Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Kwa karibu mara tatu sasa ndani ya miezi hii minne tumeshuhudia mchezo fulani ambao kidogo umeanza kukera. Pinda anacheza peke yake na kila akimpatia Rais afunge goli, rais siyo tu hafungi goli hataki kucheza! Kwenye sakata la Jairo Pinda alifanya alichoweza kufanya lakini mwisho wa siku akatuambia kuwa Rais ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuchukua hatua mara moja na kweli hata Rais aliporudi toka Afrika ya Kusini hakuna lililofanywa zaidi ya Jairo kusimamishwa na Katibu Mkuu Luhanjo.
Lilipokuja suala la mgomo wa madaktari Rais Kikwete aliondoka na kusafiri kwenda nje tena na akiwa huko mgomo uliiva huku Pinda akiachiwa jukumu la kutengeneza jambo hilo. Alijitahidi Pinda hadi ukomo wa madaraka yake - hakuwa na uwezo wa kumwajibisha Waziri yeyote na kwa kweli hakuwa na uwezo wa kuwawajibisha madaktari wote - kama alikuwa nayo basi hayakuwa wazi baada ya kuwafukuza madaktari kazi lakini hawakufukuzika! Lakini katika sakata lile la madaktari mwisho wa siku Waziri Mkuu akampasia Rais Kikwete mpira na safari hii Rais akacheza kama pele kwa kuwapiga mkwara wake madaktari na kuwalazimisha kurudi kazini. Madai yao ya kutaka Waziri na Naibu wake waondoke yakipuuzwa! Wote bado wapo na wanaendelea na kazi. Hakutaka kucheza.
Sasa suala la ripoti za CAG kwa mara nyingine limefunua yale yale tunayoyajua - hakukuwa na jipya. Lakini wabunge na wananchi walianza kupiga kelele sana. Siku ya Jumamosi kelele hizo zilizidi kiasi cha baadhi ya watu kuripotiu kuwa mawaziri kadhaa walikuwa wanajiuzulu na wengine wakisema pia kwa uhakika kuwa tayari wameshajiuzulu. Hili pia lilitokea wakati Kikwete akiwa nje ya nchi na huku nyuma ni Waziri Mkuu PInda akiachwa kukiona cha moto. Nina uhakika wa asilimia 100 kuwa kama Rais angekubali mapendekezo ya wabunge wa CCM kuwa mawaziri watoke wangetoka lakini pamoja na Pinda kuwa matatani Rais hakutaka kucheza.
Rais sasa yuko pagumu kwani ni wazi kuna njia mbili tu za kutokea (ya tatu ni ile niliyoileza kwenye mada ya 'no half revolutions'). Kwanza ni kuvunja baraza la mawaziri na kupata waziri mkuu mpya hili litaturudisha kwenye 2008. Bahati mbaya utaona kuwa tukio la 2008 lilitokea karibu miaka miwili na miezi kadhaa baada ya ushindi wake. Hili la mwaka huu kama likitokea litakuwa nalo limekuja karibu muda ule ule tena kiasi cha kutuaminisha kuwa miaka miwili ya miezi kadhaa ndio maisha tu ya baraza lake kabla halijaanza kuboronga! Ndugu yangu Mchambuzi anaita hiki ni "instability" ya serikali. Njia ya pili ni kufanya "mabadiliko makubwa" yaani kuwaondoa baadhi ya mawaziri bila kumuondoa Waziri Mkuu. Sasa akimuondoa Waziri Mkuu atajipa kazi ngumu zaidi kwani wakati Lowassa aliondolewa kwa kuhusishwa na kashfa ya Richmond, Pinda aweza kuondolewa kwa kutokuhishwa na kashfa yoyote yeye mwenyewe bali kuwa alama ya serikali iliyoshindwa.
Kuendelea hivi hivi kama ilivyo sasa inawezekana ndio option yenyewe kwa sababu maneno aliyoyasema Makinda leo yanaweza kuwa ndio sentiment ya Rais pia - kusemwa wanakosemana hakujalishi kama ni ukweli au ni uzito mawaziri na watendaji wa serikali wasijali sana kwani ni sehemu tu ya majukumu yao. Lakini kujaribu kubadilisha kwa namna yoyote ile kutathibitisha tu kuwa bado Rais Kikwete hajapata dawa ya matatizo katika uongozi wake na sasa ameamua kubadilsiha chupa tu na label tu lakini kilichomo ni kile kile.
sasa afanye nini?