Sasa nimefahamu maneno yatoayo machozi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079
*SASA NIMEFAHAMU*

*MANENO YATOAYO MACHOZI*



MAMA MUHIMU SANA.jpg



"Mama anaongea na mwanawe na kumpa *Usia"*

Mwanangu mpenzi:

Kuna siku utanikuta uzee, sitafanya mambo yangu kwa akili;

Yakitokea hayo nakuomba tafadhali nipe muda na *subira ili unifahamu !!*

Pale mikono yangu itakapotetemeka, na chakula changu kikaangukia kifuani pangu, na nisipoweza kuvaa nguo zangu;

Jifunge na *kusubiria, na kumbuka miaka imepita nilikuwa nakufunza ambayo leo siwezi kuyafanya!!*

Ikiwa leo si maridadi na sina harufu nzuri; usinilaumu.. kumbuka udogoni kwako nikijitahidi sana nikufanye uwe maridadi mwenye harufu nzuri!!

Usinicheke utakapoona ujinga wangu na
kutofahamu mambo ya wakati wenu huu, lakini wewe kuwa jicho na akili yangu ili niyapate niliyoyakosa!!

Mimi ndiye niliyekufunza adabu na mimi ndiye niliyekufunza vipi ukabiliane na maisha;

*Sasa inakuaje leo unanifundisha yaliyo wajibu na yasiyo wajibu?*

Usinichoke kwa udhaifu wa kumbukumbu yangu, na uchelewaji wa *maneno yangu na fikra zangu* wakati ninapozungumza nawe, kwani furaha yangu wakati huu ni kuwa pamoja nawe tu!!

*Wewe nisaidie tu kupata ninachohitaji;* kwani bado najua ninachotaka!!

Miguu yangu ikikataa kunipeleka sehemu ninayotaka kwenda; *nihurumie* na kumbuka kwamba mimi nilikushika sana mkono ili uweze kutembea!!

*Usione haya abadan kunishika mkono wangu leo;* kwani kesho utatafuta wa kukushika mkono wako!!

Katika umri wangu huu; elewa kuwa mimi siyaelekei maisha kama wewe; lakini kwa ufupi nangojea mauti; kwa hiyo *kuwa pamoja nami wala usinitupe!!*

Pale ukikumbuka makosa yangu; jua kuwa mimi nilikuwa sitaki ila maslahi yako!!

Na mimi napenda sana unayonifanyia hivi sasa kwa *kunisamehe matelezo yangu na kusitiri aibu zangu..*

*NAWE MOLA AKUGHUFIRIE NA AKUSTIRI!!*

Bado *vicheko na tabasamu zako vinanipa furaha* kama ulivyokuwa mdogo...
kwa hiyo usininyime suhuba yako!!

Nilikuwa nawe wakati *unazaliwa;* kuwa nami pale *nitakapofariki!!*

*Maneno bora yaliyopitia katika maisha yangu, na hata nikiyarudia mara elfu moja sichoki kuyasoma..*

"Mola wangu warehemu wazazi wangu kama walivyonilea nilipokuwa mdo"

(Rabbi Arhamu humma kama rabayan swakhira)

*MANENO MAZITO KWA MWENYE AKILI*

*SASA NIMEFAHAMU*
 
Back
Top Bottom