Sangara wa Chadema kuhamia Tanga Sept 3

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumanne, Agosti 28, 2012 05:42 Na Oscar Assenga, Tanga

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Tanga Mjini, kinatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara katika kata zote zilizopo wilayani hapa kuanzia Septemba 3 mwaka huu.

Katibu wa chama hicho Wilaya ya Tanga Mjini, Khalid Rashid aliliambia Mtanzania jana kuwa, mikutano hiyo ya kisiasa itakuwa na malengo mawili.

Alisema lengo la kwanza ni kuelimisha wananchi kujiunga na chama hicho na kuimarisha matawi yao yaliyopo katika kata mbalimbali.

Rashid alisema, lengo la pili litakuwa ni kuwaandaa wanachama waliopo wilayani hapa kwa ajili ya ujio wa viongozi wa chama hicho Taifa, pamoja na wabunge katika Operesheni Sangara awamu ya pili.

Alisema Operesheni hiyo itaanza mwezi ujao katika mikoa mbalimbali hapa nchini, ambapo itaanzia mkoani hapa na kuendelea nchi nzima ikiwa na lengo la kukiimarisha chama hicho.

Katibu huyo alisema, katika uhamasisha huo watahakikisha wanazungumza kuhusu kukichangia chama hicho kwa ajili ya zoezi la uhamasishaji wa wananchi kujiunga na chama hicho.

Akizungumzia suala la Sensa Rashid alisema, suala hilo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na hivyo wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu, ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu halisi za wananchi wake.

“Watanzania ni lazima wafahamu kuwa mchakato huo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi, hivyo wananchi waliopo hapa nchini, hawana budi kuonyesha ushirikiano kwa makarani wa Sensa,” alisema.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Wafike Muheza wawafungue wale wabondei miaka 50 ya uhuru maji ya bomba ni jambo la anasa. Inatia uchungu sana wakati chanzo cha maji ya Tanga kipo Muheza lakini siasa inakwamisha zoezi hili.
 
Safi sana M4C twanga kote kote, kila kona! maandalizi mema make sure vibali vinapatikana in time tusonge mbele!
 
Aiseee babaangu naomba utupe update huku kwetu rombo watakuja lini?? Mi na mke wangu 2nataka kuvua magamba maana yanawasha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom