Sasa ni Zamu ya Wazanzibar...

Msipokubali tutauvunja muungano
haya maneno unatakiwa uwataarifu wazenj wenzako-sisi hata kesho hatuna shida-bakini na mafuta yenu na uchafu mwingine-kuna nchi zimeemdelea bila kuwa na mafuta sembuse nyie mtutishe na mafuta yenu
 
nilijaribu kuipitia katiba yetu na siajaona kifungu kisemacho urais ni wa kupokezana bara na zanzibar.tafadhalini ndugu zangu msitake leta chokochoko.zilizopo zatosha

Halafu si wabadili na katiba ili wabara nao waweze kwenda kutawala ZNZ??
 
Haiwezekani kwani 99% ya wazenji ni ustaadhi al-jihad, hatutaki hawa watu kuongoza nchi yetu TENA wawe wametoka visiwani au bara.
Mkuu.
Unaikwepa ban...lakini unaingia katika mtego wa CCM..udini. Wakitokea wa "al jihad" na wao wakisema kinyume cha unachosema huoni tunaiingiza Nchi kule ambako hata wewe kwa kujua maafa yake hupendelei.

Nakumbuka ulipoanza mfumo wa vyama vingi ilikuwa ndio mwisho wa mzenj kuwa Rais wa Serikali ya Muungano...pia yale mabadiliko ya Katiba ya kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamo wa Rais ndio iliua Muungano. Kwa bahati mbaya kila "mtanzania" yumo ndani ya denial..tunaendeleza usanii.

La ajabu zaidi ni kauli za kuwa tuigeuze Zanzibar iwe mkoa au wilaya. Hatukuwa tunafanya review ya Muungano kila mwaka ndio sababu tumejikuta katika hali hii ya leo.Hatujui historia ya Muungano,hatuji tumeungana katika mambo yepi, hatuji nchi zilizoasisi muungano. hatujui hadhi ya muungano..sisi tumo tu kupiga kelele na mayowe.

Hizi kauli za kuwa "al jihad" wa bara au visiwani hawezi kuwa Kiongozi wetu ndio unafukia kaburi la nchi iitwayo Tanzania, tunairudisha "Tanzania bara" au jina lile maarufu la nchi anayoipigania bila aibu na bila kuchoka Rev. Mtikila. na hapo ndio huu "udini" tunaoupalilia na kuupigia matarumbeta ndio utatutafuna vizuri na hayataishia hapo.
 
Mh bahati mbaya sana kwa Zanzibar hilo swala la kupokezana halipo kwenye katiba. Nguvu ya kupokezana ilikua kwenye precedence ila kwa vile precedence hiyo ilivunjwa 2005 kwa Wazanzibar wenyewe kupenda basi meli hiyo isha zama na hakuna mwenye mawazo hayo tena.

Pia kama kuna Mzanzibar ana uwezo na ana kubalika mpigieni tu kampeni kumshawishi watu wamchague si kulazimishe eti ni zamu yenu.

Ila je 2015 na vyama vyote vya upinzani visimamishe Mzanzibar? Maana kuna vyama vingi ati.

Na pia mkuu hilo tishio la msipo pewa raisi 2015 mnavunja Muungano ndiyo mna encourage baadhi ya watu wasi wape maana wengine ndivyo wanavyo taka hivyo.
 
..wagombee kama wenzao wa Tanganyika wanavyofanya.

..upande wa Tanganyika ndiyo wenye kura nyingi ktk uchaguzi wa Raisi wa Muungano.

..kwa kuanza wawe active na kujishughulisha na masuala ya kisiasa,kijamii,na kiuchumi, yanayohusu Tanganyika. hiyo itawasaidia kujijenga kwa wapiga kura wa Tanganyika.

..pia itabidi mhusika aachane na popular rhetoric za huko Zanzibar ambazo huwakashifu wa-Tanganyika, na kuubeza muungano.
 
Hiyo ni sera ya CCM, wao watoe mgombe visiwani hala asimame mbabe mja bara kupitia CDM hivi. Hapo mbona patamu.:A S clock:
 
Hiyo ni sera ya CCM, wao watoe mgombe visiwani hala asimame mbabe mja bara kupitia CDM hivi. Hapo mbona patamu.:A S clock:

Mkuu hata CCM hiyo siyo sera yao la sivyo Kikwete asinge kuwa favorite 2005 mpaka kushinda. Ukweli ni kwamba Mwinyi alipewa 1985 ili Wazanzibar wasi lalamike. Sasa hivi watu wanaelekea kujali uwezo wa mtu na si ana toka sehemu gani ya Zanzibar. Huwezi kuniambia kama the best candidate 2015 ata toka Bara basi asubiri mpaka 2025. Hiyo hybrid democracy baadhi ya Wazanzibar wana taka kuianzisha wai practice Zanzibar kwanza kwa kupokezana Wapemba na Waunguja kwenye uraisi wa nchi yao.
 
Join Date : 16th March 2011
Posts : 9
Thanks 0 Thanked 0 Times in 0 Posts

Rep Power : 0
Uledi,
Nakukaribisha rasmi hapa JF.
 
Nadhani Rais wa mwisho wa muungano toka Zanzibar ni Mzee Mwinyi. Hamna tena biashara hiyo wakati ninyi mnajiita nchi na papo hapo mnatamani kuitawala Tanganyika kama koloni la Zanzibar? Yaani muwe na Rais mtendaji Mzanzibari na mwingine huku Tanganyika? Yaani watanganyika ni mazezeta kiasi hicho?
 
USAHIHI WA 'SIASA ZA ZAMU YETU YA URAIS' NDANI YA MUUNGANO KATIKA
MFUMO WA VYAMA VINGI NA TANZANIA YA SASA YENYE VIJANA
WENGI WAELEWA KAMA WAPIGA KURA


Unachosema ni sawa lakini mpaka kwanza tukaungane kuandika KATIBA MPYA na kupatikana Tume Huru za Uchaguzi kote Bara na Visiwani.

Lakini cha zaidi, huu utaratibu wa kupeana zammu kushika dola ya nchi hii (i) kwanza ilikua ni utamaduni binafsi ya CCM ambayo tayari wamewasaliti sana katika hilo, (ii) ilikua ni utamaduni wa mfumo wa chama kimoja lakini kwa sasa mpaka ushindani ndio kieleweke, (iii) Wagombea urai wenyewe wawe ni WASTAARABU WA SIASA NA WAKOMAVU kuliko hata alivyo hivi sasa Mzee Dr Ali Mohammed Shein.

Hatutarajii hata siku moja mkatuletee MACHEPELE ilimradi tu zamu imeangukia kwenu wala hatutarajii Vicheche WATAFUTAJI MASLAHI BINAFSI kama vile Maalim Seif kuletwa kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haka!!

Hakika, Wazanzibari wakitaka uzamu kuendelezwa basi ni (1) sharti kwanza wananchi sote tuwe kitu kimoja na kuzungumza lugha moja ya mabadiliko ndani ya taifa letu, (2) ni sharti kuwapa wale Wa-Zanzibari wasiofikirika (kwa sababu tu si watoto wa Karume, watoto wa akina Mwinyi ...) nao wapate nafasi ya kugombea kwani tunaamini hapo Visiwani wapo Wa-Tanzania wengi sana ambao huenda wakawa ni watu wazuri kuliko hata Dr Salim Ahmed Salim (ambaye siku zote hufitinishwa na nyinyi wenyewe huko) na Dr Ali Mohamed Shein (mstaarabu namba mbili wa siasa kote nchi Tanzania baada ya Mwl Nyerere, ambaye baada ya kumaliza kazi ya Urais hapo Visiwani ni sharti akapumzike nyumbani na kubaki mshauri wetu tu) au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ambao WAKIPEWA NAO NAFASI wanaweza kukubalika kote nchini kiushindani bila shida.

Nasema kwamba endapo unataka 'SIASA ZA ZAMU YETU' kuzingatiwa na sisi vijana tukayakubali basi (iv) ni mpaka utakapowafikiria watu tofauti na Hussein Mwinyi aliyetuua kinyama kule Gongolamboto na kuendeleza ukaidi wa kutokujiuzulu licha ya kutapakaa damu mikono yake yote, (v) ni sharti umuondoe kabisa kwenye ndoto zako huyu M-Kondoa Shamsi Vuai Nahodha na jinsi alivyotuchinja kule Arusha na Mbeya na kukaidi agizo letu wananchi kwamba ajiuzu bila kusikiliza kitu.

Nikipata nauli nitafika Zenji tukashauriane zaidi juu ya namna gani SIASA ZA ZAMU YETU zinavyoweza kuzingatiwa ndani ya Muungano katika Tanzania yenye idadi kubwa ya vijana waelewa na upevu wa akili na uhuru wa maamuzi.
 
Tunajua hujuma ambayo wabara wanatufanyia sisi watu wa Zanzibar hasa kwa kuhakikisha kila mara makamu wa rais wa muungano anatoka Pemba na pia tunajua jinsi mlivyomnyima rais wetu wa znz asime makamu wa pili wa rais wa muungano ila ukweli unabaki pale pale 2015 ni zamu ya znz najua manasara hawapendi hilo

Manasara? Kumbe muungano umekaa kidini? Kimsingi huna hoja; kasome katiba zote mbili vizuri. Kaka, suala la uongozi wa taifa si la zamu kama mwanaume anavyopangilia zamu za kulala kwa wake zake. Hapa ni suala la uwezo wa uongozi; hata kama marais wote wangetoka Zanzibar miaka yote mimi sina tatizo alimradi watuvushe kutupeleka kunakostahili. Vivyo hivyo, haina tija yoyote kuunga tu mkono kiushabiki kwa kuwa ni rais kutoka bara hata kama ni mbumbumbu na muflisi kiuongozi.

Suala si rais katoka upande upi wa Muungano bali ana uwezo gani wa kuliongoza taifa letu kwa maslahi ya wananchi wote bila kujali hawa ni manasara, kafir, au kundi loloe lile la kijamii.
 
Nadhani Rais wa mwisho wa muungano toka Zanzibar ni Mzee Mwinyi. Hamna tena biashara hiyo wakati ninyi mnajiita nchi na papo hapo mnatamani kuitawala Tanganyika kama koloni la Zanzibar? Yaani muwe na Rais mtendaji Mzanzibari na mwingine huku Tanganyika? Yaani watanganyika ni mazezeta kiasi hicho?
Mkuu.
Hata mimi ninahisi hivyo.Mwinyi ni Mzanzibari wa mwisho kuwa Rais wa Serikali ya Muungano. Lakini usiwalaumu wazanzibari kwa hili.
Makosa aliyafanya Mwalimu kuifuta Serikali ya Tanganyika. Na kuuweka mfumo wa kiajabu ajabu wa Muungano.

Wazanzibari wana kilio cha haki cha kuongoza serikali ya Muungano kwani wao ni wabia lakini sasa hili linakuwa si kitu kinachoweza kueleweka kwa wengi kwa sababu serikali ya Tanganyika haipo na kwa hiyo, serikali ya Muungano, ndio imekuwa serikali ya Tanzania bara"Tanganyika".

Ni jambo la kuchekesha kidogo lakini lina ukweli ndani yake.Nimesoma sehemu kuna wazanzibari wanatoa hoja kuwa Tanganyika ilijibadilisha jina mwaka 1964 na kuwa Tanzania. Hili linaonekana sasa kuwa ni kweli kwa hoja hizi tunazozitoa humu.

Tunapochelewesha zaidi mjadala wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na mfumo wake basi tunakaribisha matatizo zaidi siku zijazo. nafikiri mjadala wa Katiba mpya, ungetanguliwa na mjadala wa Muungano au mijadala hii iende sambamba.

Kwa sababu, Katiba itakayoandikwa bila ya kutilia maanani Muungano na mfumo wake itakuwa ni sawa na kuifuta serikali ya Muungano kinyemela.

Kutokana na tabia ya utendaji na utekelezaji wa kila kitu chetu kama taifa hapa Tanzania, ninachokiona kinakuja ni funika kombe tu kwa sababu hatuko makini na pia hatuko wawazi. Kila kitu kinagubikwa na usiri mkubwa.

Tunachofanya ni kuficha uchafu chini ya zulia. Kila mtu analijua hili lakini tunaogopa kusema "mfalme hajavaa nguo". Huu si ugonjwa wa kuudharau, ugonjwa umekuwa sugu sasa labda tuende kwa "babu".
 
Tatizo la wabara ni kujiona wao ni bora kuliko wengine. tena wanadhani znz haikuwa nchi ilipoungana na tanganyika. Kumbukeni znz imekuwa nchi hata kabla tanganyika haijakuwa nchi.
 
Back
Top Bottom