Takribani wiki kadhaa hivi tumesikia migomo ikifanyika ktk vyuo vikuu kadhaa hapa nchini, kwa majina baadhi UDOM,MKWAWA,DUCE,TUMAIN-IRINGA & DAR, na bila kusahau huko ARUSHA na MOSHI. Kwa kipindi hicho chote UDSM walikuwa wametulia lakini si kwa kuwa wao hawana shida la HASHA bali ukiona kobe kainama ujue.........., Sasa mgomo unakwenda kuanzishwa na wanazuoni hao wa UDSM naona ndio unaokwenda kuhitimisha rasharasha zote za migomo iliyoanzishwa katika vyuo kwa majina hapo juu!