Sarufi ya Kiswahilii

Nitaanza kwa kusema kwamba nisikufiche. Nina itikadi ya kitaaluma. Naamini nadharia za sarufi za kimapokeo hazikuenda mbali kutosha katika kuchunguza na kuchambua muundo wa lugha. Kwa maneno mengine swali la msingi halikuulizwa vya kutosha. Swali hilo ni: Kwa sababu gani lugha ina muundo ilio nao? Jibu la swali hili ni nadharia tete kadha. Na pengine kwa sababu hiyo, wanamapokeo hawakupenda kudhani kwingi. Lakini sayansi lazima iendeshwe na dhana, nadharia tete, majaribio kuona kama nadharia tete hizo ni sahihi, nk.
Nadharia mpya zimejengwa kwenye nadharia tete kwamba: lugha imeundwa hivyo kwa sababu ndivyo ubongo wetu uliundwa; lugha imeundwa hivyo ili kuwa rahisi kwa watoto kujifunza. Mambo haya yanapelekea kwenye utafiti wa kujua ni muundo gani huo ambao unaonekana ni rahisi kwa watoto kujifunza na pia unaakisi namna ambayo bongo zetu zimetengenezwa na zinavyofanya kazi.
 
ASANTE SANA MKUU...MCHANGO WAKO NIMEJIFUNA KITU...UBARIKIWE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom