Sasa imekuwa kero, bongo flava

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Sasa inakera sana tena sana. Wasanii 90% wa bongo flaza wanajidai hawajui lafdhi ya kiswahili vizuri na wakiimba wanaweka lafdhi sijui ndio ya kizungu au ya ki kayumba.

Mshazisikia hizo nyimbo za hawa jamaa? hivi BASATA hawayaoni haya na kuyakemea au ndio wamelala doro. Inakera.
 
Kweli inakera! yani wanaona wasipo weka kiswahili cha kijinga, mara mUpenzi, mara kiswanglish wataonekana too local ama?
 
Kwanza karibia wote wanaojiita wanaimba r&b wanatumia staili moja ya kubana pua, sasa sijui wanaimba nini r&b, zouk au kitu gani. Kiswahili wanachokitumia ni kibovu sana ndio maana nyimbo zao zinaitwa bigijii
 
Siku zote watu wanalalamika kuwa huu si muziki wetu bali ni wa kujiokotea toka mataifa mengine kisha tunaubatiza na kuuita wetu. Wenyewe angalieni ni msanii gani wa fleva ni mwanamuziki wa kiukweli? Jibu hapana, we utaona lijibaba linaimba nyimbo za kibigii huku anaminya pumbu na kubana pua ili mradi tu afananishwe na mmarekani mweusi.
 
Mara utasikia fulani ni mfalme wa zouk oh fulani ni mfalme wa kwaito...please, toka lini hii ikawa miziki ya kwetu? Hapa wa kuwalaumu ni media za bongo ambao wanabeba marafiki zao kwa kulipwa bia ama uroda huko uswahilini. Tunataka muziki wa kwetu Sikinde, Msondo, Sagha Rhumba, TOT, African Stars, Extra Bongo na nyinginezo, alaaaa!
 
Hiyo ni style au moja ya ubunifu katika nyimbo zao... Its like slang kwa wenzetu wa nje... Kama kila mwanamuziki ibidi aimbe kama mpoto sidhani kama itapendeza... Thats why si mbaya kila mmoja akaimba na kuburudisha kwa uwezo wake wa utungaji. Labda tu pale wanapotumia lugha chafu na matusi ndio inapokua mbaya... Otherwise mi naona si vibaya....
 
fresh jumbe yuko tokyo japani. anasema muziki unaompa jina huko ni huu wa kwetu wa asilia ambao unapigwa na msondo ,sikinde nk. unapopiga muziki wa wenzako huonakani kama wewe bali ni kivuli tu, chukulia mfano wale tatu nane, jamaa walivuma saana, na walikuwa na mialiko karibu nchi nyingi tu, kwa kuwa WALIJITAMBUA hawa bado . itawachukua miaka kufikia waliko fika akina mbaraka mwinshehe na wengineo. bila kuumiza vichwa na kupiga muziki kwa kutumia ala wataishia ndani ya nchi hii hii , nawashauli wabadilike na wawe na malengo, waumize vichwa sio watemee muziki wa computer. kweli utapata hela lkn ukishuka ndo kimojaaaaaaaa.
 
Sio tu wasanii wa bongo flava,hata watangazaji wa vpindi vya redio wanaigana sana sauti mpaka inaboa yaani haswahaswa hawa wa vipindi vya mchana.
 
Kuna msanii mmoja wa Bongo Fleva nilimsikia akizungumza kwa kujivuna sana kwamba watu wengi walifikiri yeye ni mnigeria kwa jinsi alivyoimba na staili yote ya mziki wake imekaa kinigerianigeria. Mtanzania anaona raha kuitwa Mnigeria!
 
Ndiyo ujinga wa hawa wasanii feki, yaani mtu anaona raha kufananishwa na watu wa nje. Imbeni muziki wetu wa nyumbani ya nini kuiga? Kumbukeni original ni original tu, nyie mnategemea muziki Wa computer matokeo yake mkififia mnasahaulika moja kwa moja.
 
Ndugu wana JF, tusiishie tu kuwalaumu wanamuziki wetu kwa kuiga kila kitu ati kutoka kwa wenzetu. Mi narejea na naunga mkono mawazo ya Aristotle wa UGIRIKI aliyesema kwamba kazi zoooote za sanaa ni uigaji wa UBUNIFU. Uigaji huo ndio unayoifanya kazi ya sanaa ata iyo ya Bongofleva KUTUKUKA. Kila unachofanya hapa duniani ni mwigo wa ARISTOTLE. Nawasilisha. Endeleeni kuuponda huo mziki wenye mwigo toka ulaya wenzenu wana'make' money!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom