Satelite ya Galileo katika anga za juu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,269
Roketi la Soyuz lilifyetuliwa leo kutoka kituo cha misafara ya anga za juu ya Ulaya katika Guiana ya Ufaransa katika eneo la Karibian, ikiwa inabeba satelite mbili za mwanzo za mfumo wa Galilleo wa uongozi wa safari za angani. Mradi huo wenye gharama ya euro bilioni 5.4 unatarajiwa kuwa na setalite 27 zenye kufanya kazi pamoja na tatu nyingine za kutumiwa wakati wa dharura, ifikapo mwaka 2020. Mfumo huo utakuwa unashindana* na ule wa Kimarekani wa GPS. Mfumo huu wa Ulaya utagunduwa usahihi wa mkao wa dunia hadi ukubwa wa eneo la mita moja, wakati mfumo wa Marekani wa GPS usahihi wake unafikia ukubwa wa eneo la mita tatu hadi nane.
 
Nimeiona hii kitu kwenye news kwa kweli italeta mapinduzi makubwa ya mawasiliano na wanaoendesha magari kwa kuongozwa na satelite. Inabidi tech kama hizi zije na huku kwetu
 
Nimeiona hii kitu kwenye news kwa kweli italeta mapinduzi makubwa ya mawasiliano na wanaoendesha magari kwa kuongozwa na satelite. Inabidi tech kama hizi zije na huku kwetu

kaka angalia hyo budget yenyewe,unataka tulale njaa mkuu,
 
Tatizo ni pale mlundikano wa sat. nyingi angani ambazo wakati mwingine hutokea kuanguka ardhini bila udhibiti wowote. Kila jambo lina mazuri yake na mabaya yake
 
Wenzetu hawawazi masuala ya umeme au wanafunzi wao kunyimwa mikopo,wao ni kazi tu.
 
Back
Top Bottom