Sasa umekuwa mswaada wa mabadiliko ya chadema na si mabadiliko ya katiba

sajosojo

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
1,017
619
[h=6]Bunge la 10,Mkutano wa 5,Kikao cha 6
Mpaka bunge linahairishwa mi sijaelewa nini kinaendelea Bungeni
Hivi ni kweli hawa wabunge wamejipa japo muda kidogo wa kukisoma walichokiongea?
Maana kila mbunge anayeinuka muda mwingi anautumia kurusha vijembe kwa CHADEMA na Jukwaa la Katiba,na muda mchache anaoutumia kuchangia muswada,anaonekana wazi hakujiandaa kuongea anachoongea,anajikanyagakanyaga tu,hata vitu vya ku-refer tu anababaika kutafuta reference,ilhali makabrasha anayo mezani
Na leo naona makofi sio kivile ishara tosha kuwa wao kwa wao wanaona wachangiaji 'wanafuka',muda ambao mchangiaji anapigiwa makofi ni pale anaporusha vijembe kwa CHADEMA.
Au huu ndo mjadala wenyewe wa muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba?
Mimi ni kilaza lakini pamoja na ukilaza wangu katika waliochangia leo hamna anayestahili hata kuwa afisa mtendaji wa kata yangu.[/h]
 
Mbele ya Bi Kidude waongee nini maana na yeye ni kama amejichoka tu
 
Ukweli ni kwamba ccm wamefilisika kisiasa. Uongozi wa nchi umewashinda, sasa wanatafuta mchawi! Ni aibu hata kusema tuna serikali, wameoza wote. Wanajidanganya ya kuwa watu wanawapenda na waliwachagua. Wengi wao wameingia bungeni kwa kuchakachua, hawakubaliki hata na watoto wa chekechea. Uamuzi mgumu lazima ufanyike ili kuikomboa nchi yetu. La sivyo vizazi vijavyo vitatulaani. Na hata kurudia uchaguzi kwa katiba iliyopo ni kupotezeana wakati. Inasikitisha lakini kila chema kinapatikana kwa taabu. Tukubali kufanya maamuzi ili sauti ya umma isikike. Ole wao wanaofikiri Tanzania ni nchi yao. Dawa iko jikoni!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom