Sasatel: Another crappy modem-what else is new??

Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,193
3,011
@Mods, uzi mtauweka kwene jukwaa muonalo linafit zaidi, mkipenda

Baada ya kuchoka na spidi za 'unlimited'
za 0.00 kps za Voda niliamuaga kuhamishia majeshi
huku Sasatel, kwa sababu mie ni mtu wa kutotaka
attachment huwa na nachukuaga package za wiki
ili nikiboreka iwe rahisi kusepa na kuacha kulipia.


Mwanzoni ilikuwa inaniwezesha kusurf kwa spidi
acceptable kwa kuzingatia technology yenyewe ya
CDMA. Sasa hivi ina kama siku 3 na mtandao unakata
kama hauna akili nzuri. Sasa kuwa mteja imekuwa kero na
pesa yangu yaeza ku-expire bila kumalizika kwa package
yangu ya wiki. Sasa nashindwa kuelewa hawa TCRA
wanafanya kazi gani? Hivi hii nji kuna watu wanafanya
kazi zao kweli bila kushikiwa bakora?


Speaking of these dinasaurs TCRA, Majuzikati zinakuja
sms kibao kwene line yangu ya tIGO eti sijajisajili, these
fools ni kwamba siku ninanunua line nililipa cash na kujisajili
papo hapo na karatasi ninayo, why mteja nibughudhiwe na these
incompetent fools kwa uzembe wao? where is the so called
'regulation' by regulatory body? hiyo kasma ya TCRA
kwanini wasilipwe walimu au madaktari ambao wanatusaidia
huku uswazi?


Zis kantri bana, I'm speechless.
 
Nways nimekata shauri kukatelekeza kamodem kao..maana kameniharibia siku na kuharibu ratiba yangu na kunikosesha kuwasiliana na watu muhimu, they won't see my money ever again.
 
sasatel iko bomba huku BUZA YOMBO ninakoishi, labda ni maeneo unayoishi network inasumbua, sasatel naiaminia sana mkuu.
 
sasatel iko bomba huku BUZA YOMBO ninakoishi, labda ni maeneo unayoishi network inasumbua, sasatel naiaminia sana mkuu.
Inaezekana..ila kwangu ndo baibai sirejei nyuma, siezi kubembeleza huduma mbofumbofu ninayolipia kwa Mbytes.
 
Sasatel kimeo sana, hasa ukiwa nje ya mji. Mie nilinunua modem kwa minajili ya kutumia maskani, nilivyoijaribu katikati ya jiji ilikuwa bomba tu, lakini nilipotoka nje ya mji haikuwa na network. Nimeboreka sana, ikizingatiwa kwamba nilinunua modem yao ili niwe na surf nyumbani, na si kazini.
 
dah watanzania bwana nchi hii ni capitalist economy so kama inakuboa sasatel hama so mnaleta post za ajabu, kuna tigo zantel airtel hamia huko kama unahela funga wireless yako kwako
 
dah watanzania bwana nchi hii ni capitalist economy so kama inakuboa sasatel hama so mnaleta post za ajabu, kuna tigo zantel airtel hamia huko kama unahela funga wireless yako kwako
Capitalism ndo kutoa huduma mbovu? hivi unaelewa essence ya huu uzi au unakurupuka tu? Kaa huoni mantiki ya uzi huu kaa pembeni hujaombwa wala kulazimishwa kuusoma.
 
Duh, sisi wa mikoani tulikuwa tunaomba siku Sasatel wangetia timu huku kumbe nao hovyoo.
sasa twende wapi? maana spidi za airtel, voda na tigo ni zile za kobe akishindana na konokono kupanda mlima. pathetic
 
mi natumia sasatel siku zote na iko bomba mbaya kama ulaya. Tatizo kubwa la sasatel ni pale siku 7 zinapoisha na bado bundle zipo kibao, ninachoona kinafaa kurekebishwa ni kuwa siku 7 zinapoisha wasitishe kutoa internet access lakini utakapo recharge siku yeyote basi na zile bundle zilizobaki ziendelee kutumika, hicho ndiyo kilio. speed ya internet inategemea mambo mengi katika kompyuta yako na hili watu wengi hawataki kujifunza, unakuta mtu ana pc ya RAM ya mb 250 na ana-install programme 30! huu ni mfano lakini yapo mengi pia juu ya processor na kadharika. binafsi naipenda sasatel labda kama upo nje sana na jiji
 
Back
Top Bottom