‘school bus’ la utata lanaswa na polisi dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Pick-Up hii aina ya Toyota leo mchana imenaswa na askari wa usalama barabara maeneo ya Posta ya zamani jijini Dar es Salaam ikifanya shughuli za kuwapeleka na kuwarudisha majumbani wanafunzi wa shule moja ya awali ikijulikana kama “School Bus” licha ya kuwa katika hali ya kuhatarisha usalama wa wanafunzi hao. Pichani ni wanafunzi waliokuwa wamebebwa katika gari hilo wakivuja jasho chini ya turubali lililofunika gari hilo kushika joto la jua. Kulia ni msimamizi wa wanafunzi hao.

2.jpg


“School Bus” hilo likipelekwa kituo cha polisi kwa uchunguzi zaidi.
 
Jamani hivi wazazi wa hawa watoto hawakuwa kuliona hili? watoto wanatia huruma masikini hata hawajui kinachoendelea...
 
Poor kids! They are so cute and don't deserve that. Hata mwalimu wao anahangaika kuweka **** kwenye mlango. Umaskini huu bwana...
 
Wazazi wao nao sijui hawana akili?utakubalije mwanao abebwe kwenye gari ya mizigo amekuwa viazi huyo mtoto?
 
Duh hiii ni balaa
hao wazazi wao wako wapi au walikuwa hawalijui hilo la watoto kubebwa kwenye pick up yenye turubali
Na hao walimu au huyo mwenye shule aliona kabisa hilo ni gari la kubebea wanafunzi
Hii biashara ya mtu anaanzisha shule nyumbani kwake na wazazi wanadanganywa wanapeleka watoto huko matokeo yake ndio haya
Poor kids hata hawajui kinachoendelea
Na mwalimu mwenyewe mbona nguo kama fupi sana kuwakalia wattoto mapaja yako nje anafundisha nini
Au ni kwamba watoto wakitoka hapo wamefuzu kila kitu
 
kusema wazazi hawalijui hilo hainiingii kichwani, yaani kweli gari analobebewa mwanao hulijui?
Juzi hapa yamemfika mzazi mwenzao, hata kama mtu hukuwa na utaratibu wa kuFuatilia usafiri wa shule wa mtoto, that should have rang the bell in my head...
 
Saivi kila mtu anamiliki shule bado mimi tu ila bora wafike kwetu km kadhaa porini ndio ukute shule ikitokea ht baiskeli unashukuru br hao,MUNGU WE WAJUA TUBARIKI WANAO.
 
Mkuu kumbe upo huku?nimekutana na bango la WANTED kule jukwaa la siasa na chini kuna jina lako. Pse hebu nenda tuu kule msamaha wako ushatangazwa.tehe tehe!

mpaka baada ya wiki ndio watakuwa active kule rejao ndio kimya kabisa.
 
Back
Top Bottom