Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH) Featured

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Cap.PNG
Tezi Dume (Prostate gland)

KUVIMBA KWA TEZI DUME (BENIGN PROSTATE HYPERPLASIA BPH) FEATURE

Tezi Dume (Prostate gland)

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.

Kuvimba Tezi Dume (BPH)

Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.

Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.

Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu.

Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.

BPH husababishwa na nini?

Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.

Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.

Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika

damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye

kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli: Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.

Dalili za BPH
Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote

Hukojoa mkojo unaokatika katika
Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
Husita kabla ya kuanza kukojoa
Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH

Madhara ya BPH
BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
Madhara katika figo au kibofu
Shinikizo la damu
Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
Maambukizi mbalimbali
Nimonia (Pneumonia)
Damu kuganda
Uhanithi
Vipimo na Uchunguzi

Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na

Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume.

Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.

Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.

Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.

Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.
Matibabu

Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

Matibabu kwa njia ya dawa
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na

Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.

Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.

Matibabu kwa njia ya Upasuaji
Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)
Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo niTiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume. Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa

Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo
Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwaKula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.[Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.

Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji

Shida wakati wa kukojoa: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.

Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. Hta

hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji.

Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.

Mdiso au kudindisha (Erections): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupa mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.Kutoa mbegu (Ejaculation):

Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra

karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia

kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

na Saratani ya Tezi Dume: Hakuna Uhusiano wa moja kwa mojaIngawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kila mwaka.

MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WAADAU WA JF
AINA ZA TEZI DUME NA MATIBABU YAKE
(PROSTATE DISORDERS) TEZI DUME NI NINI?
Tezi dume ni moja ya tezi la uzazi la kiume ambalo kila mwanaume anayo, tezi hili lipo chini ya kibofu cha mkojo na linazunguka njia ya mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume. Kazi ya tenzi dume ni kutoa majimaji anayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) kutengeneza manii (semen).

Jinsi umri unavyoongezeka tezi dume nalo huongezeka ukubwa ambao unaweza kuwa wa kawaida na kusababisha kufinya njia ya mkojo au saratani.

Kuna aina tatu za magonjwa ya tezi dume.
  • Maambukizi ya Bakteria (Prostatitis).
  • Kukua kwa tezi dume ambalo sio saratani (Benign Prostatic Hypertrophy-BPH).
  • Saratani ya tezi dume.
Chanzo cha tatizo la tenzi dume ;maambukizi ya bacteria (Prostatitis) mbalimbali ambao wanaweza kuwa ni visababishi vya magonjwa mbalimbali ya zinaa mfano, kaswende, kisonono, pangusa n.k au bacteria wanao shambulia mfumo wa mkojo (UTI) wanaweza kupenya na kuifikia tezi dume na kuishambulia, vyanzo vingine ni kushuka kwa kinga za mwili na ajali zinazopelekea kuumia katika eneo ambalo tezi dume ipo na pia kunamazingira hatarishi yanayo pelekea mwanaume kuathirika na hili tatizo; Kama mwanaume alishawahi kuwa na hili tatizo na hakupata matibabu sahihi.

Pia kuwa na maambukizi katika kibofu cha mkojo au mrija unao tiririsha mkojo (urethra), Kutokunywa maji ya kutosha, Kuwa na wapenzi wengi na kushiriki tendo la ndoa na mpenzi mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa na HIV/AIDS.

DALILI ZA HILI TATIZO

  • Maumivu wakati wa kutoa haja ndogo au kuhisi kama mkojo ni wa moto na maumivu wakati wa kufika kileleni
  • Kwenda haja ndogo mara kwa mara
  • Mtiririko wa mkojo kuwa dhaifu
  • Maumivu chini ya kitovu Na kiuno na chini ya mgongo
  • Maumivu ya sehemu ambayo ipo katikati ya korodani na sehemu ya kutolea choo kubwa, Maumivu ya korodani na uume
  • Mwanaume mwenye tatizo hili anaweza akawa na homa
Iwapo saratani ya tenzi dume imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu za jirani ya mwili, mgonjwa anaweza kuwa na

  • Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni
  • Uume kushindwa kusimama (uhanithi)
  • Aidha, mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k
TIBA

Matibabu ni ghali na mara nyingi wagonjwa hushauriwa kufanyiwa upasuaji ambao huwa ni gharama. Matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

Upasuaji
Upasuaji hufanyika kwa wagonjwa walio katika hatua za awali za ugonjwa (stage I na stage II) ingawa pia hufanywa kwa baadhi ya wagonjwa walio katika hatua za mwisho za ugonjwa huu yaani stage III na stage IV. Upasuaji unaofanywa ni ule wa kuondoa tezi dume pamoja na baadhi ya tishu zinazozunguka tezi hiyo.

Tiba ya Mionzi
Hii ni aina ya tiba inayotumia mionzi kuua seli zenye saratani. Tiba ya mionzi hutumika kutibu saratani ya tezi dume ambayo haijasambaa kwenye sehemu nyingine za mwili. Aidha inaweza pia kutumika kuua masalia ya tishu zenye saratani mara baada ya kufanyika kwa upasuaji.

Madhara anayoweza kupata mgonjwa kutokana na aina hii ya tiba ni pamoja na kushindwa kusimamisha uume au uhanithi, kukosa hamu ya kula, uchovu, ngozi kubabuka, kuharisha na kutoa mkojo uliochanganyika na damu.

Tiba ya Homoni
Hii ni aina ya tiba inayotumia dawa zinazopunguza kiwango au ufanyakazi wa homoni ya testosterone mwilini. Testosterone ni homoni ya kiume inayochochea ukuaji wa tezi dume, hivyo basi matumizi ya dawa hizi husaidia kupunguza ukuaji huu na kusambaa kwa seli za saratani. Tiba ya homoni hutolewa kwa wanaume walio katika hatua za mwisho za ugonjwa huu kwa nia ya kupunguza maumivu na kutibu dalili za ugonjwa. Dawa zinazotumika kwa tiba ya aina hii zimegawanyika katika makundi mawili, zile zinazochagiza uzalishaji wa homoni ya luteinizing (luteinizing hormone-releasing hormones, LH-RH) kwa mfano goserelin, nafarelin na leprolide; na zile zinazozuia ufanyaji kazi wa homoni ya androgen kwa mfano flutamide, bicalutamide na nilutamide.

Lakini, ipo njia nyingine ya kukabiliana na tatizo hili ambayo ni TIBA YA SELI SHINA AU CRYSTAL SELI. Crystal cell (stem cells) ni kirutubisho tiba chenye uwezo wa kuhisha seli zilizoharibiwa kwenye tenzi na kuzirekebisha na kusaidia kuchochea uzwalishaji wa seli mpya nzuri zenya afya na hivyo huboresha afya hatimaye kuokoa maisha ya wanaume wengi.
  • Crystal cell husimamisha usambaaji wa saratani kwenye sehemu nyingine za mwili. Aidha husaidia kuhuisha na kuchochea uzalishwaji wa seli zilizokufa wakati wa mionzi au upasuaji.
  • Crystal cell inasaidia thibiti, kuboresha na kubalance uzawalishwaji wa homoni ya testosterone katika ume inayochochea ukuaji wa tezi dume bila mpangilio kutoka na uhitaji wa mwili na hivyo hupelekea kupunguza ukuaji na kusambaa kwa seli za saratani

MADHARA ENDAPO MATIBABU YATACHELEWA
Madhara yanayoweza kusababishwa na utumiaji wa dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, upungufu wa damu, kuongezeka uzito, uhanithi na kukosa hamu ya tendo la ngono, matatizo katika ini na matiti kuwa makubwa.

  • Kusambaa kwa bacteria mbalimbali katika damu(bacteremia)
  • Kuwa na jipu kwenye tezi dume(prostatic abscess)
  • Ugumba kutokana na kuathirika kwa manii,mbegu za kiume
  • Pia tatizo hili linaweza likasababisha kansa ya tezi dume(prostate cancer )
kwa ajili ya maswali,ushauri,na maelezo kuhusiana na crystal cell na hili tatizo na matatizo mengine
---
Prostate Treatment Methods
In addition to medical treatment for enlarged prostate in a natural way can be used.
Materials needed:

  • Parsley
  • Chickpeas,
  • Barley flour
  • Chamomile,
  • Couch grass,
  • Honey
PREPARATION AND APPLICATION FORMS:
  • Dried parsley, chickpeas boiled water, then filtered dem. Filtered from the mixture, sweetening and drink three cups a day during treatment.
  • Barley flour, kneaded with Melhem until consistency of honey. Chickpea paste is prepared by grit size pills.Prepared these pills, Inc. when daisy-flavored three-day, five ingested the receiver.
  • Dried split root, crushed, pounded. The prepared powder is boiled in water for five minutes. Filtered from the liquid, syrup until consistency of honey was added and mixed. Prepared in this syrup, a cup of after dinner drink.
---
SARATANI YA TEZI DUME(PROSTATE CANCER)

1.0 UTANGULIZI:
Sisi katika picha ni waathirika, wahanga, manusura wa saratani ya tezi dume (prostate cancer).Tunawasalimu! Kwa waraka huu tunapenda kuwahabarisha juu ya gonjwa saratani. Gonjwa hili kwa sasa ni gonjwa tishio kwa maisha ya watu wengi duniani. Katika nchi zinazoendelea na hususani Afrika chini ya jangwa la Sahara Tanzania ikiwa miongoni hali ni mbaya sana. Mwaka 2010 takwimu duniani zinaonyesha kuwa malaria iliua watu laki 5, kifua kikuu 2.1 milioni, ukimwi 1.8 milioni na saratani 9.9 milioni. Asilimia 75 ya hao 9.9 milioni ambao ni 7.4 milioni walifariki toka nchi zinazoendelea.

Inatarajiwa mwaka 2020 malaria itaua watu laki 2.5, kifua kikuu 2.2 milioni, ukimwi 1.5 milioni na saratani 12.2 milioni. Asilimia 75 ya hao 12.2 milioni ambao ni 9.15 milioni watafariki toka nchi zinazoendelea.Waraka huu unawahabarisha umuhimu wa kuliangalia gonjwa la saratani na hasa saratani ya tezi dume ambao sisi ni wahanga. Tunawaomba WaTanzania muliangalie na kuliwekea uzito, mjielimishe juu ya gonjwa hili - saratani.

Pamoja na kwamba saratani inauwa watu wengi duniani kuliko magonjwa ya kuambukiza kama malaria, kifua kikuu na ukimwi, lakini tunaona elimu ya saratani haijapewa uzito unaostahiki. Katika hotuba ya kuahirisha bunge la Jamhuri ya Muungano, Mkutano wa Tatu, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo K. P. Pinda (Mb) aliongelea kwa msisitizo juu ya saratani na hasa saratani ya tezi dume (prostate cancer) na magonjwa mengine sugu.

Wa-Tanzania tuendeleze mkazo huu kwenye jamii tunazoishi. Wa-Tanzania tujielimishe juu ya hali hatarishi, dalili za saratani na umuhimu wa kujichunguza angalau mara moja kwa mwaka. Sisi tumelipata joto la jiwe la saratani ya tezi dume. Tunajua madhara ya saratani. Tusingependa watu wengine wapate mateso kama tunayoyapata kwa kuchelewa kugundulika gonjwa mapema. Hii ni sababu tosha iliyotusukuma kuanzisha Tanzania 50 Plus Campaign inayotoa elimu, utetezi na msaada wa saratani ya tezi dume kwa jamii nzima. Wachina wana methali isemayo, Ukitaka kujua unakoelekea, muulize anayerudi. Sisi tumerudi na tunakuhabarisha.

2.0 JEE SARATANI NI GONJWA GANI? Neno saratani ni jina la gonjwa ambao hutokea wakati chembe chembe za uhai katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu na mfumo wa mwili - zinaasi na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida chembe chembe za uhai mwilini huwa zinajigawa, zinapevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini chembe chembe za uhai za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe zinaishi muda mrefu kuliko chembe chembe za uhai za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza chembe chembe za uhai asi zingine na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo - saratani.

3.0 SARATANI YA TEZI DUME NI GONJWA GANI? Tezi dume linapatikana katika mwili wa kiumbe mamalia dume tu (angalia mchoro normal prostate). Chembe chembe za uhai katika tezi dume zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili - zinaasi na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo, hapo mtu anakuwa ameathirika na saratani ya tezi dume. Zipo aina nyingi za saratani. Zipo zinazowapata watoto tu, vijana, wanawake na wanaume. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Tokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiacha saratani ya mapafu kwa vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.

Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS:2010) na cha Afrika Kusini (CANSA) vimebaini kuwa,mwanaume mmoja kati ya sita atapata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Na kama wanaume mia moja watakutwa na saratani ya tezi dume. Saratani hii haina mipaka ya kitabaka asema Askofu Mkuu Desmond Tutu. Askofu Mkuu Tutu, sisi binafsi na Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela ni baadhi ya waathirika wa gonjwa hili ambao bila ya kujinyanyapaa na wala hofu ya kunyanyapaliwa, tumevunja ukimya na kuwa wawazi katika jamii. Pamoja na yote hayo, ifahamike bayana, saratani ya tezi dume ikigundulika mapema inatibika kwa urahisi zaidi.

4.0 HALI HATARISHI:
Kuna hali hatarishi nyingi zinazochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Zifuatazo ni baadhi tu:-

Umri: Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume inaongezeka sana hasa ukifikia umri wa takribani miaka 50 na kuendelea; Nasaba: Kama katika ukoo kuna historia ya ugonjwa wa saratani ya tezi dume suala na nasaba linachangia kumweka mwanamume kuwa hatarini kuathirika na saratani ya tezi dume kwa misingi ya nasaba (genetic); Lishe: wanaume wanaopenda kula nyama (red meat) yenye mafuta mengi na aina ya maziwa yenye mafuta mengi (high-fat diet) wako katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume; Mazoezi: Wanaume wasiopenda kufanya mazoezi; Unene (obesity). Upungufu: Virutubisho E.

5.0 DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME:
Swali linakuja: Jee mwanamume ataziona dalili zipi zinazoashiria saratani ya tezi dume? Zipo dalili nyingi na hapa nazitaja baadhi tu:

Udhaifu katika kujisaidia haja ndogo na unapotoka unakatizakatiza; Kushindwa kukojoa na kushindwa kuanza pata haja ndogo; Unapohisi haja ndogo unapata shida kuzuia haja ndogo isijitokee yenyewe; Hisia ya kutaka kupata haja ndogo kila wakati hasa nyakati za usiku; hata kukojoa kitandani; Mkojo kujitokea wenyewe; Maumivu au kuhisi mwasho wakati wa haja ndogo; Mbabaa kusimama kwa shida; Maumivu wakati unapotoa manii wakati wa kujamiana; Damu damu katika mkojo na katika manii; Maumivu viungoni kiunoni, miguu, mgongo nk. Kukosa hamu ya kula na kupungua uzito / kukonda.

Pamoja na kuorodhesha dalili hizo napenda msomaji ujue kwamba mwanaume anapoanza kuziona na kuzihisi kati ya dalili hizo, basi ajue chembe chembe za uhai asi katika tezi dume lake zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.

6.0 MWITO KUFANYIWA UCHUNGUZI WA TEZI DUME:
Kwa kuzipitia dalili hizi, imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi huwa na soni kwenda kumwona daktari kwa uchunguzi. Wengi huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina kuna mkono wa mtu, nimelogwa. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuliita gonjwa la mabasha na wengine kuurahisisha kama ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni haki yake kuugua mwanaume mwenye umri wa utu uzima.

Mambo kama hayo huleteleza wanaume kujinyanyapaa na kujikuta wengine wakijitibia chochoroni au kwa waganga wababaishaji mpaka pale wanapokuwa hoi bin taabani, mambo yamekuwa mabaya ndipo wanapopelekwa hospitalini. Hapa tunatoa wito kwa wanaume kuweka kipaumbele kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla na ujumuishe uchunguzi wa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.

Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kukupima mara moja ofisini kwake: Vipimo hivyo ni Digital Rectal Exam (DRE) na cha pili ni Prostate Specific Antigen (PSA). Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine vya uhakiki kama transrectal ultrasound au na prostatic needle biopsy. Kuwahi kugundua saratani mapema, kabla ya dalili, ni faida kubwa kwa mwaathirika. Maana saratani ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.

7.0 SARATANI NA MATIBABU:
Pamoja na yote hayo, katika zama hizi, matibabu ya saratani ya tezi dume yanapatikana. Ukigunduliwa una saratani hiyo unashauriwa ushauriane na daktari wako kuamua aina ya tiba itakayokufaa. Kuna tiba za uangalizi (active surveillance), upasuaji (surgery), mionzi (radiotherapy) vichocheo (hormone therapy) na kemikali (chemotherapy).

8.0 TUOMBWA KUUNGWA MKONO:
Katika mpango kazi wa kampeini hii tuna mahitaji mengi. Tumekusudia kuwafikia Watanzania wengi zaidi mwaka huu. Tunapenda kutumia nafasi hii kukuomba mchango wako na toka marafiki zako kwa ajili ya kampeini hii. Mwaka huu kati ya miradi tuliojipangia ni pamoja na kuchapicha vipeperushi vya Kiswahili vya saratani ya tezi dume milioni moja na kuvitawanya nchi nzima! Kipeperushi kimoja kinagharimu takribani Tshs. 250 hadi 300 kufuatana na wingi wa nakala. Vipeperushi vimekuwa vya msaada sana katika kutoa elimu ya gonjwa saratani. Kwa kuanzia mchango katika eneo hili utashukuriwa sana.

8.0 HITIMISHO: BAADA YA MAELEZO HAYO TUNAPENDA KUTOA WITO:
8.1 Kwa wanaume wote wenye umri takribani miaka 50 na kuendelea, tafadhali mwone daktari wako kwa uchunguzi wa afya ukijumuisha uchunguzi wa tezi dume;

8.2 Elimu hii itolewe pia kwa akina mama wote katika jamii mnayoishi. Wakinamama wakipata uelewa wa saratani ya tezi dume, wanaweza kuwaelimisha na kuwasaidia waume zao, baba, kaka, wajomba nk. Pia nao wahimizwe kujua juu ya saratani za wanawake kama za matiti na shingo ya uzazi nk.

8.3 Tunawaomba madaktari wote, mnapopata wagonjwa wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea washaurini pamoja na matibabu mengine, wafanyiwe uchunguzi wa tezi dume.

UKWELI KUHUSU SARATANI:
Saratani zote na hususani saratani ya tezi dume ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.

Kwa mawasiliano zaidi:
Mratibu, Tanzania 50 Plus Campaign, P. O. Box 1854 Dar es Salaam
au barua pepe : tanzania50plus@yahoo.com, info@tanzania50plus.org Simu: +255 754 402033.

KUCHANGIA KAMPEINI :
Weka katika tawi lolote la CRDB. Jina la akaunti : Centre for Human Rights Promotion CHRP;
Namba ya akaunti: 01 J 1027311100 au kupitia M-Pesa: 0754 402033

TUPIGE VITA SARATANI! TUPIGE VITA SARATANI YA TEZI DUME! PAMOJA TUNAWEZA!

Kimetayarishwa na kutawanywa na:

Tanzania 50 Plus Campaign
 
Kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa wazee hasa kuanzia miaka 55 na kuendelea wengi tumeona wakifariki kila wakati hivyop kunifanya nifikiri je kuna tiba sahii ya ugonjwa huu?

Naomba unijulishwe maana nina mgonjwa amepimwa kwa kutumia PSA na kukugundulika ana ugonjwa wa Tezi dume naomba kujua ni wapi anaweza kupata tiba sahii hapa nchini?
 
Prostate Treatment Methods
In addition to medical treatment for enlarged prostate in a natural way can be used.
Materials needed:

  • Parsley
  • Chickpeas,
  • Barley flour
  • Chamomile,
  • Couch grass,
  • Honey
PREPARATION AND APPLICATION FORMS:
  • Dried parsley, chickpeas boiled water, then filtered dem. Filtered from the mixture, sweetening and drink three cups a day during treatment.
  • Barley flour, kneaded with Melhem until consistency of honey. Chickpea paste is prepared by grit size pills.Prepared these pills, Inc. when daisy-flavored three-day, five ingested the receiver.
  • Dried split root, crushed, pounded. The prepared powder is boiled in water for five minutes. Filtered from the liquid, syrup until consistency of honey was added and mixed. Prepared in this syrup, a cup of after dinner drink.
 
Aksante sana tatizo langu ni kiingereza umeniacha mlango wazi,Naomba kama kuna uwezekano nitafsilie kwa kiswahili tafadhali sana.
 
kuna bidhaa inayoitwa" crusiferous plus" ya kampuni ya gnld ukichukua tembe tisa kwa sikuh tatizo linakwisha kabisa> Dr. fatma wa kenyatta hospital alitoa ushuhuda kuhusu babake aliyemtibu kwa tembe hizo, ni matunda mengina greens kwa wingizilizomondani ya crusiferous plus.
 
Njia nzuri ni kuondoa Makende

Ikifanyika kwenye early stages, mgonjwa atapona kabisa na ataishi muda mrefu. Wataalam wanahusisha prostate cancer development na presence ya excessive estrogens kulinganisha na testerone, kitu ambacho hutokea umri ukienda mbali. Kwa hiyo dawa hapo ni kuondoa source ya estrogens ambayo ni makende. Note that Wakati wa ujana testerones inakuwa nyingi kuliko estrogen na ndio maana unakuwa na nguvu za aina zote.

Kwa kuzuia, Wanaume wanatakiwa kula nyanya pamoja na Broccoli plus other Cruciferous vegetables mara kwa mara. Na ngono zisiwe too much. Too much ngono poses a burden on prostate gland resulting into its enlargement (it needs to enlarge itself in order to cope with your excessive ngono) and this enlargement may end up into abnormal growth which is cancer.
 
Nakushauri mpeleke muhimbili amuone urologist siku ya clinic ni muhimu sana kansa sio ugonjwa wa kufanyia majaribio ya dawa, atafanyiwa uchunguz na kujua kama imesambaa au bado then watajua cha kufanya, ukiwahi ndo vzuri.
 
Sasa na umri wa miaka 50,toka nikiwa kijana nikikuwa na tatizo la kukojoa mara kwa mara yaani mpaka inaudhi wakati huo nilikuwa wala sijaanza ngono.Nilipoanza ngono nikawa natoa mbegu za kiume kidogo sana na ni mara moja tu na inanibidi nisubiri siku 4 hivi ndipo nipate tena vinginevyo nikifanya kila siku basi mbegu hazitoki kabisa.

Sasa nikimaliza tu ngono mkojo unakuwa umejee sana naenda kuutoa nikitoka chhoni nikifika sebuleni umejaa tena inabidi niende tena. Hali ikawa hihivi hadi nikafikisha miaka 28 nikaoa.

Nikaanza kwenda hospitali nikaambiwa nimevimba prostate sasa nikaogopa sana nikawa nadunduliza mbegu namuingilia mrs mpaka tukapata watoto 5 nikarudi tena hosp dokta akaniambia anifanie TURP yaani trans ureter resection of prostate baada ya hapo nikawa sasa ngono nafanya ila hakuna mbegu kabisa hali ambayo ni sperm retrogration, sasa tatizo langu ni kwamba ile hali ya kukojoa ndio imezidi sana yaani nakojoa zaidi ya mara w0 kwa dk 1 na nikisema niubane nasikia maumivu makali,je sasa huu ni ugonjwa gani tena?maana nimepima kisukari nil na je nifanyeje?
 
Kwa kuondoa Makende je Mzee wa kaya ataweza kusimama bila shida??????

Kwanza kabisa sikubaliani na dhana ya kuondoa Kende, kama upo ushahidi wa kitaalamu naomba unielimishe. Prostate hutibiwa kulingana na stage. Kama ni changa huwa inatibiwa kwa dawa, lakini kama ni kubwa hufanyika operesheni inayoitwa Prostectomy yaana kuondoa hiyo Prostate. Hii inaweza kuwa Open procedure, lakini sikuhizi hasa nchi zilizoendelea hufanyika kwa ku crush prostate kwa njia ya kitaalamu bila kupasua (Open). Kwahiyo ni vema aende kumuona Urologist pale Muhimbili, Bugando au KCMC.

Kuhusu bwana aliyeuliza kama ukiondolewa kende mambo inakuwaje. Mambo yanakuwa kama kawaida ila mapungufu yataonekana kwasababu viungo hufanya kazi kwa kushirikiana. Fahamu kuwa hapo ndipo utakuwa umehitimisha uzazi. Nadhani umenielewa.
 
SARATANI YA TEZI DUME(PROSTATE CANCER)

1.0 UTANGULIZI: Sisi katika picha ni waathirika, wahanga, manusura wa saratani ya tezi dume (prostate cancer).Tunawasalimu! Kwa waraka huu tunapenda kuwahabarisha juu ya gonjwa saratani. Gonjwa hili kwa sasa ni gonjwa tishio kwa maisha ya watu wengi duniani. Katika nchi zinazoendelea na hususani Afrika chini ya jangwa la Sahara Tanzania ikiwa miongoni hali ni mbaya sana. Mwaka 2010 takwimu duniani zinaonyesha kuwa malaria iliua watu laki 5, kifua kikuu 2.1 milioni, ukimwi 1.8 milioni na saratani 9.9 milioni. Asilimia 75 ya hao 9.9 milioni ambao ni 7.4 milioni walifariki toka nchi zinazoendelea.

Inatarajiwa mwaka 2020 malaria itaua watu laki 2.5, kifua kikuu 2.2 milioni, ukimwi 1.5 milioni na saratani 12.2 milioni. Asilimia 75 ya hao 12.2 milioni ambao ni 9.15 milioni watafariki toka nchi zinazoendelea.Waraka huu unawahabarisha umuhimu wa kuliangalia gonjwa la saratani na hasa saratani ya tezi dume ambao sisi ni wahanga. Tunawaomba WaTanzania muliangalie na kuliwekea uzito, mjielimishe juu ya gonjwa hili - saratani.

Pamoja na kwamba saratani inauwa watu wengi duniani kuliko magonjwa ya kuambukiza kama malaria, kifua kikuu na ukimwi, lakini tunaona elimu ya saratani haijapewa uzito unaostahiki. Katika hotuba ya kuahirisha bunge la Jamhuri ya Muungano, Mkutano wa Tatu, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo K. P. Pinda (Mb) aliongelea kwa msisitizo juu ya saratani na hasa saratani ya tezi dume (prostate cancer) na magonjwa mengine sugu.

Wa-Tanzania tuendeleze mkazo huu kwenye jamii tunazoishi. Wa-Tanzania tujielimishe juu ya hali hatarishi, dalili za saratani na umuhimu wa kujichunguza angalau mara moja kwa mwaka. Sisi tumelipata joto la jiwe la saratani ya tezi dume. Tunajua madhara ya saratani. Tusingependa watu wengine wapate mateso kama tunayoyapata kwa kuchelewa kugundulika gonjwa mapema. Hii ni sababu tosha iliyotusukuma kuanzisha Tanzania 50 Plus Campaign inayotoa elimu, utetezi na msaada wa saratani ya tezi dume kwa jamii nzima. Wachina wana methali isemayo, Ukitaka kujua unakoelekea, muulize anayerudi. Sisi tumerudi na tunakuhabarisha.

2.0 JEE SARATANI NI GONJWA GANI? Neno saratani ni jina la gonjwa ambao hutokea wakati chembe chembe za uhai katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu na mfumo wa mwili - zinaasi na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida chembe chembe za uhai mwilini huwa zinajigawa, zinapevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini chembe chembe za uhai za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe zinaishi muda mrefu kuliko chembe chembe za uhai za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza chembe chembe za uhai asi zingine na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo - saratani.

3.0 SARATANI YA TEZI DUME NI GONJWA GANI? Tezi dume linapatikana katika mwili wa kiumbe mamalia dume tu (angalia mchoro normal prostate). Chembe chembe za uhai katika tezi dume zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili - zinaasi na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo, hapo mtu anakuwa ameathirika na saratani ya tezi dume. Zipo aina nyingi za saratani. Zipo zinazowapata watoto tu, vijana, wanawake na wanaume. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Tokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiacha saratani ya mapafu kwa vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.

Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS:2010) na cha Afrika Kusini (CANSA) vimebaini kuwa,mwanaume mmoja kati ya sita atapata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Na kama wanaume mia moja watakutwa na saratani ya tezi dume. Saratani hii haina mipaka ya kitabaka asema Askofu Mkuu Desmond Tutu. Askofu Mkuu Tutu, sisi binafsi na Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela ni baadhi ya waathirika wa gonjwa hili ambao bila ya kujinyanyapaa na wala hofu ya kunyanyapaliwa, tumevunja ukimya na kuwa wawazi katika jamii. Pamoja na yote hayo, ifahamike bayana, saratani ya tezi dume ikigundulika mapema inatibika kwa urahisi zaidi.

4.0 HALI HATARISHI:
Kuna hali hatarishi nyingi zinazochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Zifuatazo ni baadhi tu:-

Umri: Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume inaongezeka sana hasa ukifikia umri wa takribani miaka 50 na kuendelea; Nasaba: Kama katika ukoo kuna historia ya ugonjwa wa saratani ya tezi dume suala na nasaba linachangia kumweka mwanamume kuwa hatarini kuathirika na saratani ya tezi dume kwa misingi ya nasaba (genetic); Lishe: wanaume wanaopenda kula nyama (red meat) yenye mafuta mengi na aina ya maziwa yenye mafuta mengi (high-fat diet) wako katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume; Mazoezi: Wanaume wasiopenda kufanya mazoezi; Unene (obesity). Upungufu: Virutubisho E.

5.0 DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME:
Swali linakuja: Jee mwanamume ataziona dalili zipi zinazoashiria saratani ya tezi dume? Zipo dalili nyingi na hapa nazitaja baadhi tu:

Udhaifu katika kujisaidia haja ndogo na unapotoka unakatizakatiza; Kushindwa kukojoa na kushindwa kuanza pata haja ndogo; Unapohisi haja ndogo unapata shida kuzuia haja ndogo isijitokee yenyewe; Hisia ya kutaka kupata haja ndogo kila wakati hasa nyakati za usiku; hata kukojoa kitandani; Mkojo kujitokea wenyewe; Maumivu au kuhisi mwasho wakati wa haja ndogo; Mbabaa kusimama kwa shida; Maumivu wakati unapotoa manii wakati wa kujamiana; Damu damu katika mkojo na katika manii; Maumivu viungoni kiunoni, miguu, mgongo nk. Kukosa hamu ya kula na kupungua uzito / kukonda.

Pamoja na kuorodhesha dalili hizo napenda msomaji ujue kwamba mwanaume anapoanza kuziona na kuzihisi kati ya dalili hizo, basi ajue chembe chembe za uhai asi katika tezi dume lake zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.

6.0 MWITO KUFANYIWA UCHUNGUZI WA TEZI DUME:
Kwa kuzipitia dalili hizi, imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi huwa na soni kwenda kumwona daktari kwa uchunguzi. Wengi huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina kuna mkono wa mtu, nimelogwa. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuliita gonjwa la mabasha na wengine kuurahisisha kama ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni haki yake kuugua mwanaume mwenye umri wa utu uzima.

Mambo kama hayo huleteleza wanaume kujinyanyapaa na kujikuta wengine wakijitibia chochoroni au kwa waganga wababaishaji mpaka pale wanapokuwa hoi bin taabani, mambo yamekuwa mabaya ndipo wanapopelekwa hospitalini. Hapa tunatoa wito kwa wanaume kuweka kipaumbele kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla na ujumuishe uchunguzi wa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.

Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kukupima mara moja ofisini kwake: Vipimo hivyo ni Digital Rectal Exam (DRE) na cha pili ni Prostate Specific Antigen (PSA). Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine vya uhakiki kama transrectal ultrasound au na prostatic needle biopsy. Kuwahi kugundua saratani mapema, kabla ya dalili, ni faida kubwa kwa mwaathirika. Maana saratani ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.

7.0 SARATANI NA MATIBABU:
Pamoja na yote hayo, katika zama hizi, matibabu ya saratani ya tezi dume yanapatikana. Ukigunduliwa una saratani hiyo unashauriwa ushauriane na daktari wako kuamua aina ya tiba itakayokufaa. Kuna tiba za uangalizi (active surveillance), upasuaji (surgery), mionzi (radiotherapy) vichocheo (hormone therapy) na kemikali (chemotherapy).

8.0 TUOMBWA KUUNGWA MKONO:
Katika mpango kazi wa kampeini hii tuna mahitaji mengi. Tumekusudia kuwafikia Watanzania wengi zaidi mwaka huu. Tunapenda kutumia nafasi hii kukuomba mchango wako na toka marafiki zako kwa ajili ya kampeini hii. Mwaka huu kati ya miradi tuliojipangia ni pamoja na kuchapicha vipeperushi vya Kiswahili vya saratani ya tezi dume milioni moja na kuvitawanya nchi nzima! Kipeperushi kimoja kinagharimu takribani Tshs. 250 hadi 300 kufuatana na wingi wa nakala. Vipeperushi vimekuwa vya msaada sana katika kutoa elimu ya gonjwa saratani. Kwa kuanzia mchango katika eneo hili utashukuriwa sana.

8.0 HITIMISHO: BAADA YA MAELEZO HAYO TUNAPENDA KUTOA WITO:
8.1 Kwa wanaume wote wenye umri takribani miaka 50 na kuendelea, tafadhali mwone daktari wako kwa uchunguzi wa afya ukijumuisha uchunguzi wa tezi dume;

8.2 Elimu hii itolewe pia kwa akina mama wote katika jamii mnayoishi. Wakinamama wakipata uelewa wa saratani ya tezi dume, wanaweza kuwaelimisha na kuwasaidia waume zao, baba, kaka, wajomba nk. Pia nao wahimizwe kujua juu ya saratani za wanawake kama za matiti na shingo ya uzazi nk.

8.3 Tunawaomba madaktari wote, mnapopata wagonjwa wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea washaurini pamoja na matibabu mengine, wafanyiwe uchunguzi wa tezi dume.

UKWELI KUHUSU SARATANI:
Saratani zote na hususani saratani ya tezi dume ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.

Kwa mawasiliano zaidi:
Mratibu, Tanzania 50 Plus Campaign, P. O. Box 1854 Dar es Salaam
au barua pepe : tanzania50plus@yahoo.com, info@tanzania50plus.org Simu: +255 754 402033.

KUCHANGIA KAMPEINI :
Weka katika tawi lolote la CRDB. Jina la akaunti : Centre for Human Rights Promotion CHRP;
Namba ya akaunti: 01 J 1027311100 au kupitia M-Pesa: 0754 402033

TUPIGE VITA SARATANI! TUPIGE VITA SARATANI YA TEZI DUME! PAMOJA TUNAWEZA!

Kimetayarishwa na kutawanywa na:

Tanzania 50 Plus Campaign
 
Prostatitis ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya vimelea vya bakteria katika tezi dume (prostate) kwa wanaume.
Kuna aina kuu nne za ugonjwa huu wa prostatitis
1.Maambukizi ya ghafla ya tezi dume (Acute bacterial prostatitis)
2.Maambukizi sugu ya tezi dume (Chronic bacterial prostatitis)
3.Chronic prostatitis without infection/Chronic pelvic pain syndrome/chronic non bacterial prostatitis
4.Asymptomatic inflammatory prostatitis

Tuangalie aina moja baada ya nyingine za ugonjwa huu

Maambukizi ya ghafla ya tezi dume (Acute bacterial prostatitis)

Ni maambukizi ya tezi dume yanayosababishwa na vimelea vya bakteria aina yaE.coli, Klebsiella, Proteus, Pseudomonas, Enterobacter, Staphylococcus aureus, Enterococcus, Serratia na vimelea vinavyosababisha magonjwa ya zinaa. Maambukizi haya yanaweza kufika katika tezi dume moja kwa moja kupitia kwenye damu, au kutoka kwenye kiungo kilicho na maambukizi karibu na tezi dume au huweza kufika kwenye tezi dume kutokana na athari za kufanyiwa kipimo cha kuchukua nyama ya tezi dume kuipeleka maabara kwa uangalizi zaidi au kwa lugha ya kitaalamu tunaita prostate biopsy.

Dalili na viashiria vya maambukizi ya ghafla ya tezi dume
Homa
Kuhisi baridi
Kutetemeka kutokana na baridi
Maumivu chini ya mgongo
Maumivu katika maeneo ya sehemu za siri
Kupata haja ndogo /kukojoa mara kwa mara
Kupata haja ndogo wakati wa usiku inayomfanya mtu kushindwa kuivumilia na hivyo kukimbia chooni
Maumivu/kichomi wakati wa kukojoa/haja ndogo
Maumivu ya mwili mzima

Vipimo vya uchunguzi

Complete blood count Kipimo cha damu kinachoonesha kuongezeka kwa kiwango cha chembechembe nyeupe za damu

Kipimo cha damu ili kuangalia vimelea vya bakteria kwenye damu (blood cultures). Vimelea vya E-coli vina uwezo wa kupenya kwenye tishu za tezi dume, hivyo dawa za kudhibiti E-coli zinahitaji kutumiwa kamaE-coli ndio watagunduliwa

Urine for microscope- Kipimo cha kuangalia chembechembe nyeupe za damu na bakteria kwenye mkojo

Kipimo cha damu kuangalia kiwango cha Prostate Specific Antigen (PSA). Mara nyingi kiwango cha PSA huongezeka lakini ni kwa muda tu.

Kipimo cha prostate biopsy mara nyingi hakifanywi kutokana na dalili na viashiria vya maambukizi haya kuonyesha kuwa ni maambukizi ghafla ya tezi dume, lakini wakati wa kipimo hiki, chembechembe nyeupe aina ya neutrophils huonekana kwenye tezi dume.

DRE- Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho

mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari

akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kisha kuzungusha zungusha ili

kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni ngumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini. Katika maambukizi haya ya

prostatitis,tezi dume huwa limevimba, lenye maumivu linapoguswa, lililokakamaa (firm), lenye jotojoto (warm) na kinga ambazo hazieleweki.

Kipimo cha damu kuangalia aina ya protini inayojulikana kama C-Reactive protein ambayo huwa huongezeka kiwango chake pale panakuwa na maambukizi.

Vipimo vya X-ray, Ultrasound na CT Scan vinaweza kutumika kulingana na hali ya mgonjwa itakavyokuwa au kama daktari anahisi chanzo cha maambukizi katika tezi dume kinatokana na maambukizi katika viungo vilivyokaribu na tezi dume au kuangalia viungo vilivyokaribu na tezi dume kama viko katika hali yake ya kawaida au la.

Matibabu

Matibabu ya aina hii ya prostatitis yanahusisha matumizi ya dawa aina za antibiotiki ambazo huponya maambukizi haya kwa haraka sana. Aina

nyingine za dawa hizi huwa haziwezi kupenya hadi ndani ya tezi dume (mfano ciprofloxacilin) hivyo kufanya matibabu kuwa ya shida sana. Dawa za

antiobiotiki zinazoweza kupenya kwa urahisi katika tezi dume ni dawa jamii ya co-trimoxazole, tetracyclins nk.

Wagonjwa ambao wana upungufu wa kinga mwilini au wale wenye magonjwa sugu watahitaji kulazwa hospitali ili wawe chini ya uangalizi wa karibu wa daktari.

Dawa za maumivu na za kulainisha choo pia hutolewa kwa mgonjwa mwenye maumivu au ambaye anapata choo kigumu.

Mgonjwa ambaye amepata madhara ya maambukizi haya ya ghafla katika tezi dume kama kutoweza kupata haja ndogo/mkojo, atahitaji kuwekewa

mpira wa kupitisha mkojo sehemu ya chini ya kitovu ili kumpunguzia maumivu na kurahisisha mkojo kutoka nje.

Mgonjwa ambaye amepata matibabu ya antiobiotiki na hali yake haibadiliki kuwa nzuri atahitaji kufanyiwa kipimo cha Trans-urethral ultrasound ili kuangalia kama ana jipu ndani au la.

Kinga ya maambukizi haya ni:
Kuongeza hali ya usafi katika maeneo yako ya siri
Hakikisha choo (toilet) chako ni kisafi hasa wale wanotumia vyoo vya kukaa
Kutumia dawa za antiobiotiki kulingana na maelekezo ya daktari kwani dawa nyingine hupunguza kinga yako ya mwili kwa muda na hivyo kusababisha kupata maambukizi ya bakteria.
Kama chanzo ni ugonjwa wa zinaa, ni vizuri kumueleza mwenza wako ukweli na kwenda hospitali ili kupata ushauri nasaha pamoja na tiba.

Maambukizi sugu ya tezi dume (Chronic bacterial prostatitis)

Aina hii ya prostatitis huonekana chini ya silimia 5 ya wagonjwa wote wa maambukizi ya tezi dume ambayo hayasababishwi na tatizo la uvimbe katika tezi dume.Maambukizi sugu ya tezi dume ni nadra sana kutokea na husababishwa na bakteria aina ya E-coli.Maambukizi haya hayana dalili wala viashiria vyovyote isipokuwa tu pale ambapo kutakuwa na kuenea kwa maambukizi kwenye kibofu cha mkojo.

Vipimo vya uchunguzi

Kipimo cha kuangalia vimelea vya bakteria katika mkojo (urine for culture and sensitivity)
Kipimo cha kuangalia vimelea vya bakteria kutoka katika majimaji yanayotoka kwenye tezi dume (Expressed Prostatic Secretions au EPS).Majimaji haya hupatikana wakati wa kufanya kipimo cha DRE ambapo daktari atagandamiza kidole chake kwenye tezi dume ili majimaji haya yatoke.Pia majimaji haya yanaweza kupatikana baada ya daktari kufanya kipimo hiki cha DRE kama hapo awali daktari alishindwa kuyapata haya majimaji.
Kipimo cha kuangalia kiwango cha PSA kwenye damu kama nilivyoeleza hapo awali.Kawaida kiwango cha PSA huwa juu.
Semen analysis - Kipimo cha kuangalia shahawa za mwanamume.Katika kipimo hiki chembechembe za usaha (pus cells) zitaonekana kwa wingi kuliko kiwango cha shahawa, chembechembe za shahawa zinazoonekana hapa hazina uwezo (non motile semen) wa kusafiri kwenda sehemu nyingine yoyote.Pia seli aina yaepithelial huonekana hapa.

Matibabu

Matumizi ya dawa za antibiotiki kwa muda mrefu (wiki 4-8).
Matumizi ya dawa aina za alpha blockers husaidia kwa wenye maambukizi sugu ambayo hayaishi
Maambukizi ya mara kwa mara ya aina hii ya prostatitis huweza kusababishwa na kutoweza kukojoa mkojo wote wakati wa kutoa haja ndogo kutokana na sababu mbalimbali kama uvimbe kwenye tezi dume, neurogenic bladder nk Matatizo ya vijiwe kwenye tezi dume na maumbile yanayohifadhi vimelea vya bakteria pia ni chanzo cha kujirudia kwa maambukizi haya sugu mara kwa mara.
Maambukizi ya Tezi Dume (Prostatitis) Sehemu ya Kwanza
 
Mkuu
Ubarikiwe saana

Hili tatizo limekuwa KUbwa saana hususani kwa waafrica lakini tatizo
serekali zetu
sidhani kama hata zinajua
kwa west africa ndahni ni tatizo kubwa saana linalowauwa zazee kuanzia mika 48 na kuendelea
hapa kwetu
sidhani hata takwimu hakuna kabisa
 
Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH)

Tezi Dume (Prostate gland)

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Benign-prostatic-hypertrophy-BPH-.jpg

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.

Kuvimba Tezi Dume (BPH)

Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.

Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.

Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.

BPH husababishwa na nini?

Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao

wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.
Kuna dhana (theories) kadhaa zinazojaribu kuelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

  1. Uhusiano kati ya BPH na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa BPH hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.
  2. Uhusiano kati ya BPH na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji na uklimbikaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
  3. Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli: Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.

Dalili za BPH

Alama.png

Dalili za BPH hutokea kwa sababu ya kubanwa kwa njia ya kutoa mkojo nje ya mwili (urethra) au kibofu kushindwa kuthibiti mkojo. Aidha dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu, ingawa karibu wagonjwa wote

  1. Hukojoa mkojo unaokatika katika
  2. Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  3. Husita kabla ya kuanza kukojoa
  4. Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
  5. Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
  6. Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
  7. hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  8. Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)
  9. Au dalili zinazotokana na madhara ya BPH

Madhara ya BPH

BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na

  1. Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
  2. Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
  3. Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
  4. Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
  5. Madhara katika figo au kibofu
  6. Shinikizo la damu
  7. Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
  8. Maambukizi mbalimbali
  9. Nimonia (Pneumonia)
  10. Damu kuganda
  11. Uhanithi

Vipimo na Uchunguzi

uchunguzi.jpg

Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na

  1. Kuchunguza Tezi Dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonja hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru (rectum) ya mgonjwa kasha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
  2. Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.
  3. Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.
  4. Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
  5. Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.

Matibabu

Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

Matibabu kwa njia ya dawa

Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na

  • Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishajiwa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
  • Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.

Matibabu kwa njia ya Upasuaji
Upasuaji mdogo (minimal Invasive procedures)

Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo ni

  • Tiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral microwave procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.
  • Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral needle ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
  • Tiba ya kutumia joto la maji (Water-induced thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.

Upasuaji mkubwa

Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH. Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume (Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

Vitu vya kufanya baada ya Upasuaji wa Tezi dume
Mara baada ya upasuaji wa tezi dume inashauriwa

  • Kunywa maji kwa wingi ili kusafisha kibofu cha mkojo
  • Epuka kujikakamua sana unapojihisi kwenda haja kubwa
  • Kula lishe bora ili kuepuka kupata choo kigumu. Iwapo mgonjwa atapatwa na choo kigumu ni vyema amuone daktari ili amshauri jinsi ya kuondoa tatizo.
  • Epuka na acha kunyanyua vitu vizito.
  • Hairuhusiwi kuendesha gari wala kuendesha mtambo wowote ule mpaka utakapopona kabisa.

Matatizo yanayoweza kutokea baada ya upasuaji

  • Shida wakati wa kukojoa: Kawaida huchukua muda wa siku kadhaa mtu kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida ya kukojoa.
  • Shida ya kuthibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kuthibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.
  • Kutokwa na damu: Katika siku za wali mara baada ya TURP, kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo. Hta hivyo hali hii hukoma baada ya wiki kadhaa. Hata hivyo iwapo utokaji damu ni mzito sana, inashauriwa kumuona daktari haraka.

Uwezo wa kufanya ngono baada ya upasuaji

Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH uhofia sana kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ngono mara baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hili.

  • Mdiso au kudindisha (Erections): Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata mdiso au kudinda muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupa mdiso ni mkubwa zaidi. Hata hivyo iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa kudisa tangu awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake wa kudisa.
  • Kutoa mbegu (Ejaculation): Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Hali hii kwa kitaalamu huitwa retrograde ejaculation au kilele (mshindo) kikavu (dry climax). Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuajiwa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.
  • Kufika kilele (Orgasm): Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele (orgasm) kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

BPH na Saratani ya Tezi Dume: Hakuna Uhusiano wa moja kwa moja

Ingawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume. Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kila mwaka.

Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH)
 
Back
Top Bottom