hesaabu zenyewe ziko hivi:
hadi leo amehudumia watu 3,000,000/- x 500 = 1,500,000,000/-!!
Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo
na Mwandishi wetu
ZAIDI ya wagonjwa milioni 3 wamepata kikombe kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila Babu katika kijiji cha Samunge Loliondo wilayani Ngorongoro tangu aanze kutoa huduma hiyo Agosti mwaka jana.
Takwimu zilizotolewa jana na mmoja wa wasaidizi wa Babu, Jackson Dudui, zinaonyesha bado wanategemea idadi kubwa ya wagonjwa kuendelea kumiminika kijijini hapo kufuata kikombe hicho kinachotibu magonjwa sugu na kwamba juzi pekee wagonjwa 17,065 walipata huduma hiyo.
Magonjwa sugu yanayodaiwa kutibiwa na kikombe hicho kinachokwenda na imani zaidi ni kisukari, shinikizo la damu, pumu, saratani na ukimwi.
Alisema jana magari zaidi ya 400 yenye wagonjwa zaidi ya 3000 yalikuwa yakimsubiri Mchungaji Mwasapila atoke kanisani, ili awapatie tiba hiyo mbadala ambapo alieleza raia kutoka Kenya wamekuwa wakimiminika kwa wingi kijijini hapo.
Foleni ya magari si kubwa sana kwa siku ya leo kwani hivi tunavyozungumza yapo magari zaidi ya 400 yakimsubiri Babu atoke kanisani na kuanza kuwahudumia kuanzia saa 8 mchana na hakika atawamaliza leo hii, alisema.
Msaidizi huyo alisema kuwa katikati ya wiki iliyopita walipata ugeni wa wachungaji zaidi ya 10 kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati waliokuwa kijijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano wao mkuu wa mwaka wakiongozwa na Mkuu wa Jimbo aliyetajwa kwa jina moja la Nangole.
Alisema mbali na wachungaji hao kushiriki mkutano huo waliungana na Babu kutoa vikombe kwa wagonjwa waliokuwepo kijijini hapo kupata tiba hiyo.
Habari zaidi zilizopatikana zimeeleza kuwa Babu amepiga marufuku wagonjwa kutoka Kenya wanaosafirishwa kutumia magari yasiyoruhusiwa kama malori na gari ndogo saloon wakiwa wamejazana hali aliyosema ni mateso kwa wagonjwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alieleza kuwa utoaji tiba unaendelea vizuri kijiji hapo, na alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa ukusanyaji ushuru wa magari na helikopta alisema hayo ni mambo ya kisiasa zaidi na kumtaka mwandishi wa habari hizi kusubiri maamuzi ya kikao halali kitakachofanyika leo kijijini hapo.
Alisema bado maamuzi hayajafikiwa kujua ni mamlaka ipi itakayokuwa ikikusanya ushuru huo kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngoromngoro na serikali ya kijiji cha Samunge.
Siwezi kuingia kwa undani zaidi kuzungumzia suala hilo naomba usiandike chochote kwani kesho kutakuwa na kikao kitakachozungumzia suala hilo na tutawapeni taarifa, alisema.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mgogoro wa kugombea ushuru wa magari na helikopta kati ya pande hizo na wakati fulani iliripotiwa kuwa serikali ya kijiji iliwafukuza watoza ushuru toka halmashauri.
source: Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo
haka kazee kana laana! yaani kameanzia utapeli uzeeni na umekachanganyia kweli, duh!!
ama kweli wajinga ndio waliwao, na hapo samunge wameliwa kwelikweli