoja msafi ndani ya hicho Chama sembuse Kamati Kuu. Unataka kukiua chama wewe.

Wakiamua kweli kujivua gamba itabidi waondoke wote kisha wafunge ofisi na kukabidhi funguo kwa CCM asilia ya akina Butiku.
 
Napenda kutoa rai yangu kwa SECRETARIAT KUU ya CCM ichukue hatua juu ya maazimio ya kujivua gamba yaliyoafikiwa mwezi wa sita!
Nyinyi ni watendaji wakuu ndani ya chama ambao mnatakiwa muwe wabunifu katika kuendesha chama, acheni kupambana na CHADEMA,tafuteni sera nzuri zinazoweza kutekelezwa ili wananchi wawe na imani na serikali ya CCM.

Acheni woga wakuwafukuza wanachama wezi na ambao si waaminifu kwa CHAMA.
MAFISADI wanapata kiburi kwa vile mnaweka maazimio ambayo hamuwezi kuyatekeleza.Kama ROSTAM alitii,
kwa nini mnaacha mtandao wake?

Fukuzeni wakaanzishe CHAMA chao cha KIFIDI waone uchungu wakutunyonya badala yakulindana !

huyu sidhani kama alitii maagizo zaidi aliikinanga chama na wakaishia kumpigia magoti wakati wa kampeni uchaguzi mdogo igunga!!!!
 
Wengine tuslishalisema hili toka day one baada ya maazimio ya viongozi wa juu wa CCM. Cha ajabu tukaanza tena kukana kilichoazimia na kuweka tafsiri kibao za kinadharia juu ya KUVUA GAMBA wakati mwanzoni kila mtu alielewa kilichomaanishwa! Ni kweli kuwa hakuna malaika ndani ya sekretariet ya CCM; Si katika CHADEMA, CUF wala NCCR- Mageuzi n.k ambapo utawapata malaika lakini hapa tunasema kuwa ndani ya CCM kumekuwepo na watu waliondekeza Ufisadi na hao wanakidhoofisha Chama Tawala. Hao hawatakiwi kabisa. Wanapaswa kujiuzuru wenyewe na kama hawajafanya hivyo, zile siku 90 zilipita kitambo kwa kupotoshwa maana! CCM haistahili kupambana na CHADEMA bali kupambana na mafisadi na pia kuendelea kutekeleza ahadi walizozitoa kwa umma basi! Kamwe CCM isifikirie hata kwa sekunde kumsimamisha mtu mwenye tuhuma asiyekubalika katika jamii haijalishi tutatumia kiasi gani cha fedha; wananchi watampiga chini!!!
 
Napenda kutoa rai yangu kwa SECRETARIAT KUU ya CCM ichukue hatua juu ya maazimio ya kujivua gamba yaliyoafikiwa mwezi wa sita!
Nyinyi ni watendaji wakuu ndani ya chama ambao mnatakiwa muwe wabunifu katika kuendesha chama, acheni kupambana na CHADEMA,tafuteni sera nzuri zinazoweza kutekelezwa ili wananchi wawe na imani na serikali ya CCM.

Acheni woga wakuwafukuza wanachama wezi na ambao si waaminifu kwa CHAMA.
MAFISADI wanapata kiburi kwa vile mnaweka maazimio ambayo hamuwezi kuyatekeleza.Kama ROSTAM alitii, kwa nini mnaacha mtandao wake?

Fukuzeni wakaanzishe CHAMA chao cha KIFIDI waone uchungu wakutunyonya badala yakulindana !

Wanchekesha, aka mwenzangu ngoja nijinywee juice yangu. Nani amfukuze nani?
 
Napenda kutoa rai yangu kwa SECRETARIAT KUU ya CCM ichukue hatua juu ya maazimio ya kujivua gamba yaliyoafikiwa mwezi wa sita!
Nyinyi ni watendaji wakuu ndani ya chama ambao mnatakiwa muwe wabunifu katika kuendesha chama, acheni kupambana na CHADEMA,tafuteni sera nzuri zinazoweza kutekelezwa ili wananchi wawe na imani na serikali ya CCM.

Acheni woga wakuwafukuza wanachama wezi na ambao si waaminifu kwa CHAMA.
MAFISADI wanapata kiburi kwa vile mnaweka maazimio ambayo hamuwezi kuyatekeleza.Kama ROSTAM alitii, kwa nini mnaacha mtandao wake?

Fukuzeni wakaanzishe CHAMA chao cha KIFIDI waone uchungu wakutunyonya badala yakulindana !

Nani kakuambia ccm ina wanachama wasio waaminifu kwa chama? yupi sio mwaminifu kwa chama?
 
jombaa acha uongo, ccm hakuna gamba ila kulikuwa na tetesi za hapa na pale lakini nazo zilizokosa ushahidi. Chama kinanukia waridi na manukato ya muscat
 
Kweli wewe unauchungu na hisa zako kupotea hivi hivi,tatizo unajidai huju sera kuu ya magamba kuwa ni kulindana
Napenda kutoa rai yangu kwa SECRETARIAT KUU ya CCM ichukue hatua juu ya maazimio ya kujivua gamba yaliyoafikiwa mwezi wa sita!

Nyinyi ni watendaji wakuu ndani ya chama ambao mnatakiwa muwe wabunifu katika kuendesha chama, acheni kupambana na CHADEMA,tafuteni sera nzuri zinazoweza kutekelezwa ili wananchi wawe na imani na serikali ya CCM.

Acheni woga wakuwafukuza wanachama wezi na ambao si waaminifu kwa CHAMA.
MAFISADI wanapata kiburi kwa vile mnaweka maazimio ambayo hamuwezi kuyatekeleza.Kama ROSTAM alitii, kwa nini mnaacha mtandao wake?

Fukuzeni wakaanzishe CHAMA chao cha KIFIDI waone uchungu wakutunyonya badala yakulindana !
 
ushauri wa maana na si wa kupuuzwa hata kidogo kwa mustakabali wa chama chetu but my note is that asifukuzwe mtu bila uthibisho wa dhahiri kuhusika kwenye ufisadi na sio kutumia shutuma za magazetini au kamati zenye watu ambao ni mahasimu wa watuhumiwa kisiasa.ccm juu

hata wewe nakutilia shaka. Ni upepo tu utapita
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom