Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
Nimefurahi sana kuona wadau mbalimbali wapenda maendeleo ya soka hapa nchini kwetu wamejitokeza kwa wingi kupinga kauli za kibabaishaji zinazotolewa na watu wachache wasiopenda kuona Tanzania inapiga hatua muhimu katika maendeleo ya soka. Ni wakati muafaka sasa tujifunze kuwaheshimu wataalam na pia kujifunza kutoka kwao. Nina hakika leo hii ukipata wasaa wa kufanya mahojiano na waliowahi kuwa makocha wa Taifa Stars nadhani tunaweza kusikia mambo ya aibu zaidi ya tunavyohisi. Kelele zinazopigwa juu ya kutaka kuingilia kazi za Maximo huenda zimejitokeza baada ya kundi ambalo lilizoea kufanya hivyo huko nyuma kushindwa kujipenyeza katika ukuta mgumu unaoongozwa na beki mashuhuri na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Rais Leodgar Tenga. Laiti kama tungekuwa na uongozi wa kubabaisha sidhani kama Maximo angekuwepo leo hii. Mwisho tumpatie ushirikiano kwa wakati maximo kama kocha wetu wa Timu ya Taifa.