sasa ni rasmi: babu wa samunge ni bilionea!!

Ha ha haaaaaaaaaaa! Anataka kuwa mshika mafao mkuu! Anajiuliza saa hii angekuwa mrs Mwasapile angekuwa ana ngapi kama babu anazo hizo!
Mkuu,
Kuna aliyeshikwa masikio kwenye thread yake kule, tunamhurumia huyo bwana!
Babu yuko makini bana, hawezani na wababaishi!
 
Dah kwa sasa hivi nikisia habari za babu nasikia uchungu kweli. Anko wangu akiuguliwa na figo ,yupo nachingwea,alivyoona hali si shwari ikabidi aanze safari ya muhimbili. Wakati yupo mtwara kabla hajapanda ndege kwenda daslam, habari za bau zikamkuta hapa,akashawishika,akakata tiket nyiingine hadi Arusha-samunge...baada ya kupata kikombe akarudi zake na amani kabisa kajua kwamba kapona. mwezi na ushehe umepita sasa anataabika kweli hadi juzi nimepata simu ananiomba nimpe details za matibabu India, hali yake si mzuri kabisa na sasa anafanya utaratibu aende india akafanye matibabu ya figo.
Najua watu watasema mambo ya imani n.k lakini tiba yake hadi hivi leo ni kizungumkuti, na magumashi. yaani haieleweki kabisa.!!

ni lini babu alikutangazia anatibu figo?
 
Sio ajabu mganga wa kienyeji kuwa bilionea kwani wajinga ndio waliwao!
Tunaongelea Mchungaji Mwasapile wa Samunge broda!....are we together?
Mambo ya waganga wa kienyeji unayalokota wapi?
Come to the pertinent subject....right?
 
Mtoto wacha kupiga mayowe,waache wayaone wenyewe!
We mtoto wacha kupiga mayoe waache wayaone wenyewe!

Miss judith wapotezee hawa!wameingizwa mjini na hawataki kukubali.iko siku watakukumbuka hata DECI walikataa hivi hivi!
 
Hata dawa ya malaria mseto(ambayo inadaiwa kuwa ya kisasa kabisa) kuna baadhi ya watu inawadhuru, wengine haiwaponyi kabisa, wengine inaweza kuwasababishia kifo!
Kwahiyo kwa kulinganisha tu, mjomba wako ni percentage ni 0.0000000000001 ya watu WALIOTIBIWA na babu na kupata complication hiyo!
Na huenda kuna masharrti alikiuka!
kWAHIYO bWANA sizinga, acha upotoshaji, acha watu wasafiri kwenda SAMUNGE, dawa ya babu inaponya, na hii ni kwa mujibu wa HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI!
Hata hivyo namtakia MJOMBA wetu AFYA NJEMA!

PakaJimmy..umetumia busara kunijibu...Amina!!sasa hivi nimeshaongea na muhasibu wa ubalozini India..Mr Yahya naona atanisaidia sana kwa hili. Namuombea afya njema Anko angu

Infact hii kitu sio upotoshaji bali nimemchukulia anko kama reference, kwamba dawa ya badu haijamtibu...kama wengine imewatibu basi Innshhallah wamepona!!
 
U will wait for your favorable aftermath on this matter for centuries , but too bad, its going to be in vain!
Mungu siye Othman bana!
 
ZAIDI ya wagonjwa milioni 3 wamepata kikombe kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila ‘Babu’ katika kijiji cha Samunge Loliondo wilayani Ngorongoro tangu aanze kutoa huduma hiyo Agosti mwaka jana.
Takwimu zilizotolewa jana na mmoja wa wasaidizi wa Babu, Jackson Dudui, zinaonyesha bado wanategemea idadi kubwa ya wagonjwa kuendelea kumiminika kijijini hapo kufuata kikombe hicho kinachotibu magonjwa sugu na kwamba juzi pekee wagonjwa 17,065 walipata huduma hiyo.

sasa ni rasmi: babu wa samunge ni bilionea!!

Which is which...!

MCHUNGAJI Ambilikile Masapila 'Babu' wa Samunge wilayani Ngorongoro, Arusha amefikishwa vikombe laki tatu wiki hii tangu kuanza kwa tiba hiyo Oktoba mwaka jana, imefahamika. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Msaidizi wa Babu, Bw. Jackson...

Babu atoa kikombe cha 300,000

Watapatikana wengi na kupukutika wengi sana mwaka huu.
 
Hata dawa ya malaria mseto(ambayo inadaiwa kuwa ya kisasa kabisa) kuna baadhi ya watu inawadhuru, wengine haiwaponyi kabisa, wengine inaweza kuwasababishia kifo!
Kwahiyo kwa kulinganisha tu, mjomba wako ni percentage ni 0.0000000000001 ya watu WALIOTIBIWA na babu na kupata complication hiyo!
Na huenda kuna masharrti alikiuka!
kWAHIYO bWANA sizinga, acha upotoshaji, acha watu wasafiri kwenda SAMUNGE, dawa ya babu inaponya, na hii ni kwa mujibu wa HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI!
Hata hivyo namtakia MJOMBA wetu AFYA NJEMA!

PakaJimmy..umetumia busara kunijibu...Amina!!sasa hivi nimeshaongea na muhasibu wa ubalozini New Delhi-India..Mr Yahya naona atanisaidia sana kwa hili. Namuombea afya njema Anko angu

Infact hii kitu sio upotoshaji bali nimemchukulia anko kama reference, kwamba dawa ya badu haijamtibu...kama wengine imewatibu basi Innshhallah wamepona!! Kama kukiuka masharti sidhani sema labda aichokosea ni kwamba kabla ya kwenda samunge angeenda medical kwanza, lakini sidhani kama baada ya kikombe kuna masharti tena.
 
Hata dawa ya malaria mseto(ambayo inadaiwa kuwa ya kisasa kabisa) kuna baadhi ya watu inawadhuru, wengine haiwaponyi kabisa, wengine inaweza kuwasababishia kifo!
Kwahiyo kwa kulinganisha tu, mjomba wako ni percentage ni 0.0000000000001 ya watu WALIOTIBIWA na babu na kupata complication hiyo!
Na huenda kuna masharrti alikiuka!
kWAHIYO bWANA sizinga, acha upotoshaji, acha watu wasafiri kwenda SAMUNGE, dawa ya babu inaponya, na hii ni kwa mujibu wa HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI!
Hata hivyo namtakia MJOMBA wetu AFYA NJEMA!

hospitali ya muhimbili?
Mbona sijasikia hii.kweli kipenda roho...
 
PakaJimmy..umetumia busara kunijibu...Amina!!sasa hivi nimeshaongea na muhasibu wa ubalozini India..Mr Yahya naona atanisaidia sana kwa hili. Namuombea afya njema Anko angu

Infact hii kitu sio upotoshaji bali nimemchukulia anko kama reference, kwamba dawa ya badu haijamtibu...kama wengine imewatibu basi Innshhallah wamepona!!
Aksante sana broda kwa kujifunza!
Pia pole kwa mihangaiko ya kumpeleka Anko India...Wengine imani zinatufunza kuwa "Maisha ya binadamu ni mafupi na yamejaa taabu!"
Hivyo usitaabike sana moyoni na hili, ndiyo maisha kaka!
Niwakilishie pole zangu kwa mgonjwa!
 
Zimefika...tuko pamoja!!
 
Which is which...!

Watapatikana wengi na kupukutika wengi sana mwaka huu.
M,kuu wangu X-Paster,
Naweza kukuunganisha toka Zanzibar hadi Samunge na Ukarudi Zenji same day!
Ni matter ya mafao mfukoni mwako tu!...ha ha haaaa!
Hayo mambo ya kusubiri utasubiri sana hadi dahari, usione kitu!
 
Yaani Miss alivyomshupalia Babu we acha tu. Kanisa lile waumini wake wangetoa sadaka ya mia 500 kila wakienda kusali saa hii wasingepiga kelele.
Poleni kwa hilo lakini hakuna wa kumzuia tena ndo imetoka hivyo.
Yule DJ wa pale temeke mbona alipofungua kanisa na kuwaambia dhahabu ni za kishetani hamkumhoji. Mbona hamhoji mapato yake!
Unajua mke wa mganga wa kienyeji kazoea kula kuku wa kijani! wa bluu nk sasa hakuna wenyekupeleka kuku shida kweli kweli!

Rafiki naomba kusikia ushuhuda wako maana kumbukumbu yangu inaniambia wewe ni mmoja walioenda kwa babu kupata kikombe cha uzima. Vipi mambo yako yako safi ama? Tunaomba ushuhuda jamani maana hata mamajusi walipoiona ile nyota yake waliifuata ikatua nyumbani aliko Yesu nao walishuhudia kuwa nikweli mtoto amezaliwa na wamemwona kwa macho yao. Kwa ushuhuda wako wengi watapona! Ukisema kweli na kweli tupu Mungu aonaye sirini atakujazi.
 
hesaabu zenyewe ziko hivi:

hadi leo amehudumia watu 3,000,000/- x 500 = 1,500,000,000/-!!

Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo

na Mwandishi wetu

ZAIDI ya wagonjwa milioni 3 wamepata kikombe kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila Babu katika kijiji cha Samunge Loliondo wilayani Ngorongoro tangu aanze kutoa huduma hiyo Agosti mwaka jana.
Takwimu zilizotolewa jana na mmoja wa wasaidizi wa Babu, Jackson Dudui, zinaonyesha bado wanategemea idadi kubwa ya wagonjwa kuendelea kumiminika kijijini hapo kufuata kikombe hicho kinachotibu magonjwa sugu na kwamba juzi pekee wagonjwa 17,065 walipata huduma hiyo.
Magonjwa sugu yanayodaiwa kutibiwa na kikombe hicho kinachokwenda na imani zaidi ni kisukari, shinikizo la damu, pumu, saratani na ukimwi.
Alisema jana magari zaidi ya 400 yenye wagonjwa zaidi ya 3000 yalikuwa yakimsubiri Mchungaji Mwasapila atoke kanisani, ili awapatie tiba hiyo mbadala ambapo alieleza raia kutoka Kenya wamekuwa wakimiminika kwa wingi kijijini hapo.
Foleni ya magari si kubwa sana kwa siku ya leo kwani hivi tunavyozungumza yapo magari zaidi ya 400 yakimsubiri Babu atoke kanisani na kuanza kuwahudumia kuanzia saa 8 mchana na hakika atawamaliza leo hii, alisema.
Msaidizi huyo alisema kuwa katikati ya wiki iliyopita walipata ugeni wa wachungaji zaidi ya 10 kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati waliokuwa kijijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano wao mkuu wa mwaka wakiongozwa na Mkuu wa Jimbo aliyetajwa kwa jina moja la Nangole.
Alisema mbali na wachungaji hao kushiriki mkutano huo waliungana na Babu kutoa vikombe kwa wagonjwa waliokuwepo kijijini hapo kupata tiba hiyo.
Habari zaidi zilizopatikana zimeeleza kuwa Babu amepiga marufuku wagonjwa kutoka Kenya wanaosafirishwa kutumia magari yasiyoruhusiwa kama malori na gari ndogo saloon wakiwa wamejazana hali aliyosema ni mateso kwa wagonjwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alieleza kuwa utoaji tiba unaendelea vizuri kijiji hapo, na alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa ukusanyaji ushuru wa magari na helikopta alisema hayo ni mambo ya kisiasa zaidi na kumtaka mwandishi wa habari hizi kusubiri maamuzi ya kikao halali kitakachofanyika leo kijijini hapo.
Alisema bado maamuzi hayajafikiwa kujua ni mamlaka ipi itakayokuwa ikikusanya ushuru huo kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngoromngoro na serikali ya kijiji cha Samunge.
Siwezi kuingia kwa undani zaidi kuzungumzia suala hilo naomba usiandike chochote kwani kesho kutakuwa na kikao kitakachozungumzia suala hilo na tutawapeni taarifa, alisema.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mgogoro wa kugombea ushuru wa magari na helikopta kati ya pande hizo na wakati fulani iliripotiwa kuwa serikali ya kijiji iliwafukuza watoza ushuru toka halmashauri.

source: Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo

Kuna kunukuliwa vibaya. Vikombe ni 300,000 kwa hiyo ni sh 150 milioni. Ukisoma story ya Majira kuna tofauti. Ukilinganisha na fedha zilizopatikana mwezi mmoja uliopita (mil 50 kwa miezi 6) hakuna uhalisia kufikia 1.5 bilioni.sasa
 
Miss Judith yuko manual zaidi kuliko kufikiria uhalisia wa data ANAZOOKOTEZA.
Anasoma na kusikia kwenye redio zinazoishia MAGOMENI, na kukimbilia kubandika conclusive informatio!

How pity!...sijui ni kukanganyikiwa!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Back
Top Bottom