Sasa nimejiridhisha,mradi wa kigamboni ni magumashi

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
944
545
WAKUU,
Niliwahi kusema hapa kuwa nimeona doa kwa Mama Tibaijuka kwa namna ambayo anashughulikia mradi wa Kigamboni.Leo katika kipindi cha Generali On Monday nimethibitisha hofu yangu hiyo kupitia kwa wazee wanaowawakilisha Wanakigamboni.Wazee hawa ambao wanaonyesha wanaijua sheria vya kutosha wanasema serikali haiko wazi kwao na haifuati sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 katika kutekeleza mradi huo.Wazee hawa wanadai kuwa walimtaka Tibaijuka awe wazi na afuate sheria hiyo.Walipoona anakiuka sheria wakamtuma mbunge wao akawasemee bungeni na si kweli kuwa mbunge hakutumwa na wanakigamboni kama baadhi ya madiwani wa manispaa ya Temeke walivyodai.
Mimi naona Mhe.Tibaijuka hajui kuwa hapa bongo ni usanii kwa kwenda juu; kwa hiyo anafikiri wanao mshauri wana nia njema au yeye mwenyewe ameamua kushiriki ufisadi
 
Back
Top Bottom