Samweli Sitta aongoza harambee ya kuchangisha pesa Dodoma

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
DSC_0019.jpg


DSC_0096.jpg

Picha ya kwanza:
Mkuu wa Mkoa Dodoma akiongoza maandamano ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watawa wa shirila la Mt. Gemma Galgani jimbo Katoliki dodoma.

Picha ya pili:
Mheshimiwa Swamweli Sitta aliyekuwa mgeni wa heshima katika kuchangisha pesa za ujenzi wa nyumba ya watawa akimsalimia Askofu mstaafu Mathias Isuja wa jimbo katoliki Dodoma.

Kuna kitu ambacho najifunza katika matukio haya yanayoendelea katika kuhamasisha watu kuchangia maendeleo, vyama vya siasa na mashirika mbalimbali.

Kuna dalili za wazi wafadhili ambao tulizoea kuwa nao ambao wamesaidia mengi kwa sasa hali ngumu ya uchumi inayoikumba dunia wameanza kuadimika, na njia pekee ni sisi wenyewe kushikamana na kuwasaidiana kwani uwezo tunao, sababu tunazo, tukiunganisha nguvu tutaweza.

Chadema wamekusanya mamilioni katika harambee yao pale Dar, Samweli sitta kakusanya kadhaa leo hapa Dodoma, na kwengineko tukiendelea na moyo huu huu tutafika mbali kuliko kupitisha bakuli huko nje na hivyo kupambana na masharti magumu ya mikopo yao yenye riba.

Rais Mkapa alifanikiwa kuanzisha mradi wa maji ya Ziwa Victoria kuja Shinyanga na mikoa mingine ya kati, hali kadhalika ujenzi wa Daraja la Tanzania-Msumbiji. Aliweza kwa nini tusifuate nyanyo hizo?
 
sijui wanatoka mitaa ya nyerere square? au wanaelekea wimpy heheheheheheh
 
Tungejaribu kuanzishwa kwa mtindo wa online. Hii ya aina hii maandalizi yake tu ni ghali, unaweza kushtukia pesa ipatikanayo katika harambee hii ni kidogo kuliko iliyotumika katika maandalizi.
 
Back
Top Bottom