Easyway
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 2,606
- 3,702
Utoaji mkubwa wa rushwa kwenye uchaguzi wa CCM kuanzia wilayani,mikoani na sasa kwenye ngazi ya taifa hususani kwenye UWT na UVCCM si jambo la kificho na bahati mbaya hakuna wa kudhibiti rushwa hapa nchini,taasisi ambayo inatakiwa kudhibiti rushwa ilishakufa siku nyingi,makamu wa rais analalamika,rais naye analalamika,rais anakemea rushwa hachukui hatua yoyote.
Rushwa ambayo imebakia ni kwenye uchaguzi wa jumuiya ya wazazi ya CCM, nafikiri nayo wajumbe wanaisubiri kwa hamu!,na tutegemee kiongozi atakayefungua mkutano wao naye kukemea rushwa ni mwendo wa kukemea tu hakuna kuchukua hatua.
Anayetoa hizo fedha anafahamika na mawaziri wa Kikwete sasa wamekuwa mawakala wa kugawa fedha za rushwa , hakuna wa kuchunguza tuhuma hizi wala wa kuchukua hatua, ni upepo tu utapita.
Kwa jinsi rushwa ilivyo tawala na hakuna wa kuidhibiti basi uchaguzi mkuu wa 2015 utavunja rekodi ya matumizi makubwa ya rushwa kwa sababu CCM imeacha watoa rushwa watambe na washinde kwenye chaguzi zake.
Sasa tumekuwa taifa la rushwa la Afrika mashariki.