Sasa ni Zamu ya Wazanzibar...

Muungano hakuutaka nyerere bali wazanzibari wenyewe, Tanganyika inapakana na nchi nyiiingi zana kwa nini iungane na zenj tu si wametaka wenyewe, ina ardhi hata ndege atapata ikiwa itaamua klugawiwa-

Wazanzibari hawajawahi kuutaka huo Muungano kama unavyodai lakini walitiwa kwenye Muungano kwa utashi wa kiongozi wao na kwa upande wa pili mliwahi kuujadili na kuupiitisha hata kama nyie sio mlioutaka?
 
Hao ni sawa na ngamia wa jangwani aliyeomba aiingize kichwa tu kwenye hema ili ajinusuru na mvua ,baadaye mwenye hema akajashutukia keshatolewa nje,hapa bara wamejaa na vidaladala vyao lakini thubutu nawewe upeleke chai maharage huko kwao utafanyiwa mtima nyongo mpaka utakoma
DUH hawa wengine hawajui hata maana ya Tanzania ( TAN ZAN ia)
 
Niwazavyo huu utatu hauna maana sana na sioni manufaa yake kwa sasa labda hapo kale...maana kale ilidhaniwa ardhi ya visiwa vya Z'bar ingeweza kutumika kuishambulia Tanganyika kirahisi! ila kwa maendeleo ya kiteknolojia ya sasa unaweza kushambuliwa kutoka kona yoyote mathalan mshambuliaji anajua shabaha yake vyema! kwa kutumia haki yangu ya msingi kikatiba ibara ya 18 B ,nasema huu utatu ni batili!
mkuu.
Tukitokea wengi ambao tutatoa sauti kusema huu muungano tulionao haufahamiki Muundo wake wala uendeshaji wake.

na kuwambia watawala kuwa sasa ni wakati muafaka uje mjadala wa Muungano na muundo wake basi itakuwa ni hatua nzuri sana.

Hivi sasa tunajadili zaidi muungano kama Simba na yanga na sio mijadala ya tija .
Sote tunajua kuwa muungano huu tulionao umelalamikiwa sana kwanza na wazanzibari, baadae Rev.Mtikila na G55 ni wazi watu wa pande mbili wanaona lipo tatizo juu ya aina hii ya muungano tulionao lakini CCM wamefanya ni mali yao na kila anayepaza sauti kusema "wakuu, tumejenga nyumba ya karata" ukija upepo tumeipoteza wanakuona mhaini au kichaa.

Sasa tutokee wengi na tuseme bila woga kuwa huu Muungano wa usanii na ujanja ujanja hautufai tena. sifikirii kuwa watu wanakataa muungano lakini watu wanataka Muungano unaofahamika na wenye tija. Ndio sababu sisi kama TZ tunapeleka timu yetu kwa majadiliano katika EAC na sio Kenya waamue sisi tufate tu.
 
Mlishamtoa Alhaj Hassan Mwinyi, msubiri mpaka mikoa yote iliyobaki ya bara itoe rais ndio na nanyi mtafikiriwa
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.

It is the ability that counts, not the locality!!!
 
Nafasi yao ya makamu wa raisi hawaihesabu kila msimu wameisahau... au?
Wao wawe na raisi wao mzenj kila msimu halafu sisi tuletewe mzenji kuwa rais wa bara hiyo aina uwiano... waache wanogewe na favor tunayowapa kama watanganyika kwa kutaka ndoa yetu idumu. Ila raisi wetu Awe MBARA na sio MZENJI.
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.
hivi karatu washawahi kutoa raisi? nafikiri ni zamu yao sasa tuwaachie lol
 
Niwazavyo huu utatu hauna maana sana na sioni manufaa yake kwa sasa labda hapo kale...maana kale ilidhaniwa ardhi ya visiwa vya Z'bar ingeweza kutumika kuishambulia Tanganyika kirahisi! ila kwa maendeleo ya kiteknolojia ya sasa unaweza kushambuliwa kutoka kona yoyote mathalan mshambuliaji anajua shabaha yake vyema! kwa kutumia haki yangu ya msingi kikatiba ibara ya 18 B ,nasema huu utatu ni batili!

Well said,tufikie mahali huu mjadala wa muundo wa muungano urudishwe mezani ujadiliwe kwa uwazi..
 
Zanzibar in Rais wake ambaye ni Mzanzibari, mnataka Mzanzibari aongoze Tanganyika kwa kivuli cha Muungano? Hilo haliwezekani kabisa! Mwinyi ndiye wa mwisho kuongoza Tanganyika. Haitatokea tena. Muache kabisa hiyo ndoto!
 
Utaratibu wa Tanganyika na Zanzibar kuwa na zamu ya kuwa na Rais wa Muungano uliwezekana wakati CHAMA KIMOJA KIKISHIKA HATAMU. Baada ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa haiwezekani kuwa na zamu tena.
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.

Did you mean CCM?......... Maana siamini kama kwenye uchaguzi wa kidemokrasia ndani na nje ya vyama unaweza kukipangia kila chama kinachoshiriki uchaguzi kutoa nafasi maalum ya upendeleo kwa watu wa sehemu moja ya Muungano. Nafikiri mtazamo kama huo hauna maana tena siku hizi kwa kuwa Urais ni majukumu na si zawadi useme kama leo kapata Mke Mkubwa basi kesho apewe Mke mdogo.

Ukiangalia vizuri utagundua kwamba fikra za kubalance mgawanyo wa viongozi kwa vigezo kama pande za muungano, kabila, dini, mkoa nk vinatuumiza bure kwa kuwa viongozi wanatakiwa kuwa wachapakazi, waadilifu na wapenzi wa dhati wa Tanzania kama taifa na si vinginevyo.

Ikitokea tukapata viongozi hata mia moja mfululizo kutoka eneo dogo kama Mafia au Ukerewe ni sawa tu kama watu hao wataweza kutusaidia kutatua matatizo makubwa tuliyonayo kama; ufinyu wa maarifa ya kuleta maendeleo kwa taifa(mingoni mwa viongozi wa kitaifa), ufisadi, umeme, barabara, maji, umasikini, elimu duni, huduma za afya nk itakuwa faraja kubwa sana kwa wapenda maendeleo kuliko anakotokea rais.

Watu wenye mtazamo wa kudhania urais ni swala la zamu ndo wamesababisha debate kubwa sana kuhusu utawala hapa nchini. Wakati mmoja analalamikia utawala mbovu, mwingine anachowaza ni kwa nini wanamsumbua rais wakati hii ni zamu yetu. Zamu yenu kufanya nini? Maendeleo na hali ya nchi ni swala nyeti sana kuliko nani ana madaraka leo na nani hana.
 
Mlishamtoa Alhaj Hassan Mwinyi, msubiri mpaka mikoa yote iliyobaki ya bara itoe rais ndio na nanyi mtafikiriwa
Hatuendi hivyo! Mkowa wa Pwani umeshatowa mara mbili, Kikwete na Ali Hassan Mwinyi. Mwinyi hakuwa Mzanzibari bali alikuwa muhamiaji tu.
 
Did you mean CCM?......... Maana siamini kama kwenye uchaguzi wa kidemokrasia ndani na nje ya vyama unaweza kukipangia kila chama kinachoshiriki uchaguzi kutoa nafasi maalum ya upendeleo kwa watu wa sehemu moja ya Muungano. Nafikiri mtazamo kama huo hauna maana tena siku hizi kwa kuwa Urais ni majukumu na si zawadi useme kama leo kapata Mke Mkubwa basi kesho apewe Mke mdogo.

Ukiangalia vizuri utagundua kwamba fikra za kubalance mgawanyo wa viongozi kwa vigezo kama pande za muungano, kabila, dini, mkoa nk vinatuumiza bure kwa kuwa viongozi wanatakiwa kuwa wachapakazi, waadilifu na wapenzi wa dhati wa Tanzania kama taifa na si vinginevyo.

Ikitokea tukapata viongozi hata mia moja mfululizo kutoka eneo dogo kama Mafia au Ukerewe ni sawa tu kama watu hao wataweza kutusaidia kutatua matatizo makubwa tuliyonayo kama; ufinyu wa maarifa ya kuleta maendeleo kwa taifa(mingoni mwa viongozi wa kitaifa), ufisadi, umeme, barabara, maji, umasikini, elimu duni, huduma za afya nk itakuwa faraja kubwa sana kwa wapenda maendeleo kuliko anakotokea rais.

Watu wenye mtazamo wa kudhania urais ni swala la zamu ndo wamesababisha debate kubwa sana kuhusu utawala hapa nchini. Wakati mmoja analalamikia utawala mbovu, mwingine anachowaza ni kwa nini wanamsumbua rais wakati hii ni zamu yetu. Zamu yenu kufanya nini? Maendeleo na hali ya nchi ni swala nyeti sana kuliko nani ana madaraka leo na nani hana.

Hili la malalamiko ya watu wa namna fulanmi mbona nayaona sana hapa jamvini mwetu. Kwa vile wewe ni mgeni hapa basi jizoweshe na hali hiyo. Fatilia nyuma hutofika mbali utakuta Thread kuwa Waislamu wanapendelewa na upande mwengine Waislamu tunanyimwa nafasi pahala fulani mara ooh sisi ndio Wapinzani hivyo nafasi zote ni zetu. Hatujafikia hali ya Kidemokrasi kama unavyofikiria.
 
Utaratibu wa Tanganyika na Zanzibar kuwa na zamu ya kuwa na Rais wa Muungano uliwezekana wakati CHAMA KIMOJA KIKISHIKA HATAMU. Baada ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa haiwezekani kuwa na zamu tena.

Bado tuko katika mfumo uleule kwani bado CCM wanaendelea kuongoza na hao wanaotaka huo mzunguko na hata wanaopinga wanakusudia Rais kutoka CCM.
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.[/QUO

AMA NYIYI KWELI MWAPENDA KUJIFURAHISHA? HAKUNA MZANZIBAR MZANZIBAR MZANZIBAR HATA MOJA MWENYE HAMU YAKUWA RAIS WA TANGANYIKA TAGETI YA WAZANZIBAR NIKUONDOKANA NA HILI JINDAMIZI LA MUUNGANO FAKE KAMA NYIYI WENYEWE, NILINI HASA KTK KUMBUKUMBU ZENU MZANZIBAR KUWA RAISI WA TANGANYIKA?.
JEE ALI HASSAN NI MZANZIBAR? NYIYI DAINI KATIBA MPYA SISI TUKO KTK KUVUNJA MUUNGANO,CHAKUSHANGAZA SISI TUNA RAIS WETU NA BENDERA NA WIMBO WA TAIFA NA MENGINE YAKUWA NCHI NA TUNATAKA KUVUNJA MUUNGANO, NYIYI HAMUNA NCHI NA MUNATAKA KATIBA MPYA? KWA NINI MUSIDAI TANGANYIKA YENU KWANZA MULIO IPIGANIA UHURU WA 9DECEMBER1961 MUDAI KATIBA YA TANZANIA? NYIYI WAZIMA VICHWANI LAKINI? SISI HATUPASRADII MUUNGANO TUNATAKA UFEE WAKATI WWTE ITAKUWA URAISI?. THINK TWICE.
 
Hizo ni chuki zako tu...waznz ni watu safii tena sio mafisadi
Slamini naye alikuwa mtu Safi!!!!!!!!!!!! na mwenzie yuele aliyekuwa mshauri wake wa mambo ya biashara hao ndio nadhani wamefundisha wabara kuwa mafisadi
 
Back
Top Bottom