Sauti nzuri na sura havitoshi kuwa mtangazaji

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
Jioni ya leo katika radio ya pashen fm huwa kunakuwa na kipindi nimekisahau jina. Wapo watangazaji watatu; wa kiume mmoja na mabinti wawili wenye sauti nyororo. Kilichoniboa kuhusu wote watatu ni ufaham wao mdogo wa mambo na kutokujua kiswahili kwa ufasaha. Kiukweli nimewakosoa kimoyomoyo mpaka basi. Mfano kuna habari moja toka kenya kuwa bwana mmoja-ochieng kawaua watoto wake watatu wa kufikia pamoja na mama yao. Wao wakajichanganya wasijue wanasoma nini na kufikia uamuzi kuwa ile familia ndo imemuua huyo bwana. Imenifanya kununua gazeti hilo la dar leo na kuisoma habari hiyo. Kingine ni habari iliyohusu majambazi ambapo wanasema majambazi 'waliweza' kuuawa. Hii inasikitisha
 
Asasi/taasisi zinazotawala media zinatakiwa kulivalia njuga suala la kuondoa makanjanja kwenye uandish wa habari.
 
Back
Top Bottom