Sasa ni Zamu ya Wazanzibar...

Je, UVCCM huwa ni chombo cha Muungano pia au Bara tu maana wala hatuwasikii Wa-Tanzania Visiwani kwenye nafasi za juu miaka yote mle??
 
WANASHERIA, wanasiasa na wananchi wa Zanzibar wametaka ziundwe tume mbili tofauti kuratibu maoni ya Katiba mpya ili kuepusha Zanzibar kufunikwa katika suala la kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano.
Kauli hizo zimetolewa jana mjini hapa katika mfululizo wa mijadala ya Katiba mpya iliyofanyika katika ukumbi wa EACROTANAL.
Wakili maarufu Zanzibar, Awadh Ali Said, alisema kwa kulingana na mazingira ya Zanzibar si busara maamuzi kuhusu Katiba ya Muungano yakatokana na mawazo ya jumla kati ya wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema idadi ya Wazanzibari ni wachache na kwa msingi huo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iunde tume yake kukusanya maoni ya Wazanzibari na upande wa Tanzania Bara uunde tume yake, ili kuwe na usawa katika suala hilo nyeti.
“Zanzibar haitanufaika, serikali iunde tume yetu itakayokusanya maoni na upande wa pili wa Muungano uunde tume yao ili kuwe na usawa katika kuamua aina gani ya Muungano na mfumo wake,” alisema Wakili Said.
Omar Mussa Makame, alisema Wazanzibari lazima wawe tayari kupigwa mabomu, lakini lazima wasimame imara kutetea masilahi yao ndani ya Muungano.
Alisema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hatawapiga mabomu Wazanzibari wakikataa Muungano, lakini alisema Muungano huo si halali na hakuna mtu atakayeweza kuitetea Zanzibar zaidi ya Wazanzibari wenyewe.
Mjumbe mwingine wa mjadala huo, Ahmada Omar Khamis, alisema ushirikishwaji wananchi wa Zanzibar katika kuandaa na kuandikwa Katiba ya Muungano mwaka 1964 haukuwa mzuri na ndilo chimbuko la matatizo mengi yanayojitokeza hivi sasa.
Alieleza kwamba tume za Jaji Nyalali na Kisanga zilikuja na ripoti za kutatua kero za Muungano, lakini kwa vile tume hizo zilianzishwa kiujanja ujanja ripoti zao hazikutekelezwa wala kusaidia kutatua kero hizo.
Alisema jambo la busara kwa tume za kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya ziwe mbili, ili Tanzania Bara iwe na yake na Zanzibar iwe na tume yake.
Naye, Dk. Omar Juma Khatib alisema katika mabadiliko ya Katiba suala la wakuu wa mikoa kuteuliwa na rais libadilishwe na badala yake wapatikane kwa kupigiwa kura na wananchi ili wawajibike vizuri.
Alisema kuna mataifa yanafanya hivyo ikiwemo Marekani, badala ya kuendelea na utaratibu wa viongozi hao kuteuliwa na rais.
Naye, mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), Juma Sanani, alisema wananchi wa Zanzibar hawapaswi kuangalia upungufu katika Katiba ya Muungano pekee, bali hata Katiba ya Zanzibar ina matatizo mengi ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika mjadala huo.
“Huwezi kubadilisha Katiba ya Muungano bila ya kugusa Katiba ya Zanzibar, ni vizuri wakati huu tukajadili na Katiba ya Zanzibar,” alishauri.
Mjadala huo mkali uliibuka katika majadiliano hayo baada ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ibrahim Mzee kuwasilisha mada ya ‘Katiba za Tanzania na Zanzibar, changamoto juu ya mianya na utata uliopo”, ambapo alisema vifungu vingi vya katiba vina utata.
Alisema miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na kile kinachompa mamlaka Rais wa Muungano kuunda Baraza la Mawaziri kwa kushauriana na Waziri Mkuu na kumuweka kando Rais wa Zanzibar, wakati Serikali ya Muungano ni zao la kuungana Tanganyika na Zanzibar.
Aidha, alisema kwamba kifungu kinachoweka utaratibu wa kumpata rais wa Muungano na makamu wake kina utata, kwa vile hakitamki iwapo rais katoka Tanzania Bara, makamu atoke Zanzibar na badala yake kinasema atoke upande mwingine wa Muungano.
Alisema katika tafsiri ya Kiswahili sehemu nyingine inaweza kuwa eneo lolote ndani ya Jamhuri ya Muungano na si lazima iwe Zanzibar au Tanzania Bara.
Katibu huyo wa Baraza la Wawakilishi alisema kwamba Ibara ya 21 ya katiba hiyo haikuweka mipaka katika suala la uteuzi wa mawaziri na rais wa Muungano anaweza kuwateua mawaziri kutoka Zanzibar katika wizara zisizohusu mambo ya Muungano.
Alisema hali hiyo inajitokeza hivi sasa kutokana na muundo wa wizara hizo kuhusisha mambo yasiyokuwa ya Muungano, kama vile Wizara ya Ulinzi na ya Mambo ya Ndani.
Mzee alisema katika Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo inaongozwa na Mzanzibari, kuna idara za vikosi vya Magereza na Zimamoto, ambavyo si mambo ya Muungano, sawa na Ulinzi ambako kuna Jeshi la Kujenga Taifa, ambalo si katika mambo ya Muungano.
Alieleza kwamba upungufu mwingine wa kikatiba hiyo ni kesi za uchaguzi kwa wabunge hata wale wa Zanzibar kutakiwa zisikilizwe na Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati suala la Mahakama Kuu halimo katika orodha ya mambo ya Muungano na Zanzibar ina Mahakama Kuu yake.
Alisema kwamba imefika wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibadilishwe ili itoe nafasi kwa mgombea binafsi ili kukuza demokrasia.
Akizungumzia ibara ya 98 ambayo imeweka sharti la kupatikana theluthi mbili ya wabunge kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika kuongeza au kuondoa mambo ya Muungano alisema hilo si sahihi. Alisema iwapo upande mmoja wa Muungano umeamua kuliondoa suala lolote katika mambo ya Muungano hakuna haja ya kulazimishwa kupatikana theluthi ya wajumbe kutoka upande mwingine. Katibu huyo wa Baraza la Wawakilishi alisema upande mmoja katika makubaliano unapoamua kuliondoa jambo katika orodha ya mambo ya Muungano kuna kuwa hakuna tena makubaliano na si sahihi kulazimisha kupatikana theluthi mbili ya wajumbe kutoka pande hizo.
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.

acheni tamaa uledi,raisi, mahakama na bunge mnavyo shida nin? huku bara asilani msitegemee kabisa.
 
Mambo ya zamu yanatoka wapi kwenye demokrasia ya vyama vingi. Tena Zanzibar imefanya vizuri kutangaza wazi kuwa ni nchi na dola yenye mipaka inayojulikana na kutambuliwa. Swala kubwa ni kupunguza mambo ya Mwungano kuwa kama yalivyokubaliwa mwanzoni bila nyongeza. Hapo swala la zamu halitakuwepo. Sijui kama kuna mwana CDM katika kamati kuu yao toka ZNZ ambaye ataweza kusimama kama mgombea. CCM labda, hivyo maombi haya yaelekezwe huko. Halaf mchakachue matokeo.

Ikiwa unatka kupunguza mabo ya muungano kama tulivyokubaliana mwanzo basi itabidi tulete serikali tatu,kutakuwa na rais wa tanganyika ambaye anatoka upande wenu siku zote,pia kuna rais wa zanzbar,na rais wa muungano tunapokeza kila baada ya miaka mitano,ikiwa rais wa muungano atatoka zanzbar makamo atatoka tanganyika,pia rais wa muungano itakuwa haina haja ya kupiga kura.

Kutakuwa na kura ya kuchangua rais wa tanganyika na zanzibar tu,suala la rais wa muungano,itakuwa hivi,,rais wa zanzibar moja kwa moja atakuwa rais wa muungano kwa muda wa miaka mitano na rais wa kanganyika atakuwa makamo wa kwanza wa muungano,baada ya miaka mitano rais wa tanganyika atakuwa rais wa muungano na zanzibar atakuwa wa makamo.

Kila nchi tunataka iwe na kiti chake katika mumoja wa mataifa,kila nchi iwe na balozi zake njee zanzbar na tanganyika,,,hatutaki ubishiiiiii

Katika wabunge hatutoitaji wabunge kwa kupiga kura pia kwa sababu kila nchi itakuwa inajiendesha wenyewe,na ina rais wake na mawaziri wake na wawakilishi wake kila nchi,tutahitaji mawaziri wa tanganyika na zanzibar ndio waingie bungeni,pamoja na wakilishi,kila upande itateuwa wawakilishi wao na mawaziri waweze kuwakilisha katika bunge hilo

Hapo ndio tutaondoa ulalamishi,,na muungano utadumu,,na tutaudumisha..

Lakini mufahamu wazanzibar wa leo sio wa mwaka 1964 ,,,tumeamka musitupeleke kama chadem hapa,,zanzbar ni nchi toka nyerere hajazaliwa.
 
Mlishamtoa Alhaj Hassan Mwinyi, msubiri mpaka mikoa yote iliyobaki ya bara itoe rais ndio na nanyi mtafikiriwa

Wewe inaonyesha una chuki ndani ya moyo wako na wazanzbari,,,lakini nakuambia kitu kimoja,ikiwa maneno yako unaongea moyoni mwako basi maisha wewe hutofanikiwa na ukifanikiwa mtoto wako atapata shinda kutokana na roho yako mbaya,huna hoja wewe ya kuongea,sijui kama hata umesoma wewe,,,hujui elimu ya shule,wala msikitini wala kanisani unaishi ishi tu..

Sisi wanzanzibari tutaendelea kutoa ufahari wetu kama wanzanzibari kwa sababu ni nchi yetu hiii,hatuwezi kuukana utaifa wetu kama nyerere alivyoukana utanganyika,naaamini watanyangika wanaitaka nchi yao,,,hata G55 walikuwa ni watanganyika ambao walitaka serikali tatu.

wewe unaonekana wa kuja sio mtanzania wala mtanganyika,ni msumbiji weweeeeeee
 
..ikiwa Raisi wa muungano atatoka Zanzibar basi tutakuwa tunadumisha muungano kitu ambacho wa-Zanzibar wanapingana nacho.

..pia suala la kupokezana linakwenda kinyume na dhana nzima ya Demokrasia.

..kama wa-Zenj wana nia ya kugombea nafasi ya Uraisi wa muungano basi wajitangaze kwa wapiga kura wa Tanzania nzima.

..Raisi wa Tanzania atakayetokana na kura milioni 1 za wa-Zanzibari atakuwa na wakati mgumu sana wa kukubalika miongoni mwa wa-Tanganyika milioni 35.
 
Back
Top Bottom