Sasababu saba zinazowafanya wanaume wachelewe kuoa

KakaNanii

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
325
52
  1. kupenda kuoa mwanamke mrembo kuliko wote ambaye hayupo
  2. ukosefu wa fedha unaoweza kusababishwa na ukosefu wa ajira ya uhakika
  3. kujiringanisha na wanaume wengine ambao wana mafanikio ya juu sana na baadae mwanaume huyo kuona hajafikia bado mafanikio anayoyataka ili aweze kuoa.
  4. ukosefu mkubwa sana wa nguvu za kiume yaani uhanithi
  5. ubinafsi wa baadhi ya wanaume ambao huona kuoa ni sawa na kupoteza fedha tu. Kwa kuwa yeye mwanaume akioa itabidi amhudumie mke.
  6. kutokujiamini kwa baadhi ya wanaume ambao huona kuoa ni jambo gumu sana na kwao wao halitawezekana.
  7. baadhi ya wanaume huogopa wanawake sana kiasi cha kuogopa kuwatongoza ambako husababishwa na kuogopa kukataliwa !!!
 
wanachoka kufua ,kupika na kuosha vyombo

Hapo mkuu Firstlady naomba kutofautiana nawe kidoogo.Hatuoi ili kupikiwa kufuliwa na kuoshewa vyombo maana kama ni hivyo mbona yote hayo tunayaweza na kuna vifaa vya kurahisisha kazi hiyo.Tunaoa kwa kuangalia vigezo mbalimbali,mfano uwezo wa akili(maana 80% ya akili ya mtoto hutegemea mama)ukarimu na upendo wake kwa wanafamilia,kujiamini kwake n.k.Kwa wanaoishi western style of life kazi ya kuweka nguo kwenye mashine ni ya mwanaume na hata jikoni anaingia,hivyo kwa wanaotegemea kuolewa ili akaweke mpododo chini na kumsubiri bwana alete na yeye akaangize tu wajue wana wakati mgumu karne hii.Na kwa mwanaume ni bora akawie kuoa lakini ampate atakayekidhi vigezo hivyo kuliko ajichukulie mzigo utakaomlemea maisha yake yote.
 
Mimi ni mmoja wapo ambae 'm delaying to marry. Reason No. 2 & 3 ya kumpata an intelligent & family lovin woman is why i still hang on. I have people asking me when i will get married.
Kwa wale wanaotaka kuoa sabab wamechoka kufua na kupika, well i got my x driver who told me the same. 'Mkuu natakiwa nioe. Nimechoka kufua, kupika na kupiga deki...'
 
  1. kupenda kuoa mwanamke mrembo kuliko wote ambaye hayupo
  2. ukosefu wa fedha unaoweza kusababishwa na ukosefu wa ajira ya uhakika
  3. kujiringanisha na wanaume wengine ambao wana mafanikio ya juu sana na baadae mwanaume huyo kuona hajafikia bado mafanikio anayoyataka ili aweze kuoa.
  4. ukosefu mkubwa sana wa nguvu za kiume yaani uhanithi

    [U][*]ubinafsi wa baadhi ya wanaume ambao huona kuoa ni sawa na kupoteza fedha tu. Kwa kuwa yeye mwanaume akioa itabidi amhudumie mke.
    [/U]
  5. kutokujiamini kwa baadhi ya wanaume ambao huona kuoa ni jambo gumu sana na kwao wao halitawezekana.
  6. baadhi ya wanaume huogopa wanawake sana kiasi cha kuogopa kuwatongoza ambako husababishwa na kuogopa kukataliwa !!!
namba tano nikweli tupu
kuna mijitu miselfidh acha ..yan imesoma ina ela ina makila kitu ila kuoa anasema nimlete demu tu apa ale matunda ya jasho langu kwan tulikesha wote darasan? ye anachojua nikwamba demu akija bas atafaidi vya bure!!
sure wengine hawajiamini na ili tatizo la uhanisi nw days ndo lawamaliza waume zetu mwee!!
 
kwa watu wengine kuoa au kuolewa it's a matter of choice. Kama wewe uliyetumia uhuru wako kuoa ama kuolewa vivyo watu hutumia uhuru huo kuchagua kutooa. Sio lazima kuoa. Watu wengine simply hupenda kuishi wenyewe.
 
Sidhani kama ni kweli hayo..

Mimi na dhani ni mtazamo tu.. Hakuna sababu ya msingi ya kuchelewa kuoa....
 
mara nyingi sababu zinazowafanya wanaume wasioe ni kuogopa majukumu mengi yanayoambatana na suala zima la kuoa: majukumu hayo ni pamoja na kutafuta mchumba, kufanya maandlizi ya harusi, kuandaa maisha yenu na ya familia yenu (kama mkijaaliwa kupata watoto) hapa ni pamoja na kuhakikisha familia ina mahali pa kuishi, chakula , mavazi, elimu, afya n.k. n.k., kuwa tayari kukabiliana na mambo kama magomvi na kuyatatua, vikwazo katika ndoa n.k., majukumu ya kuhudumia extended family (ya mke na ndugu zake na wa mume pia) n.k. n.k. majukumu haya yote yangekuwa yanaepukika na still ukawa na mke nakwambia kusingekuwa na bachelors mitaani! otherwise kama ni suala la kupika na kufua na kufanya ngono basi majawabu ya hayo yote yapo kuna house keepers wanaweza kufua na kupika, hotels zipo, madobi wapo, sex workers wapo n.k. lakini kuoa is more that that
 
kweli kabisa kaka.....pia kwa mtazamo wangu matokeo makubwa zaidi ya kuoa ni kupata watoto, mara nyingine mimi nadhani kama una-sibling wa kutosha suala la kuendeleza uzao linakuwa halina utata kwani genes zako zitaendelezwa na nduguzo. hivyo kimsingi unaweza usioe ukaishi tu haya maisha ya ki-bachelor mahitaji mengine yanakuwa covered kama ulivyosema hapo juu.
 
Ushauri kwa vijana

Oeni mapema ili majukumu ya kulea na kusomesha muyamalize kabla ya kustaafu.

Sisi tulio saa 11 za jioni tunaona taabu ya wenzetu wanaostaafu wakiwa na watoto darasa la pili. Kasheshe.
 
Wanaume wengine wachoyo na wengine hawajiamini, anaona nitawezaje kuwa na mtu humu ndani kila siku.
 
Back
Top Bottom