Basi limetoka Dar kwenda Mwanza na sio Mwanza kuja Dar.
Nimepewa taarifa na jamaa yangu ambaye yuko ktk basi aneniambia basi hilo walikuwa wanaongozana tangu Ubungo na hapo Gumira kuna ajali 2 hiyo ya Basi ambalo hadi sasa wmeshaopowa maiti 8 na zoezi linaendelea. na mbele kidogo kuna ajali nyingine ya basi ya abiria na lori la mafuta ambapo kwenye hiyo ajali pili ya lori na basi kuna majeruhi tu hakuna watu waliopoteza maisha.
Ni kazi nzito sana hiyo ndugu yangu, wee acha tu, hiyo kuchanganya majeruhi na maiti ni kutokana na ugumu wa kazi yenyeweJamani hii inasikitisha sana, hivi ni nani huwa anatenga maiti na majeruhi? wengine wanacheleweshwa kwenda hosp kwa kudhaniwa wamekufa kumbe majeruhi. Mambo ya uokozi yanahitaji umakini sana.
mkuu wa emirates hapo barabara mbovu ndio chanzo kikubwa cha ajali zimazoendelea kutokea hapa nchininini kinachoendelea kuhusu hizi ajali kila siku? ni barabara mbovu au ni madereva wazembe? inasikitisha sana kuona watu wanapoteza maisha kila siku kutokana na ajali za mabasi.najua kwamba ajali ni kazi ya mungu lakini nadhani kuna uwezekano wa kuzipunguza kama watu husika wakiwa makini.nawatakia pole wafiwa wote na majeruhi nawaombe mpone haraka sana.
aaaaaaarrrhg jamani loh imefikia hatua nikipanda magari siku hizi huwa nasali kabisa sala ya toba manake najua madereva wetu siku hizi ni mawakala wa israel. na ukishuka salama unashukuru Mungu, mbona tunaandamwa hivi, nakosa la kusema kwa kweli. RIP marehem wote
Tajiri Mtu Mzima,
Mabasi yanayotoka Mwanza au Ziwa Magharibi uwa yanapambazua either Dodoma au Morogoro. Kwa hiyo yawezekena kabisa SkyLink ili-LALA Dodoma na kudamka kuja Dar es Salaam na nikitizama muda yawezekana ilikuwa imefika Gairo. There are chances kuwa Bus lilikuwa lina "Mechanical fault" na ndio maana liko nyuma sana ya "ETA".
kufika mapema tunapo kwenda tunapenda..ila gharama yake muda mwingine gharama yake ni kubwa...tuwe wakali kwa madereva wanaoendesha mwendo kasi hatarishi,....
Katika kipindi hicho JK ametoa wito kwamba wanaosababisha hizi ajali wafungiwe maisha kuendesha magari, na si hivyo tu na hata adhabu ziwe kali mpaka kifungo cha maisha maana kwa kweli wote tuna kuwa ni ni majeruhi watarajiwa...
Nadhani namuunga mkono JK kuwa sheria zetu zifanyiwe marekebisho na kuweka adhabu kali sana.
sasa inakuwaje jk anasema mderva wapewa adhabu kali kabla serikali haija solve tatizo ya barabara mbovu?mkuu wa emirates hapo barabara mbovu ndio chanzo kikubwa cha ajali zimazoendelea kutokea hapa nchini
Tatizo hapa sio sheria, barabara wala nini, kiini cha haya yote ni rushwa kuanzia TBS na Police ikichagizwa na uzembe wa madereva.