Saratani ya Mlango wa Kizazi inavyowatesa wanawake wengi duniani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Saratani ya Mlango wa Kizazi.jpg



HAPANA shaka kuwa wanawake ni moja ya makundi muhimu katika jamii yetu. Mwanamke ni mama, na ndiye kiumbe pekee ambaye hufanya kazi ya kuleta uhai duniani.

Lakini mwanamke huyu hivi sasa yu mashakani, kwani ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi umeshika kasi nchini, hivyo hutesa na hatimaye kuua maelfu ya wanawake.Saratani ni mfumo au tabia ya chembe hai nyeupe kukua katika sehemu ya mwili wa binadamu katika mfumo usio wa kawaida.

Hivyo basi, chembe hizo zikikua katika shingo ya kizazi cha mwanamke, kinyume cha taratibu, hiyo huitwa saratani ya shingo ya kizazi.

Dk Henry Mwakyoma, Daktari Bingwa wa Kitengo cha Patholojia katika hospitali ya Muhimbili, amefanya utafiti kati ya Februari 2001 na Februari 2002. Lengo la utafiti huo lilikuwa ni kuangalia ukubwa wa tatizo la saratani ya shingo ya kizazi kwa hapa nchini.

Aliwapima wanawake 224 kutoka mikoa mbalimbali nchini waliopewa rufaa ya kufika Muhimbili. Katika wagonjwa hao, 193, sawa na asilimia 86.2 waligundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na 31 sawa na asilimia 13.8 walikuwa hawana saratani.

Dk Mwakyoma anasema, miongoni mwa waliokutwa na saratani hiyo, walikuwa na umri wa kuanzia miaka 24 hadi 82.
"Katika hao walioathirika zaidi walikuwa ni wenye umri wa miaka 40 hadi 49 na wengine walikuwa na umri wa chini ya miaka 40," anasema Mwakyoma.

Daktari bingwa huyu alifanya utafiti mwingine kuhusu saratani ya aina hii kati ya mwaka 1980 hadi 1984 katika nchi za Tanzania na Uswisi. Lengo lilikuwa kuangalia ukubwa wa tatizo hili katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea.

Utafiti ulifanyika katika hospitali kuu za rufaa Tanzania, ambazo ni Bugando, KCMC, hospitali ya rufaa ya Mbeya na Muhimbili.

"Niliamua kufanya utafiti huo katika hospitali za rufaa nchini ili kupata namba ya wagonjwa katika mikoa mikubwa," anasema Dk Mwakyoma.

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa, katika hospitali ya KCMC asilimia 13.9 ya wanawake waliopimwa waligundulika na saratani ya shingo ya kizazi. Bugando, asilimia 20, Mbeya asilimia 24.3, na Muhimbili walikuwa ni asilimia 18.4 ya wanawake.
"Katika aina kumi za saratani duniani, basi saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayoongoza kwa kuwaathiri wanawake hapa nchini," anasema Dk Mwakyoma.


Chanzo cha saratani hii
Dk Mwakyoma anabainisha kuwa, sababu kubwa ambayo hupelekea wanawake wengi kupata saratani ya shingo ya kizazi ni matokeo ya ufanyaji wa ngono.

"Kufanya ngono ninaweza kusema ni sababu kubwa na sababu nyinginezo huambatana na hizo lakini kichocheo kikubwa ni ngono," anasema.

Anasema, sababu nyingine zinazosababisha mwanamke kupata saratani hii ni kufanya mapenzi katika umri mdogo. Wanawake wengi wanaofanya mapenzi chini ya miaka 16, wapo katika hatari kubwa.

"Katika wanawake waliogundulika na saratani, asilimia 14.95 kwa wastani walikuwa wameanza kufanya mapenzi wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 25," anafafanua Dk Mwakyoma.

Asilimia 17.8 ya wanawake hao, walikuwa wameolewa wakiwa na umri wa kuanzia miaka 11 hadi 35.
Hali kadhalika kati ya wanawake 161, 71 (44%) ya waliopimwa na kugundulika na saratani ya shingo ya kizazi, waliolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Sababu nyingine inayosababisha saratani ya shingo ya kizazi ni mimba na kuzaa. Dk Mwakyoma anasema, idadi ya ujauzito kwa wanawake husababisha saratani ya shingo ya kizazi.

Kwa mfano, mtu ambaye amebeba ujauzito zaidi ya mara sita (kwa hapa nchini) yupo katika hatari ya kupata saratani ya aina hii.

"Katika wanawake 193 niliowapima, 136 waliwahi kupata mimba zaidi ya mara nne, nasisitiza si kuzaa, yaani wastani wa mimba ulikuwa ni saba," anasema.Katika kiwango cha kimataifa, wastani wa kubeba mimba usio katika hatari ya kusababisha saratani ya shingo ya kizazi ni mara nne.

"Sababu nyingine ni kiwango cha kuzaa, wanawake wanaozaa sana huwa katika hatari, kwa mfano katika wanawake 193 niliowafanyia utafiti, 107 walikuwa na watoto zaidi ya wanne," anasema.

Anasema, idadi ya wapenzi ni sababu nyingine. Mwanamke mwenye wapenzi wengi, bila shaka atakuwa anafanya mapenzi kwa kiwango kikubwa, hivyo basi kupata magonjwa ya zinaa yanayosababisha saratani hii ni rahisi.

Vilevile wanawake walioolewa mara nyingi nao wamekuwa wakigundulika na saratani ya shingo ya kizazi. Kwa mfano, wenye historia ya kupewa talaka kisha kuolewa tena, au wajane wanaoolewa kwa mara nyingine na wanaotengana na wapenzi katika vipindi tofauti tofauti.

"Wapo wanaume hatari ambao nao huchangia wanawake kupata saratani ya shingo ya kizazi, hawa kitaalamu tunawaita High Risk Male Sexual Partner' hawa wanapokuwa na wapenzi wengi hutokea wakawaambukiza wanawake magonjwa ya zinaa."

Dk Mwakyoma anaongeza kuwa, ugonjwa wa zinaa ambao ndicho kichocheo kikuu cha saratani ya shingo ya kizazi ni Human Papiloma Virus 16 na 18 (HPV).Ugonjwa huu unapokomaa huzalisha seli ambazo hukua kinyume na utaratibu na kuanza kushambulia sehemu ya shingo ya kizazi.

Jambo lingine linalosababisha saratani ya shingo ya uzazi ni usafi katika sehemu za siri za mwanamke. Wanawake wanaofanya usafi sehemu zao za siri kwa kutumia bidhaa au baadhi ya vifaa visivyofaa kutumiwa ukeni huweza kupata saratani hii. Kwa mfano, bidhaa zenye kemikali ya coal tar,' ambayo mara nyingine huwekwa kwenye sabuni ama manukato.


Dalili
Dk Mwakyoma anasema, ni vyema na muhimu mno kwa wanawake kupima afya zao za uzazi kabla ya kuona dalili.


Mwanamke anapoona dalili basi saratani huwa imefikia hatua mbaya ya kifo. Anasema hatua hizi zipo katika makundi ambayo yamegawanyika.

"Ipo hatua ya mwanzo (pre-invasive) ambapo saratani bado haijafanya mashambulizi katika mwili kwa asilimia kubwa na hatua ya pili (invasive) ambayo imegawanyika katika hatua nne na hatua hii saratani huwa imeshasambaa katika sehemu nyingine za mwili," anasema.

Anazitaja dalili kuu za ugonjwa huu kuwa ni kutokwa na damu kwa wingi hasa wakati wa hedhi. Nyingine ni kutoa maji maji yenye harufu mbaya ukeni, na kupata maumivu sambamba na kutoka damu baada ya kufanya tendo la ndoa.
Dk Mwakyoma anatoa ushauri kwa serikali kuwa, itungwe sera ambapo ni lazima kila mwanamke aliye katika umri wa kufanya mapenzi akapimwe saratani ya shingo ya kizazi.

"Ili kupunguza tatizo ni bora kuwapima, tunatumia kipimo cha ambacho hata Uswisi hutumia kuwapima wanawake," anasisitiza

Naye Dk Innocent Mosha, wa kitengo cha patholojia Muhimbili anasema, ni vyema wasichana wadogo wafuate maadili na wajiepushe na vitendo vya ngono katika umri mdogo ili kujiepusha na maradhi haya.

Takwimu za mwaka 2010 kutoka Shirika la Afya Duniani, (WHO) zinasema, kwa Tanzania wastani wa wanawake 6,241 huugua saratani ya shingo ya kizazi kila mwaka na 4355 kati yao hupoteza maisha.


Chanzo: Saratani ya shingo ya kizazi yaongoza kwa kuua wanawake nchini

TIBA YAKE IPO HUO UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA MWENYE KUTAKA ANITAFUTE KWA WAKATI WAKE ILI NIWEZE KUMTIBIA NA APATE KUPONA MARADHI YAKE.
 
Kwa mujibu wa daktari inaonesha waliopimwa ni watu ambao tayari walipata rufaa kwa kuwa na dalili za awali za saratani. Sasa sitashangaa hiyo 80%. Pengine tatizo sio kubwa kama dr anavyosema.
 
je dawa za uzazi wa mpango zinachangia saratani ya shingo ya kizazi? Maana toka dawa hizo ziingie na kuanza kutumika matatizo ya wanawake ya uzazi yanaongezeka kwa kasi ya ajabu tofauti na miaka ya nyuma ambapo zilikua hazitumiki. NAOMBA UFAFANUZI
 
Maundumula, uko sahihi. Hao ni wale walioshukiwa kuwa na saratani.
Angel, sidhani kama dawa za uzazi wa mpango zinachangia kwa sababu saratani hii inasababishwa na virusi (human papilloma virus). Japo indirectly kwa sababu ya kujiamini kuwa hupati mimba pengine itaongeza ujasiri wa kufanya ngono zisizo salama.
MziziMkavu, asante kwa mada nzuri. Natamani wange-bold kuhusu kipimo cha pap-smear, kinapatikana hospitali zipi tanzania na kifanywe kila baada ya muda gani. Nitashukuru kama utaweza kufafanua kwa faida ya wote humu jamvini kwani ni kipimo rahisi tu ambacho kila mwanamke akifanya tutapunguza hili tatizo na vilio vingi.
 
dawa za kupanga uzazi ndizo zimeongeza kasi ya kufanya ngono hata kwa watoto wadogo kwa sababu hawaogopi kupata mimba. Kwa hiyo indirectily zinahusika.
 
Saratani ya kizazi inatibika iwapo itajulikana mapema. Ukimsoma Mzizi hapo juu ameongelea kuhusu dalili. Tatizo la kansa zote ni kuwa hadi dalili ziwe wazi inakuwa imeshasambaa sana na kupungua uwezekano wa kutibika. Ujanja pekee ni kufanya checkup ya hiyo pap smear kila baada ya miaka 2 (japo naona ni bora kufanya kila mwaka, haidhuru na inachukua dk 5 tu!). Matibabu ni pamoja na mionzi na kutolewa kizazi ikibidi.
Swali la nyongeza: JE KUNA TIBA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?
 
Kwa mujibu wa daktari inaonesha waliopimwa ni watu ambao tayari walipata rufaa kwa kuwa na dalili za awali za saratani. Sasa sitashangaa hiyo 80%. Pengine tatizo sio kubwa kama dr anavyosema.

Hao ndio watafiti wetu bwana,hata yule aliyesema nusu ya wanaume wagumba nilishangaa sana sample yake,eti ni wagonjwa walienda kupata tiba kwake khaaa kweli utafiti umeingiliwa,akaja kuaribu eti ukibeba laptop unaweza kupata ugumba kwa m/me,hv kuna uhusiano gani laptop hipo kwenye beg naibeba mkonon lakn huku kwenye dushelele. Linaaffectika how?
 
Saratani ya kizazi inatibika iwapo itajulikana mapema. Ukimsoma Mzizi hapo juu ameongelea kuhusu dalili. Tatizo la kansa zote ni kuwa hadi dalili ziwe wazi inakuwa imeshasambaa sana na kupungua uwezekano wa kutibika. Ujanja pekee ni kufanya checkup ya hiyo pap smear kila baada ya miaka 2 (japo naona ni bora kufanya kila mwaka, haidhuru na inachukua dk 5 tu!). Matibabu ni pamoja na mionzi na kutolewa kizazi ikibidi.
mh. Spika nina maswali mengine ma 2 ya nyongeza: KWA MUJIBU WA WATAFITI, matumizi ya baadhi ya sabuni na kemikali nyingine kusafishia "uke" husababisha cancer {1.} Je usafishaji wenye madhara ni wakusafisha uke kwa nje au kwa ndani i mean kuingiza vidole kujisafisha? {2.} je sabuni detol, na detol ya maji zina madhara?
 
Kweli mambo yanatisha lakini swali muhimu ni Je ugonjwa huu hata ukishafikia kilele chake kuna uwezekano wa kutibika?
 
Maundumula, uko sahihi. Hao ni wale walioshukiwa kuwa na saratani.
Angel, sidhani kama dawa za uzazi wa mpango zinachangia kwa sababu saratani hii inasababishwa na virusi (human papilloma virus). Japo indirectly kwa sababu ya kujiamini kuwa hupati mimba pengine itaongeza ujasiri wa kufanya ngono zisizo salama.
MziziMkavu, asante kwa mada nzuri. Natamani wange-bold kuhusu kipimo cha pap-smear, kinapatikana hospitali zipi tanzania na kifanywe kila baada ya muda gani. Nitashukuru kama utaweza kufafanua kwa faida ya wote humu jamvini kwani ni kipimo rahisi tu ambacho kila mwanamke akifanya tutapunguza hili tatizo na vilio vingi.

Hapa naona huyu daktari alikuwa na message ambayo alitaka kufikisha kwa jamii akatafuta njia rahisi.

Yeye alitakiwa atafute "unbiased" sample halafu apime watu ndio atuambie, inawezekana alikuwa anatoroka somo la statistics.

Hata hivyo ni kweli tatizo linaongezeka bongo na vizuri wakina mama wakapima matiti na shingo.
 
Hao ndio watafiti wetu bwana,hata yule aliyesema nusu ya wanaume wagumba nilishangaa sana sample yake,eti ni wagonjwa walienda kupata tiba kwake khaaa kweli utafiti umeingiliwa,akaja kuaribu eti ukibeba laptop unaweza kupata ugumba kwa m/me,hv kuna uhusiano gani laptop hipo kwenye beg naibeba mkonon lakn huku kwenye dushelele. Linaaffectika how?

laptop ni wakati unaitumia umeweka juu ya mapaja
 
je dawa za uzazi wa mpango zinachangia saratani ya shingo ya kizazi? Maana toka dawa hizo ziingie na kuanza kutumika matatizo ya wanawake ya uzazi yanaongezeka kwa kasi ya ajabu tofauti na miaka ya nyuma ambapo zilikua hazitumiki. NAOMBA UFAFANUZI
Mkuu dawa za uzazi wa mpango hazisababisha mtu kupata saratani ya shingo ya kizazi.. Mpaka sasa it has been clearly documented kuwa saratani ya shingo ya kizazi is SEXUALLY TRANSMITTED DISESASE. Hii ni kutokana na utafiti uliofanyika kuwa wagonjwa wenye saratani ya shingo ya kizazi huwa na vijidudu vya Human Papilloma Virus, HPV type 16, 18 ambao ndio husababisha saratani ya shingo ya kizazi by altering the cellular changes at the cervix and ctreate abnormality of celle with uncoordinated growth... ukilinganisha uzazi wa mpango na saratani the possibility ni kwamba those using them are sometimes having more than one partner na hivyo kuelekea uwezekano wa kupata maabukizi ya vijidudu vua human papilloma virus.
 
Nakubaliana kabisa na Dr Mwakyoma kuwa saratani ya shingo ya kizazi inaongoza kwa vifo kwa kina mama hapa nchini na hata kwa nchi nyingine zinazoendelea na hasa ukiongelea vifo vinavyosababishwa na kansa!
study sample yake siyo representative ya cimmunity na inakuwa vigumu kuongelea burden ya tatizo kwenye community kwa data zake. Yeye anasoma tu slides anazoletewa na gynecologists tu wanapochukua biopsy, na hivyo study sample yake tayari iko biased, kwa sababu hao wote ni wagonjwa wenye symptoms.

Angeenda kwenye community na akafanya sampling ndo tungeweza kupata the actual burden ya ugonjwa kwenye jamii!
 
watu wamezidi bana mtu anatundika ma valuu yake huko akirudi home ni kutwanga mtindo mmoja watakosa kupata kansa za vizazi akina mama gaude...
 
000000sarat.jpg


KWA mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2010, Tanzania kwa upande wake inao wastani wa wanawake 6,241 ambao huugua saratani ya shingo ya kizazi kila mwaka, ambapo 4,355 kati yao hufa.

WHO inakadiria kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea katika zaidi katika nchi zinazoendelea.
Hali hiyo si ya kufikirika bali ni ya kweli kwani wanawake wengi wa Kitanzania wanathibitisha hilo kwa kutoa shuhuda mbalimbali.


Mmoja wa wanawake hao, Esther Ngunangwa ambaye aliamua kufanyiwa uchunguzi baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo ambayo yalimsumbua kwa zaidi ya miezi sita.


“Nilifanyiwa uchunguzi na baadaye ikaonekana nina tatizo la saratani ya mlango wa uzazi, niliamua kufanyiwa uchunguzi huo kwa sababu nilihangaika kwa zaidi ya miezi sita bila kupata ahueni,” anasema Ngunangwa.


Naye Anitha Msigwa, anasema aligundua kwamba, anakabiliwa na ugonjwa huo baada ya ugonjwa kufikia hatua mbaya, jambo ambalo limemfanya akate tamaa ya kupona ingawa anaendelea na matibabu ya kudumu.
Idadi ya wanawake, wanaoamua kufanyiwa uchunguzi huo, inaongezeka baada ya kuwepo kwa huduma hiyo ambayo awali haikuwahi kuwepo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Getrude Mpaka, hakuwa nyuma katika kuhamasisha wanawake kukubali kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi ili wale wanaobainika kuwa na tatizo hilo waweze kupatiwa tiba.

“Niliamua kupima ili nihakikishe afya yangu baada ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kuanza kutoa huduma ya uchunguzi na tiba ya saratani ya mlango wa kizazi, Nashukuru sina tatizo la kansa, jambo la msingi hapa nimepima na nimejijua,”


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na hospitali nyingine za wilaya mkoani humo, inafanya uchunguzi wa tatizo hilo baada ya tafiti kuonyesha kuwa saratani ya mlango wa kizazi ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi hana nchini na duniani kwa ujumla.


Mratibu wa huduma ya uchunguzi wa saratani hiyo mkoani Iringa, Dk Gwachele Faustine anasema mkoa wake ni miongoni mwa ile ambayo idadi kubwa ya wanawake wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

“Nchini Tanzania hasa katika Mkoa wa Iringa, tatizo la saratani ya mlango wa kizazi ni kubwa na linakua kwa kasi ndio maana tumeanza kampeni hii kwa wanawake,ili wengi wachunguzwe na kutibiwa mapema,” anasema Dk Gwachele.


Mtaalam huyo anasema tangu waanze zoezi hilo, wamewachunguza wanawake 887 kati yao 70 walionekana na mabadiliko ya awali, 20 walikuwa kwenye hatua ya awali na tisa walifanyiwa upasuaji.


Anaongeza kuwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 30 hadi 50, ndio walio katika hatari kubwa ya kupata maambukizi na kwamba, saratani hiyo inatibika iwapo ugunduzi utafanyika mapema.


Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina wanawake milioni 10.97 walio na umri wa miaka 15 na kuendelea, ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hiyo.


Kwa Afrika Mashariki, asilimia 33.6 ya wanawake wote, wanasadikiwa kuwa na virusi aina ya Human Papilloma Virus (HPV)ambavyo ndivyo visababishi vya ugonjwa huu.


Hata hivyo, RAS Mpaka anasema licha ya kwamba huduma hiyo inatolewa bure bado wanawake wengi hawajapata mwamko wa kupima afya zao, jambo ambalo ni hatari ikiwa kansa hiyo itafikia hatua za mwisho.
Anasema ni vema wanawake wakapima ili kujua afya zao ikiwa wameathirika wapate matibabu haraka, kwa madai kuwa inawezekana kutibiwa kwa wale wanaowahi.


Kuanza kutoa huduma


Dk Gwachele anasema Mkoa wa Iringa umeanza kufanya uchunguzi na kutoa tiba ili kuokoa maisha ya wanawake ambao wamekuwa wakipoteza maisha yao kutokana na saratani ya mlango wa uzazi.


Uchunguzi huo ambao unafanywa na mkoa huo ukishirikiana na Wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Jhpiego, ulianza mnamo mwaka jana.


Kwa sasa huduma hiyo inatolewa katika vituo saba katika Mikoa ya Iringa na Njombe.

“shirika hili (Jhpiego) linasaidia kutoa ushauri katika ngazi ya kitaifa juu ya mbinu mbali mbali za kupambana na saratani ya Mlango wa uzazi ili tatizo hili hatari, litokomeze,” anasema

Hata hivyo, anasema huduma ya uchunguzi wa tiba ya saratani haipatikani kiurahisi jambo ambalo limekuwa likiwafanya wanawake wengi kwenda kutibiwa katika hospitali ya Saratani ya Ocean Road wakiwa katika hatua mbaya.

“Hali ni mbaya kwa sababu uchunguzi wa tatizo hili haufanyiki mara kwa mara, ndio maana wale wanaoenda ocean roard hufika wakati wakiwa katika hatua ya mwisho jambo linalowafanya waanze kupata tiba endelevu,” anasema Dk Gwachele


Anasema ugonjwa huo unaweza kuchukua miaka 10 hadi 20 toka maambukizi hadi kujitokeza jambo ambalo limewafanya waanze kuwachunguza wanawake mapema.
Nini husababisha saratani hii?


Mtaalamu wa magonjwa ya saratani katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk Scholastica Malangalila anasema, saratani ya mlango wa kizazi husababishwa na Maambukizi ya Virusi viitwavyo HPV.


Anasema kuwa virusi hivi huambukizwa kwa njia ya kujamIiana au kugusana kwa ngozi ya mtu mmoja na mwengine, na huambukiza wanaume na wanawake.


Vihatarishi vya saratani ya shingo ya kizazi


Dk Malangalila anataja vihatarishi vya kansa ya kizazi kuwa ni kuanza kufanya ngono mapema, kati ya umri wa miaka 16 wako kwenye hatari kupata saratani ya shingo ya kizazi siku za baadaye.

Mwanamke mwenye wapenzi wengi au mwenye mwanamume mwenye wapenzi wengi pia yupo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

Anasema utumiaji wa mipira ya kiume au ya kike hupunguza hatari ya kupata saratani hii, lakini ikumbukwe ya kwamba kondomu siyo kinga ya ugonjwa huu.


Sababu nyingine ni uvutaji sigara kutokana na kemikali zilizopo kwenye sigara ambazo zikichanganyika na seli au chembechembe za shingo ya kizazi, huleta mabadiliko katika shingo ya kizazi hatimaye kusababisha saratani.
Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi kwa muda mrefu hasa wale wanaotumia kwa zaidi ya miaka mitano, lishe duni au utapia mlo, kuzaa watoto wengi pamoja na umri mkubwa.


Dk Malangalila anasema wapo ambao wanapata maambukizi ya saratani huyo kutokana na uasili wa mtu kwa madai kuwa saratani ya shingo ya kizazi huonekana zaidi kwa watu weusi kuliko watu weupe.

Zipo sababu nyingine kama upungufu wa kinga mwilini, Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia na Kujamiana na mwanaume ambaye hajatahiriwa.

Dalili na viashiria vyake


Mtaalamu huyo anasema saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote jambo ambalo limewafanya kuanza kutoa huduma ya uchunguzi katika mjkoa huo ili wanawake,waweze kupima mapema, na kujua hali zao.


Anasema dalili nyingine za ugonjwa huo ni pamoja na kutokwa na damu, Kutokwa na damu mara baada ya kujamiana na maumivu makali wakati wa kujamiana.


Dalili za saratani iliyosambaa ni kupungua kwa hamu ya kula, kupungua uzito, kuhisi uchovu, maumivu ya nyonga, maumivu kwenye mgongo, maumivu ya mguu, mguu mmoja kuvimba, kuvunjika mifupa na kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye sehemu ya uke wa mwanamke.


Anasema matibabu ya ugonjwa wa saratani hiyo hutolewa kulingana na hatua za ugonjwa na hali ya mgonjwa.
“Matibabu ya ugonjwa huu yanatolewa kulingana na hatua ya mgonjwa mwenyewe na njia za kutoa matibabu ni pamoja na upasuaji katika hatua za mwanzo, mionzi na dawa za saratani,” anasema.


Hata hivyo anaongeza kuwa, ipo huduma endelevu kwa wagonjwa wa saratani ambayo hutolewa kwa lengo la kupunguza makali na kuboresha afya kwa watu wenye magonjwa sugu, ikiwemo saratani.


Aidha, anashauri wanawake kujenga tabia ya kupima mara kwa mara ili kubaini mapema endapo wana saratani na kuanza matibabu mapema kabla maradhi hayo hayajafikia hatua mbaya.
Mwisho.Saratani ya mlango wa kizazi inavyowatesa wanawake wengi duniani


 
Darasa lako zuri,endelea kutuelimsha. kwa mwanaume ambaye hajatahiriwa inakua vipi hadi kusababisha saratani hii,kwa uchafu au maumbile tu?
 
Hala hala wanjF, leo hii nilikuwa hospitali ya ocean road nikimsindikiza kimwana mmoja hivi ambaye aliitikia mwito wa MEWATA. Nikiwa pale, ndipo alijitokeza doctor fulani ambaye kwa bahati mbaya sikulipata jina lake kwa lengo la kutoa elimu kwa watu wote tuliokuwa tuko pale tukisubiri ama huduma ya tiba au wagonjwa wetu tuliowasindikiza. Alisema mengi lkn ninayoyakumbuka ni haya yafuatayo.
1. Saratani hurithishwa lkn haiambukizwi.
2. Saratani inaweza kutibika ikiwa utawahi kuanza tiba.
3. Kuna tiba aina mbili za saratani-mionzi na/au drip
4. ikiwa saratani ya shingo ya kizazi itatibiwa kwa mionzi basi hupelekea uke kuziba kwani hupona kwa kuumanisha nyama za ndani za mashavu ya uke- hii aliitaja kwa kitaalamu kama "healing by fibrosis" (kama nilisikia sawasawa). Athari ya kuziba huku ni kwamba uchafu wa ndani (natural internal discharges) utakuwa hautoki. Hii haihusishi mkojo.
Ili kuepuka hili ni lazima uanze mara moja kukutana na mwanaume kama umeolewa ama utumie medical artificial penile objects kama hujaolewa. "Vinginevyo uke utaziba na hakuna namna ya kuuzibua na hutakaa uingiliwe tena" alisisitiza daktari yule.
5. Tiba ya mionzi kwenye saratani ya kizazi huua mayai yote na mwanamke hatozaa tena.
6. Dalili za saratani ya shingo ya kizazi ni kutokwa na damu unapokutana na mwanaume.
Naishia hapo wanaJF Asnteni.
 
Wana jamvi na madaktari naomba kupata ufahamu/elimu kuhusu kansa ya kizazi/ovarian cancer

  • Inasababishwa na nini?
  • Dalili zake (za awali na zionekanazo kwa vipimo)
  • Madhara yake
  • Matibabu
  • Jinsi ya kuzuia
Natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom