Sauti ya wazanzibari- kilio cha Haki juu ya muungano.

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
[h=6]Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 02 May 2012 MWANA HALISI

KILA yanapojitokeza matatizo mazito katika suala la muungano, watawala hufikiria njia ya mkato ili kuziba midomo ya watu wanaohoji au wanaokosoa.

Baadhi ya mambo ambayo watawala walifikiria haraka kama mkakati wa watawala wa kuwaridhisha wananchi ni kuunda sekretarieti kamili ya kujadili muungano.

Baadaye, ofisi ya makamu wa rais ilipewa jukumu kamili la kushughulikia kero za muungano.

Katika suala hili, kazi ya ofisi hiyo ni kusimamia, kufuatilia kwa lengo la kutatua kero za muungano. Ofisi hiyo pia ikapewa jukumu la kuratibu hata yasiyokuwa mambo ya muungano.

Muundo huu nao unazua manung’uniko. Makamu wa Rais ni Dk. Mohammed Gharib Bilal atokaye Zanzibar, kule ambako pia anatoka waziri anayeshughulikia masuala ya muungano, Samia Suluhu Hassan.

Hawa, pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndio, linapofika suala la kujadili kero za muungano hukutana na wawakilishi wa Zanzibar. Uwakilishi huo unatosha?

Baada ya watawala kuzindua sekretarieti yao na kuipa jukumu hilo zito ofisi ya makamu wa rais kushughulikia kero za muungano, bado msimamo wa wananchi, hasa upande wa Zanzibar kutaka wapewe fursa ya kuujadili upya muungano uko palepale.

Mwaka jana watawala wakaongeza kitanzi kuzuia kabisa muungano kujadiliwa. Bunge lilipitisha Sheria ya Marekebisho ya Katiba yenye kifungu kinachozuia uhuru wa kujadili muungano.

Sheria hiyo inataka wananchi wajadili kwa lengo la kuboresha tu muungano. Kwa lugha nyingine, wale wenye maoni tofauti watakuwa wanajisumbua kutoa maoni kwa mtazamo tofauti na muundo wa serikali mbili.

Wakati sheria inakataza wananchi kuhoji muungano wa serikali mbili au inakataza kujadili kwa mtazamo tofauti, maelfu ya watu wanahudhuria mikutano inayoitishwa na kikundi cha Uamsho cha Zanzibar chenye msimamo mkali dhidi ya muungano.

Nilipohudhuria moja ya mikutano ya jumuiya hiyo kisiwani Pemba Machi mwaka huu, na hata ninaposoma habari za mihadhara yao, maelfu ya watu wanaohudhuria mikutano hiyo Unguja wakiulizwa wanataka muungano uendelee au uvunjwe, sauti husikika, “Uvunjweeeeee.”

Hawa ni Wazanzibari. Hawa hawapaswi kupuuzwa kwa mbinu za sheria, tishio la kufungwa au adhabu nyingine zozote.

Serikali inataka isikie sauti za watu gani ili ikubali kuwa umefika wakati wa kutoa fursa watu watoe dukuduku zao? Si tuliambiwa kuwa muundo wa muungano wa serikali mbili ni sera ya CCM, sasa kwa nini sera ya CCM inalindwa kwa sheria?

Kama muungano ni wa serikali basi waachiwe watawala wafanye wanavyotaka. Ila kama muungano unawahusu watu wapewe fursa ya kuujadili kama tutakavyojadili maeneo mengine tunayosema yamepitwa na wakati. Hata muungano huu umepitwa na wakati.

Watawala wanajua kwamba malalamiko ya Wazanzibari dhidi ya muungano huu yalianza kabla na baada ya Rais Abeid Amani Karume kutia saini mkataba wa muungano 25 Aprili 1964.

Wanadai watu wa kawaida hawakuulizwa. Wanadai pia Karume hakupewa fursa ya kuwa na mshauri wa kisheria. Wengine wanasema alikataa mwenyewe kushirikisha wasaidizi wake.

Aidha, wanadai Karume alidhani ametia saini mkataba wa shirikisho la Afrika Mashariki na siyo muungano na kwamba hati za muungano hazikuridhiwa na Baraza La Mapinduzi.

Vilevile, wanadai hata chama chao cha Afro-Shirazi Party (ASP), kilikuwa hakijataja katika katiba na ilani yake kwamba dira yao ilikuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Watawala wanajua kwamba miaka ile ya 1980 Mwalimu Julius Nyerere aliwashutumu watu waliokuwa wanadai 1+1=3 yaani Tanganyika + Zanzibar = 3. Mwaka 1984, suala la muungano lilisababisha Rais wa awamu ya pili Zanzibar, Alhaji Aboud Jumbe kujiuzulu kwa shinikizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pamoja na mzee Jumbe kulazimika kutema urais, bado Wazanzibari waliendelea kudai Zanzibar yao. Hicho ndicho kilichochea mwaka 1994 wabunge 55 maarufu kama G55 kuanzisha mchakato wa kuidai Tanganyika.

Hoja hiyo ilizimwa na Mwalimu Nyerere aliposema wote wanaotaka Tanganyika kwanza watoke CCM maana muungano wa serikali mbili ni sera ya chama hicho tawala.

Kwa majibu hayo, vyama vingine vyote havifungwi na sera hiyo. Sera ya Chama cha Wananchi (CUF) na hata Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni muungano wa mfumo wa serikali tatu.

Muundo huu ndio wengi wanaona kuwa utaipa hadhi Zanzibar itambulike kama nchi kimataifa na hata iwe na kiti katika Umoja wa Mataifa (UN).

Tume zote zilizoundwa na marais waliopita na hasa ile Tume ya Jaji Robert Kisanga (1999), japo haikupewa hadidu rejea kujadili muungano, walioulizwa walitaka Zanzibar yao.

Kwa hiyo, sheria iliyowekwa leo kuzuia watu kuujadili kwa uhuru ni woga wa watawala kuonekana wao wamevunja muungano huo.

Inajulikana CCM hawakuweka katika ilani yao hoja ya kurekebisha Katiba, ila Rais Jakaya Kikwete aliamua ‘kuiba’ hoja ya CHADEMA. Hata baada ya hapo, hakuweka bayana hadi alipoona maandamano ya kutisha nchi nzima yaliyoitishwa na CHADEMA.

Rais alitumia maneno yaliyowapa furaha watu kwamba watapata katiba mpya wakati yeye alikuwa na maana ya kufanyia marekebisho. “Tutahuisha katiba iliyopo,” alisema. Hii ina maana kuipa uhai.

Rais Kikwete akasema muungano ni tunu ya taifa lazima ulindwe. Kwa mujibu wa sheria hiyo ya marekebisho ya katiba, majukumu ya Tume aliyounda Rais Kikwete chini ya Jaji Joseph Warioba yatakuwa:

Kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi.
Kupitia na kutafiti usahihi na ulinganifu wa masharti ya kikatiba yanayohusu mamlaka ya watu, mifumo ya kisiasa, demokrasia, utawala wa kisheria na utawala bora.
Kutoa mapendekezo kwa kila hadidu ya rejea.
Kuandaa na kuwasilisha ripoti.
Katika kutekeleza masharti ya kifungu kidogo 1, Tume itazingatia misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii na kwa mantiki hiyo, kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo:
Kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano
Kuwepo kwa serikali, bunge na mahakama
Mfumo wa kiutawala wa kijamhuri
Kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Umoja wa kitaifa, amani na utulivu
Uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote kupiga kura
Ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu
Utu, usawa mbele ya sheria na mwenendo wa sheria
Uhuru wa kuabudu na uvumilivu wa dini nyingine.
Kwa madhumuni ya vifungu 1 na 2 na kwa jambo lolote jingine muhimu kwa taifa, Tume itatoa fursa kwa watu kwa lengo la kuendeleza na kuboresha
.[/h]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom