Samweli sitta na ufisadi huu

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Je tunawezaje kuwatoa kwenye sakata la ujenzi wa chini ya kiwango wa ukumbi wa bunge jipya ? bunge lililojengwa kwa mabilioni sasa linavuja na ukaguzi umeonyesha uhajajengwa kwa kiwango stahiki na hakuna mitambo ya usalama iliyofungwa mle ndani na pili wamepoteza nyaraka za jengo hili ya michoro na BOQ zake.

je samweli sitta na katibu wa bunge bwana kashilila hawakuhusika katika ufisadi huu?

au ni njama za Anna makinda na kundi lake kumchafua sitta ?
 
Hivi umeandika nini hapa? Hoja nzito kama hii haina vielelezo wala takwimu?
 
Halafu wakati wa ujenzi wa jengo hilo Kashilila wala hakuhusika
 
Mtatamani sana kumchafua sita hamtafanikiwa,
Mtanadi sana mafisadi hamtafanikiwa,
Mtatumiwa sana na mafisadi hamtafanikiwa,
Sita bado atasimama na kuwanyoshea kidole hao mafisadi bila woga
Na siku yao itafika wananchi watamuunga mkono!
 
Sita kapata ubunge wakati jengo lishajengwa.....hahusiki na hiyo kashfa unless una njama zingne...hukumbuki jengo limeanza kutumika lini mpaka unatoa thread ambayo haina mashiko?Hiyo ni issue ya makamu mwenyekiti ccm Pius Msekwa.
 
Bila shaka huyu jamaa katumwa na nape na chama chao cha magamba,.............hata mkioga kamwe hamtaenda mjini
 
hoja ni ujenzi wa Bunge chini ya kiwango je sitta amehusikaje katika sakata hii? kwani jengo ni bovu wala halina mitambo ya usalama na wamepoteza document muhimu za michoro na mikataba ya ujenzi
 
Je tunawezaje kuwatoa kwenye sakata la ujenzi wa chini ya kiwango wa ukumbi wa bunge jipya ? bunge lililojengwa kwa mabilioni sasa linavuja na ukaguzi umeonyesha uhajajengwa kwa kiwango stahiki na hakuna mitambo ya usalama iliyofungwa mle ndani na pili wamepoteza nyaraka za jengo hili ya michoro na BOQ zake.je samweli sitta na katibu wa bunge bwana kashilila hawakuhusika katika ufisadi huu?au ni njama za Anna makinda na kundi lake kumchafua sitta ?
Ujinga ni kipaji. Kwa taarifa tu. Ukumbi mpya wa bunge ulijengwa enzi za Msekwa, ulijengwa na serikali kwa mkopo wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Hawakutoa fedha, bali walikuwa wanalipa moja kwa moja kwa wakandarasi. Hata kama kuna ufisadi, kwa vyovyote vile Sitta hakuhusika wala kashillila, maana katibu wakati huo alikuwa Damian Foka. Madudu haya ya kijinga huibuka siku Lowassa akiguswa kwa ufisadi wake.
 
Sita kapata ubunge wakati jengo lishajengwa.....hahusiki na hiyo kashfa unless una njama zingne...hukumbuki jengo limeanza kutumika lini mpaka unatoa thread ambayo haina mashiko?Hiyo ni issue ya makamu mwenyekiti ccm Pius Msekwa.
mjumbe punguza jazba kwani kama yeye si aliyeanzisha ujenzi huu ok, lakini wakati wa makabidhiano ya jengo si angefuatilia kama ujenzi umefanyika kwa kiwango husika una maana kama rais kikwete kasaini mkataba 2014 na 2015 rais mwingine kaingia hatowajibika kuona mkataba umefuatwa au sitta kwanini hakuchunguza viwango vya bunge na kama mitambo ya usalama imefungwa na ata mic zimefungwa za mchina
 
Jengo wala si la serikali.....ni la muungano wa mashirika ya pensheni sasa Sitta ndio Dr. Dau?......mstitake kumpaka SAMAKI matope akiwa mtoni
 
Jengo la bunge bovu linavuja, Chuo kikuu Dodoma kibovu majengo yana nyufa na kinavuja. Spika ni mwanasiasa mahali pabovu pakipakwa rangi inayovutia huridhika asihusishwe wala kusemwa.

PPF ya William Erio mjomba wa Fisadi mwandamizi Mkapa, NSSF ya Ramadhani Dau mtaalamu wa madau ya kifisadi na PSPF ya Mama Mmanga AKA mama wa Quality Plaza ya Manji ndio wa kuhojiwa na polisi kwa ubovu huo

Kama Erio wa PPF alikiuka taratibu za manunuzi ujenzi wa UDOM na kumpa kazi ndugu yake kwa kisingizio kuwa ameagizwa na Ikulu unategemea nini kwenye majengo ya umma? UDOM inavuja hasa majengo yalijengwa na PPF. Angalieni pia huo ukumbi wa bunge kama sio kipande cha PPF maana ni wachakachuaji mno.
 
mjumbe punguza jazba kwani kama yeye si aliyeanzisha ujenzi huu ok, lakini wakati wa makabidhiano ya jengo si angefuatilia kama ujenzi umefanyika kwa kiwango husika una maana kama rais kikwete kasaini mkataba 2014 na 2015 rais mwingine kaingia hatowajibika kuona mkataba umefuatwa au sitta kwanini hakuchunguza viwango vya bunge na kama mitambo ya usalama imefungwa na ata mic zimefungwa za mchina
kwa mantiki hiyo sitta bado hausiki labda anne makinda spika wa sasa.isitoshe yeye alikuwa naibu spika
 
Jengo jipya la bunge lilijengwa na kuanza kutumika wakati wa awamu ya tatu (Rais Mkapa, Waziri Mkuu Sumaye, Spika Msekwa)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kila kitu kilchofanywa na serikali ya ccm kina ufisadi ndani kabla wapenda nchi wafuasi wa cdm hamjachangia hii mada na kwa vile kila kitu kinawahusu magamba hata kama wengine wanachafuana wao watuambie kwani hata hii thread wameanzisha wao.
faiza fox,malaria sugu,riz1,na magamba wenzenu changieni hiyo sisis tukishuka ni rungu tu.
peoplessss..............................
 
Jengo jipya la bunge lilijengwa na kuanza kutumika wakati wa awamu ya tatu (Rais Mkapa, Waziri Mkuu Sumaye, Spika Msekwa)
jengo jipya limefanya makabidhiano chini ya spika sitta kwa hiyo mnataka kusema kwanini tunamsakama kikwete kwa mikataba ambayp ameingia mkapa ....je kwa upande wa sitta yeye mbona mnasema hausiki na kama hausiki ni nini alifanya ili sisi watanzania tumuone kuwa anapambana na ufisadi, mbona wa bunge yeye akutaka kusema ata kidogo. ni mara ngapi ata spika zinagoma kuongea bungeni hakuhoji. ni mara ngapi anakona wakati wa mvua linavuja hasemi. napenda kujua yeye amehusikaje kwenye sakata hili
 
Je tunawezaje kuwatoa kwenye sakata la ujenzi wa chini ya kiwango wa ukumbi wa bunge jipya ? bunge lililojengwa kwa mabilioni sasa linavuja na ukaguzi umeonyesha uhajajengwa kwa kiwango stahiki na hakuna mitambo ya usalama iliyofungwa mle ndani na pili wamepoteza nyaraka za jengo hili ya michoro na BOQ zake.

je samweli sitta na katibu wa bunge bwana kashilila hawakuhusika katika ufisadi huu?

au ni njama za Anna makinda na kundi lake kumchafua sitta ?

Jengo jipya la Bunge limejengwa na Mashirika ya Mifuko ya Pensheni kwa pamoja kukubali kufadhili na kusimamia ujenzi wa ukumbi huo. Mashirika hayo ni Public Service Provident Fund (PSPF), Local Authority Provident Fund (LAPF), Parastatals Provident Fund (PPF) na National Social Security Fund (NSSF). Samuel Sitta siye alijenga jengo la Bunge.

MODERATORS toeni hii thread, ni dhahiri huyo aliyeiweka ametumwa kumchafua Sitta baada ya kumbana ipasavyo Edward Lowassa kuwa maamuzi magumu pia ni kwa kiongozi kuwa muadilifu na kukataa 10 percent kama Lowassa alivyopokea kwenye Richmond.
 
Back
Top Bottom