ScanLink likitoka Mwanza kuja Dar lapinduka Gairo - Morogoro

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,277
8,492
Taarifa zinazoingia hivi punde ni kuwa Basi la SkyLink toka Mwanza kuja Dar limepinduka muda si Mrefu maeneo ya Gairo, likiwa limevuka kidogo eneo hilo. Mtoa habari anasema watu wengi wamefariki na wengi kujeruhiwa wakiwa katika hali mbaya.

Tafadhali Jeshi la Polisi na wadau wengine mlio karibu mjitokeze kwenda kuokoa jahazi na kuwasaidia Wahanga.

Tuendelee kupeana updates
 
Samahani mkuu, uelekeo wa hili basi ni Dar - Mwanza au Mwanza - Dar?
 
Hii ni too much!! wahusika wawajibike.
Poleni sana wafiwa na majeruhi!!
 
nini kinachoendelea kuhusu hizi ajali kila siku? ni barabara mbovu au ni madereva wazembe? inasikitisha sana kuona watu wanapoteza maisha kila siku kutokana na ajali za mabasi.najua kwamba ajali ni kazi ya mungu lakini nadhani kuna uwezekano wa kuzipunguza kama watu husika wakiwa makini.nawatakia pole wafiwa wote na majeruhi nawaombe mpone haraka sana.
 
Kafara? uzembe? rushwa? hii inaonyesha upande wa pili wa athari za ufisadi ....miundo mbinu mibovu na isiyoendana na wakatietc etc

Eh Mungu utunusuru na dhahama hii!
 
Kama ni kweli ... Ajali mpaka lini?

Speed Governor ... hazikusaidia

Speed Chat ... hizi ni mashine za rushwa

Vehicle Inspection ... mashine za rushwa

Sasa majuzi tumeambiwa

Bus inayotembea zaidi ya masaa 12 lazima ikaguliwe kabla ya kusafiri tena! Hili linafanyika?

Pole waiofiwa na waliojeruhiwa wapone haraka
 
soma heading kwanza

Kigogo,
The reason I'm asking, kwa muda huu sio rahisi kwa basi litokalo Mwanza kuwa limefika Gairo, vinginevyo liwe limetoka jana, but ni muda ambao most likely utakuwa maeneo hayo if coming the other way.

NATOA POLE KWAWOTE WALIOFIKWA NA JANGA HILI..
 
Ni jana tu ITV wameonyesha kipindi maalumu cha ajali za barabarani na jinsi zinavyoligarimu taifa hasa katika nguvu kazi.

Katika kipindi hicho JK ametoa wito kwamba wanaosababisha hizi ajali wafungiwe maisha kuendesha magari, na si hivyo tu na hata adhabu ziwe kali mpaka kifungo cha maisha maana kwa kweli wote tuna kuwa ni ni majeruhi watarajiwa...

Nadhani namuunga mkono JK kuwa sheria zetu zifanyiwe marekebisho na kuweka adhabu kali sana.
 
Taarifa zinazoingia hivi punde ni kuwa Basi la SkyLink toka Mwanza kuja Dar limepinduka muda si Mrefu maeneo ya Gairo, likiwa limevuka kidogo eneo hilo. Mtoa habari anasema watu wengi wamefariki na wengi kujeruhiwa wakiwa katika hali mbaya.

Tafadhali Jeshi la Polisi na wadau wengine mlio karibu mjitokeze kwenda kuokoa jahazi na kuwasaidia Wahanga.

Tuendelee kupeana updates
Mkuu asante sana kwa taarifa ila neno WAHANGA nadhani umelitumia vibaya.
 
Kigogo,
The reason I'm asking, kwa muda huu sio rahisi kwa basi litokalo Mwanza kuwa limefika Gairo, vinginevyo liwe limetoka jana, but ni muda ambao most likely utakuwa maeneo hayo if coming the other way.

NATOA POLE KWAWOTE WALIOFIKWA NA JANGA HILI..

Tajiri Mtu Mzima,

Mabasi yanayotoka Mwanza au Ziwa Magharibi uwa yanapambazua either Dodoma au Morogoro. Kwa hiyo yawezekena kabisa SkyLink ili-LALA Dodoma na kudamka kuja Dar es Salaam na nikitizama muda yawezekana ilikuwa imefika Gairo. There are chances kuwa Bus lilikuwa lina "Mechanical fault" na ndio maana liko nyuma sana ya "ETA".
 
Last edited:
Kigogo,
The reason I'm asking, kwa muda huu sio rahisi kwa basi litokalo Mwanza kuwa limefika Gairo, vinginevyo liwe limetoka jana, but ni muda ambao most likely utakuwa maeneo hayo if coming the other way.

NATOA POLE KWAWOTE WALIOFIKWA NA JANGA HILI..

Basi limetoka Dar kwenda Mwanza na sio Mwanza kuja Dar.
Nimepewa taarifa na jamaa yangu ambaye yuko ktk basi aneniambia basi hilo walikuwa wanaongozana tangu Ubungo na hapo Gumira kuna ajali 2 hiyo ya Basi ambalo hadi sasa wmeshaopowa maiti 8 na zoezi linaendelea. na mbele kidogo kuna ajali nyingine ya basi ya abiria na lori la mafuta ambapo kwenye hiyo ajali pili ya lori na basi kuna majeruhi tu hakuna watu waliopoteza maisha.
 
Napajua hapo mahali gari lilipo angukia wala hakuna kutafuta mchawi nani hapo, hiyo sehemu lami imekosewa mvua kidogo lami inateleza na polisi wanalijua hilo na wausika TANROAD wanalijua yani mvua ikinyesha kidogo tu hiyo sehemu magari yanaangukaga sababu si nyingine ni uzembe wa watendaji polisi wenyewe wanajua wakiona manyunyu tu wanatangulia kupima sababu lazima gari itaanguka, yani mi hii itakuwa ajali ya tano kuisikia ajali ikitokea hapo niliona shabiby inaanguka kwa macho yangu achana na magari madogo si kwamba wausika hawajui watakwambia fungu halijatoka, Hivi kuna nini nchi hii kila mtu kuwa mwanasiasa siasa mpaka kwenye maisha ya watu
 
Doh...! Hii hali tutaondokanayo lini sisi watanzania, eeh mungu tusaidie.

Maana wenye majukumu na hili inaonyesha hawana habari nalo, kutwa kucha rushwa tuu ndo la muhimu kwao. Ooh nilitaka kusahau, na kununua latest cars kwa comfort zao binafsi huku watanzania tukitaabika kwa mikasa mingi ya ajabu ajabu...

Kinachouma zaidi ni pale linapotokea jambo basi wao ndo ooh kuanzia sasa tutafanya hivi kudhibit hili na lile...

Mi naomba kuuliza, hawa watu inamaana hawajui kazi yao mpaka itokee maafa ndo wajue mbinu za kuepuka ili lisitokee tena??? nimechoka mimi na ujinga huu

Mwenyezi mungu Awalinde majeruhi wapate kuweza kupita wakati huu mgumu
Kama kuna wafiwa nawapa pole wote, Na Mwenzi mungu aweke roho za marehemu mahali pema
 
Basi limetoka Dar kwenda Mwanza na sio Mwanza kuja Dar.
Nimepewa taarifa na jamaa yangu ambaye yuko ktk basi aneniambia basi hilo walikuwa wanaongozana tangu Ubungo na hapo Gumira kuna ajali 2 ....

BornTown,

Hapo ni Dumira au Gumira? Sikumbukiki vizuri Dar-Dom road, lakini sijawahi kusikia kituo kinaitwa Gumira...
 
...najua kwamba ajali ni kazi ya mungu lakini nadhani kuna uwezekano wa kuzipunguza kama watu husika...

Kwa hiyo ungependa kujaribu kurekebisha "kazi ya Mungu"?

Unataka kupangua mipango ya Mungu?

Tazama imeandikwa, kazi ya Mungu haina makosa.

Piga magoti tumkemee pepo mchafu aliyeingilia roho na nafsi yako asubuhi ya leo.

Ifahamike, Mwenyezi Mungu ndio ameua hawa watu.

Kwa maana Mungu wetu mwenye upendo ni serial killer.

Akikupangia siku ya kifo, anakupangia na ajali ya kukuadhibu as you go.

Point is, Mungu hahusiki kwenye mi ajali yetu ya kizembe hii. "Kazi ya Mungu" my foot!
 
kama ni kweli basi hatari, MABASI ya kisasa kiboko Mwanza-Gairo masaa manne.
Labda zinafungwa INJINI ZA NDEGE itabidi polisi wakague na hilo pia
Poleni sana wafiwa na majeruhi mpate nafuu mapema
 
Poleni sana wote.

Suluhisho la kupunguza ajali ni: kuboresha miundombinu hasa alama za barabarani; kuongeza adhabu kwa madereva, wamiliki wa magari ya abiria na askari wa usalama barabarani wasiofuata maadili ya kazi zao; kukagua mara kwa mara ubora wa magari; na kusimamia kwa ukali ratiba za mabasi.

Ni ujinga kuendelea kuona watu wasio na hatia wanakufa hovyo mara kwa mara kwa ajali!
 
Back
Top Bottom