Wana Jamvi, kwa mtazamo wangu sita ni mzalendo wa kweli mwenye uchungu na nchi yake
kwasababu kuu zifuatazo:
-Uwezo wake kama spika kuruhusu mijadala ambayo imeweza kutishia uhai wa ccm.
-Kuto wogopa mafisadi wenye fedha ambao wanaogopewa.
-Kukataa kuwaangukia mafisdi.
Nani asiyekumbuka jinsi ndugu Sitta alivyoweza kuruhusu mjadala wa richmond bungeni, ambao umeleta kitimutimu kufikia hatua ya EL kujiuzuru? kutoka na mkasa huu ndipo tulipojua udhaifu wa ccm, wengine tulikuwa hatujuhi.
Sitta aliweza kushikilia msimamo wake wa kuwashambulia mafisadi bil kuigopa, inahitaji ujasiri kwa kweli kwani kama waziri mkuu mizengo pinda mwenye ulinzi madhubuti aliwagwaya mafisadi kwa kusema ni watu hatari, lakini Sitta aliendeleza mapambano nao.
Kitendo cha Sitta kukataa kuwaomba radhi mafisadi mbele ya kamati ya usuluishi wa ccm ni kitendo cha ujasiri.
Kweli sitta ni mzalendo mwenye uchungu na nchi yake na ni zaidi ya raisi, kitendo cha kikwete mtu ambaye yupoyupo asiyejali chochote kumpa uwaziri sitta ni ukweli tosha kuwa sitta ni zaidi y raisi.
Mkuu Zimwi la DR Slaa bado linakuandama, Hapa anasemwa sitta wewe unamuingiza Dr Slaa. Madrasa bwana!Hata huyo Dr Slaa sio msafi mkienda kwenye database ya kanisa mtaona madudu yake, na ni aibu kwa mtu mzima mwenye umri kama Dr Slaa mwenye kuijua dini awe anavunja amri ya sita!
Binafsi kila mmoja anamawaa yake na kila mtu ana sifa zake.