Sarafu Moja E.A.C : Ripoti Yatoka, Mabishano Makali Yazuka

Thanda

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,915
596
Mabishano makali yamezuka katika mjadala unaoendelea Katika Makao Makuu ya Jumuiya Ya Afrika Mashariki Huko Arusha katiya Kenya na Rwanda. Hoja ikiwa ni wao wanataka kuwe na sarafu moja ya jumuiya, lakini waendelee kubaki na sarafu zao kama kawaida huku Rwanda ikisisitiza USD iwe ndio hela ya jumuiya na kila mmoja abaki na sarafu yake. majadiliano yatakayodumu kwa siku sita mfululizo yanalenga kuikomboa Afrika Mashariki kiuchumi. Tofauti ya mikopo toka IMF kwa nchi mojamoja jinsi ya kuulipa mkopo huo kwa pamoja, ni moja kati ya masuala yaliyojadiliwa.

Sudan ya Kusini ambaye mara zote yeye huwa mgeni mwalikwa na "Mtazamaji" tu (Observer) safari hii kaambiwa asubiri kwanza hadi wao wakubaliane mambo ya msingi. Kenya imetunisha misuli baada ya Tanzania kuitunishia misuli kuhusu suala la ardhi. hivi punde nita-attach nakala ya ripoti yote na mchakato mzima jinsi ulivyokuwa.
 
Kwa kuanzisha sarafu moja haitokubalika mana kiukweli kila nchi inajivutia kwake tuuuu
 
Politicians think that a common currency is achievable by looking the case of the USA.
In order to attain a common currency, each country should agree to forego it's monetary sovereignty and then build upon a framework to regulate inflation and bilateral trade between member states and third countries.

There are so many issues that will make monetary integration impossible, we have inflation, sovereign debts, unbalanced international trade, black markets etc.
 
Tukisema tutumie sarafu ya marekani, yaani usd, then kila kitu kitakuwa non sense kwa maana ya kuukomboa uchumi wa jumuia. tutakuwa tunamuimarisha marekani. Hata hivyo liwalo na liwe
 
USD ni hela ya Wamarekani, haiwezi kuwa hela ya Jumuiya.

Wanaosema USD iwe hela ya Jumuiya wana maana jumuiya itakuwa na uwezo wa kuchapisha USD?

Kuna tofauti kati ya kutaka USD itumike throughout jumuiya na kusema USD iwe ndiyo hela ya jumuiya.
 
Nadhani Tanzania na Uganda ndo wanapenda sarafu moja , ikikubalika Tanzania tutakuwa na hela tatu tofauti zikitumika kwa wakati mmoja
 
West African CFA franc inatumika nchi nane; Benin,Burkina Faso,Cote d ivoire,Guinea Bissau,Mali,Niger,Senegal na Togo tangu 1945 bila matatizo/mgogoro wowote na kwa mafanikio makubwa. Sarafu moja bila shaka itarahisisha biashara EA.
 
Kwa kuanzisha sarafu moja haitokubalika mana kiukweli kila nchi inajivutia kwake tuuuu
Ripoti zote za awali zapita, Final report ni leo au kesho....Tanzania yatunisha misuli,yaukataa mwongozo wa IMF na World Bank, Burundi yabebwa, hadi sasa bado hawajaiona lunch.
 
Wajinga ndio waliwao. Hata hawajifunzi nini kinatokea Europe au kwenye francophone countries.
Tanzania iko juu, yakataa mapendekezo ya IMF na WB waziwazi mbele ya wajumbe, member state walalamika, Warwanda wabishi mno..Beno Ndulu apaa.
 
Kwa Rwanda kusema tuitumie dollar ya marekani ni matusi heri wangesema tuitumie sarafu yao.
Uganda wajitetea, wakumbushia ya vita ya Kagera, waomba "Monetary and Repayment Grace Period" mapema kabla hata ya final report kutoka. Kila mjumbe ana page yake mkononi...asijesaini baadaye akasema nilikurupushwa...Wakishindwana leo mkutano ujao utafanyika Rwanda....Ujerumani yaonya kupitia GIZ
 
Kwa sasa hali ni imekuwa mbaya, Kwenya imekataa kwenda Rwanda kwa sababu ya kuisapoti M23 na Uganda pia yahusishwa, Final Report kutosainiwa leo makubaliano yagonga mwamba, wanakamilisha ratiba.....kama nilivyoahidi nitawajulisha na nita-attach documents muhimu mtaziona wakuu. JF NI KILA KITU
Politicians think that a common currency is achievable by looking the case of the USA.
In order to attain a common currency, each country should agree to forego it's monetary sovereignty and then build upon a framework to regulate inflation and bilateral trade between member states and third countries.

There are so many issues that will make monetary integration impossible, we have inflation, sovereign debts, unbalanced international trade, black markets etc.
 
Uganda wajitetea, wakumbushia ya vita ya Kagera, waomba "Monetary and Repayment Grace Period" mapema kabla hata ya final report kutoka. Kila mjumbe ana page yake mkononi...asijesaini baadaye akasema nilikurupushwa...Wakishindwana leo mkutano ujao utafanyika Rwanda....Ujerumani yaonya kupitia GIZ
Ukienda sokoni kule kigali, hata mboga za majani hununuliwa kwa USD
 
Hizi ni habari za sasa hivi, ndo wanarudi ndani na speech inaanza waganda wanalalamika kuwa waganda wanasema "tanzanians sayingi no issues on this"...kweli kwa hili kumekuwa na umakini. Nitawahabarisha na gharama zote za mkutano huun tangu ulipoanza siku ya Tarehe 19.10.2012
Mabishano makali yamezuka katika mjadala unaoendelea Katika Makao Makuu ya Jumuiya Ya Afrika Mashariki Huko Arusha katiya Kenya na Rwanda. Hoja ikiwa ni wao wanataka kuwe na sarafu moja ya jumuiya, lakini waendelee kubaki na sarafu zao kama kawaida huku Rwanda ikisisitiza USD iwe ndio hela ya jumuiya na kila mmoja abaki na sarafu yake. majadiliano yatakayodumu kwa siku sita mfululizo yanalenga kuikomboa Afrika Mashariki kiuchumi. Tofauti ya mikopo toka IMF kwa nchi mojamoja jinsi ya kuulipa mkopo huo kwa pamoja, ni moja kati ya masuala yaliyojadiliwa.

Sudan ya Kusini ambaye mara zote yeye huwa mgeni mwalikwa na "Mtazamaji" tu (Observer) safari hii kaambiwa asubiri kwanza hadi wao wakubaliane mambo ya msingi. Kenya imetunisha misuli baada ya Tanzania kuitunishia misuli kuhusu suala la ardhi. hivi punde nita-attach nakala ya ripoti yote na mchakato mzima jinsi ulivyokuwa.
 
You can hardly have a successful single currency without streamlining the various countries monetary and fiscal policies. This is evident from the Eurozone example.
 
USD ni hela ya Wamarekani, haiwezi kuwa hela ya Jumuiya.

Wanaosema USD iwe hela ya Jumuiya wana maana jumuiya itakuwa na uwezo wa kuchapisha USD?

Kuna tofauti kati ya kutaka USD itumike throughout jumuiya na kusema USD iwe ndiyo hela ya jumuiya.

Well said!!
 
You can hardly have a successful single currency without streamlining the various countries monetary and fiscal policies. This is evident from the Eurozone example.
Mkutano mwingine unaendelea AICC, unahusu masuala ya elimu, ni wa hiyohiyo EAC, vuta nikuvute inaendelea. Uganda yabanwa ieleze vigezo ilivyotumia kuwa na masomo zaidi ya 20 kwa shule zake za sekondari....yatakiwa ieleze pia vigezo ilivyotumia kuyapunguza hadi 18. Kama ni kwa shinikizo la "Member States" au ni utaratibu wake yenyewe.....Naye mwakilishi wa wizara ya elimu ajichanganya...mkutano huu siwezi pata attachment kabisa, sina mtu wa uhakika kule...Ila huu wa fedha nina access nao sana tu. Wa elimu naweza kuwapa updates tu lakini si picha, nitajaribu na huu wa fedha kama nitapata picha kidogo, hata mbili tu zinaweza kuwa ushahidi.

Katika mjadala huu wa sarafu ya pamoja jion hii, Uganda yajitoa.
Mwenyekiti wa kitaifa mwenye mwongozo hakuingia (amedai eti Tanzania imemchefua)
Katibu wake hakuwepo
Mwakilishi wa Wizara ya Afrika Mashariki Kaingia mitini
Waganda wameushindwa huu mkutano
Kenya waonesha ukomavu- wametetea nafasi yao vyema, Secretary wa Mwenyekiti adai ana udhuru, aondoka ghafla kurudi Nairobi.....kaletwa wa dharura kuokoa jahazi, waambiwa hawana ukarimu hata shukrani pindi wanapoingia nchi za watu, Rwanda yauliza sababu za wakenya wanaofanya kazi Uarabuni kupewa muda wa mwisho kufanya kazi nchini humu...hoja: labda walijihusisha na hela chafu..waulizwa kama wameiomba serikali ya Riyadh isiwafukuze huko ili wachangie katika pato la nch yako pindi warudipo nyumbani..wajieleza, Tanzania yakataa kuridhika....Uganda yatetea hoja, yaulizwa kauli ya chokochoko ya Kaguta Museveni kuwa "IKIWA MIGINGO NI YA KENYA MAJI YAKE NI YA UGANDA" alimaanisha nini,,,,,alihatarisha usalama wa pato la wenzao."Tanzania yajibu"
Tanzania wapo wote, wanashindana kwa nguvu ya hoja.....VIVA TANZANIA.

Anazungumza Tarsice Kadede, Huyu ni Director of Planning wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kitengo cha Uchumi

Rwanda na Uganda wapandishiwa kodi za bandarini hadi watakapoacha kusapoti vita kwa majirani zao, wakikataa watawekewa viwango na aina ya bidhaa watakazosafirisha. (Jamani mdau mwingine aliyeko mkutanoni aongezee kitu hapa)
Masikini Sudan ya Kusini, hata kualikwa hakupo kwa vigezo vitatu tu: 1. Fedha yake haitambuliki kimataifa, 2.Bado sio mwanachama, 3. Ukanda wake una vita visivyo vya lazima.

taarifa za hivi punde ni kwamba "Final Report" ni kesho Jmosi, na huenda Tanzania ikawa ndio sababu "kama mwenyeji pia" ya sarafu hiyo kukwama...Mkutano kwa leo umeisha hadi kesho saa tatu asubuhi....Kesho jioni nitaanza ku-attach some important documents kwani hata yanayojadiliwa ni siri mno. hakuna waandishi wa habari ni yule mpiga picha wa E.A.C pekee ndio yuko humo ndani, E.A.C wana mwandishi wao wa habari...hakuna cha ITV wala TBC, kBC wala EATV wote watasubiri hadi repoti ikisainiwa au isisainiwe hapo tu ndio wataalikwa rasmi.HII NDIYO JUMUIYA MPYA YA AFRIKA MASHARIKI.....

Kwa leo basi....kesho ndio mbivu ama mbichi....tusubiri.

Back
Top Bottom