Anajuuliza jinsi ya kutumia u Dr (heshima-UDOM) kukanusha tangazo la Sheikh Yahya kuhusu kumwongezea ulinzi usioonekana ili wananchi wasimuone mpunga mapepo na kujitenga naye (Kuogopa mapepo yasije yakawadakia )WanaJF,
Hivi karibuni nilijumuika kwenye ziara ya Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) ya kutembelea eneo la Gongolamboto lililoathiriwa na mabomu. Juzi nilijumuika pia kwenye hafla ya kumpokea uwanja wa ndege Rais aliyechaguliwa na NEC, Dr. Kikwete (heshima-UDOM) wakati akiwasili kutoka katika ziara yake aliyokwenda kusuluhisha mgogoro wa nchi nyingine ya kiafrika.
Kwa wanaomfahamu Kikwete wa zamani (enzi zile akiwa hana udaktari wa heshima) hawatachelewa kubaini mabadiliko makubwa kwenye sura yake. Ukweli sasa amechoka, amechoka, jamani nasema amechoka, siyo utani amechoka, yupo hoi. Hata wananchi wanaompokea au kusalimiana nae kwenye hafla mbalimbali unaweza ukawasoma kwa kutumia 'body language' namna walivyokata tamaa na kukosa matumaini. Mimi naamini kabisa kwa jinsi hali ilivyo, hata Kikwete mwenyewe atakuwa amebaini mabadiliko hayo na lazima anatamani miaka mitano itimie haraka akapumzike. Wakati yeye anateseka hivyo, mafisadi anaowafuga mwenyewe wanakula maisha ya peponi!