Samwel Sitta Live on Mlimani TV

hawa uliowataja walikuwa wanashauri wakiwa nje ya uongozi lakini Sita yupo ndani na anaweza kushauri ndani kwann asifanye hivyo wakati nafasi yake inamruhusu ndio maana tunasema kama ushauri wake hausikilizwi hana budi ujiuzulu uwaziri kwa sababu huwezi fanya kazi na serikali ambayo inatenda mambo ambayo hayatendi haki na wewe haukubali haki isitendeke.

Chakunyuma unauhakika na unachokiandika usipotoshe watu sokoine mauti yalimukuta akiwa kiongozi au akiwa amesitafu upande wa mzee baba wa taifa toka mwanzo wa uongozi alikuwa mpigania haki
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM. Mhe. Sita toka huko uanzishe upinzani wa kweli!!!!!!
 
Anayoyasema Sitta ni kweli tupu, lakini baadhi watamshambulia kwa kumuita kwamba ni mnafiki. Sijawaona wala kuwasikia hao wasio wanafiki ndani ya CCM au Serikali wasimame hadharani na kuyazungumza hayo yanayozungumzwa na Sitta ambayo ni kweli tupu. Hao wanaodhaniwa kwamba si wanafiki ndani ya CCM/Serikali wako kimyaaaa! huku wizi wa mchana kweupe wa kuwalipa Dowans shilingi bilioni 113 ukiandaliwa kimya kimya. Na hao wasiokuwa wanafiki wakisubiri mgao wao kwa kufanikisha malipo.

Bora mnafiki anayesema kweli hadharani kuhusu maudhi mbali mbali ndani ya nchi yetu ikiweko ufisadi uliokithiri au asiye mnafiki lakini kayafumbia macho maudhi yote na ufisadi kama vile kila kitu ndani ya nchi kiko shwari kabisa?

Salute
 
Jikelambegu tuambie, unafiki wake ni upi???kazi yake hujaiona??bunge alililoliongoza la tisa unalinganisha na bunge lip?la sappi, msekwa?au makinda???
 
Wel said bak, watu wanasemasemasema tu, unafiki wake ni upi??ameongelea ccj, alifuatwa ila hakukubali wito!suala kumsamehe mtu kiasa huku kaliingiza taifa kwenye janga ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite,akaongelea kuubana uongozi usisamehe mambo ya ovyoovyo?

Kafunguka sana huyu mzee na amethubutu kutokea na kuruhusu simu kuulizwa na watanzania!amejibu kwa busara na hekima wasio wanafiki wako wapi????AMEONGELEA JUU YA USHAURI WANAOUTOA KWA UONGOZI NA MENGI YANAPUUZWA SASA UNATAKA AFANYE NINI YEYE SI MUAMUZI, UPEO MDOGO WA MAMBO NDO UNAFANYA WATU WANAPOST ISUE ZA AJABU HUMU!
 
Ata kama ni mnafiki angalau anathubutu!
Ila mzee six chunga afya na uhai wako baba maana nowdays ni mwendo wa kuwacollimba wale wote wenye mtazamo hasi na mafisadi
 
Anayoyasema Sitta ni kweli tupu, lakini baadhi watamshambulia kwa kumuita kwamba ni mnafiki. Sijawaona wala kuwasikia hao wasio wanafiki ndani ya CCM au Serikali wasimame hadharani na kuyazungumza hayo yanayozungumzwa na Sitta ambayo ni kweli tupu. Hao wanaodhaniwa kwamba si wanafiki ndani ya CCM/Serikali wako kimyaaaa! huku wizi wa mchana kweupe wa kuwalipa Dowans shilingi bilioni 113 ukiandaliwa kimya kimya. Na hao wasiokuwa wanafiki wakisubiri mgao wao kwa kufanikisha malipo.

Bora mnafiki anayesema kweli hadharani kuhusu maudhi mbali mbali ndani ya nchi yetu ikiweko ufisadi uliokithiri au asiye mnafiki lakini kayafumbia macho maudhi yote na ufisadi kama vile kila kitu ndani ya nchi kiko shwari kabisa?
[/QUOTE

Kaka Sitta siyo Mnafki hata kidogo, umesahau wadanganyika wa nchni hii akili zao na uwezo wao wa kufikiri, kuweka kumbukumbu na hata kufikiria maslahi ya taifa hili?

Umesahau walivyoimbishwa wimbo wa Kikwete mwaka 2005 na wakauimba bila hata kuhoji uwezo wake na makosa yote aliyofanya ya IPTL, na zero perfomance toke awe mbunge wa Bagamoyo 1990 na hadi 2005, huku wakijuwa CV yake imejaa vimwana tu na kukenuwa meno?

Huo wa Siita Mnafsi ni wimbo mpya wamepewa wanauimba kwa bidii kwa sauti kubwa na kukalili besi zake kwa mtiririko wa sauti ya kwanza hadi ya nne bila hata kufikiri, maudhui ya huo wimbo. Uliona wapi support ya Umma wakati Sitta, Mwakyembe na wenzao wachache wakipamba na Dowans takriban watu watano tu nchni nzima bila support yoyote hata ya kuandamana kuwaunga mkono! Uliona wapi support ya Umma dhidi wa wapinaji wa Ufisadi ndani ya CCM kama si wao wenyewe kupoteza huku Watanzania wakicheka na kushangilia katika mabaa na kusikiliza Bunge kama mchezo wa kuigiza, na mara walipopewa Original Comedy basi ndio ikawa adithi zao na simulizi zao kila kukicha kuanzia kwenye daladala hadi maofisini! Wapo wapi wakina Selelii na Shelukindo Umma umewaenzi vipi kwa kazi waliyofanya kama siyo kuwanyima kura za Ubunge na kuwapa mapandikizi wa Mafisadi?

Kila anayemwita Sitta Mnafki kwangu mimi namuona kama sawa mtu mfu hasiye na faida yoyote humu ndani ya Tanzania maana nchni haijengwi bila Umoja wetu na kamwe haitasimama bila ujasiri wa Vijana ambao ndio punguwani sasa hivi wanaoimaliza hii nchni.
 
Kaka Sitta siyo Mnafki hata kidogo, umesahau wadanganyika wa nchni hii akili zao na uwezo wao wa kufikiri, kuweka kumbukumbu na hata kufikiria maslahi ya taifa hili?

Umesahau walivyoimbishwa wimbo wa Kikwete mwaka 2005 na wakauimba bila hata kuhoji uwezo wake na makosa yote aliyofanya ya IPTL, na zero perfomance toke awe mbunge wa Bagamoyo 1990 na hadi 2005, huku wakijuwa CV yake imejaa vimwana tu na kukenuwa meno?

Huo wa Siita Mnafsi ni wimbo mpya wamepewa wanauimba kwa bidii kwa sauti kubwa na kukalili besi zake kwa mtiririko wa sauti ya kwanza hadi ya nne bila hata kufikiri, maudhui ya huo wimbo. .

Simple and clear, hapa ndipo tatizo letu Watanzania lilipo, i salute you..
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM. Mhe. Sita toka huko uanzishe upinzani wa kweli!!!!!!

Wewe hukumwelewa Nyerere. alisema upinzani utatoka ndani ya CCM hii hina maana kuwa watu watatoka ndani ya CCM ili wapinge sera za CCM. Mimi namshauri huyu mzee abanane nao hukohuko mpaka kieleweke na ikiwezekana wasambaratishe hicho chama ili upinzani upate pa kupenyea. Akitoka tu amekwisha kwani na yeye wanazijua kashfa zake na atakuwa ameji - expose akiwa nje ya CCM na serikali.
 
Chakunyuma unauhakika na unachokiandika usipotoshe watu sokoine mauti yalimukuta akiwa kiongozi au akiwa amesitafu upande wa mzee baba wa taifa toka mwanzo wa uongozi alikuwa mpigania haki
Nakubaliana na ww kwamba alikuwa mpigania haki lakini hakusema tu halafu akakaa kimya kwa mfano alipoona kuna makosa yanafanyika alianzisha programu kama azimio la Arusha, na wahujumu uchumi sasa m6 yeye anasema tu hatuambii tufanye nn kama malipo dowans ni wizi wa mchana! Nipo tayari kurekebishwa.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM. Mhe. Sita toka huko uanzishe upinzani wa kweli!!!!!!
Hiyo pointi ishakuwa irrelevant.Sooner or later,wakienda upinzani itakuwa too late kwasababu itaonekana ni hawakufurahishwa na nafasi walizopewa hapo awali.Kama hawakupenda jinsi serikali inavyoongoza,na wao wanafanya nini kwasasa?Si walikuwabli nfasi walizopewa na wanapokea order toka juu?Ndio hapo unapoona wananchi wengi wanadai kuwa ni unafiki.Hilo litawacost.Ndani na nje ya chama wasipokuwa makini.Decisiveness was lacking.Ni kweli mwalimu alisema mambo mengi ambayo ni right.Lakini siyo yote yaliyotokea ama yatakayotokea kuwa kweli.Ndo ukweli huo.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
attachment.php

Wanafiki wote hawataurithi ufalme wa Mungu; heri wanyenyekevu na wapole maana hao watarithi nchi....na heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu...
 
kweli ni mnafiki yeye na Mke wake, wamehozi ardhi kubwa , huko nyuma ya nyama chabisi BOKO eti wamejenga ka shule uwanja una ekali kumi una thamani ya Billion Moja , watuambie wana mradi gani, nao sio wasafi kabisa kama baba wa taifa alijengewa na Jeshi nyumba nzuri wao hata million 300 wamezipata wapi? au mzee wa madili, kiwanja kinaitwa kwa mama sita kiko njia ya Boko ZOO ya wanyama
 
kama kweli basi umefika wakati sasa inabidi watz tuanze kujitetea wenyewe kwa sababu tunaowategemea nao wanatuumiza kwa njia zingine.
 
anasema wahujumu uchumi ambao walipigwa vita enzi ya mwalimu hivi sasa ndio wanaoheshimika na kupewa nafasi na hata kupata heshima kubwa zaidi, taifa limepoteza ile misingi aliyoanzisha mwalimu

Sita bwana! alijisahau kuwa hata yeye Mwalimu alimweka benchi kwa ajili ya ufujaji wa mali ya umma, anafikiri Watz tumesahau. Unafiki wake anaona wenzie wote vimeo isipokuwa yeye...puh!
 
i hate Ccm but i like 6. Huyu mzee anafanya kazi nzuri, bila yy ririchm
ond scandal isinge kuwa kama ilivyo sasa. Wanaosema mnafik
i hawajatambua mchango wake.
 
Bora kusikiliza katuni kuliko sita .Tatizo anachoongea sio anachomanisha,CCM wote ni wabadhirifu wa mali ya watanzania hana usafi wowote kaoza kuliko hata anaowaimba mafisadi kila siku.akafie zake Urambo na aombe kuzikwa ndani ya lile jenge alilobeba mabilioni ya serekali kwenda kujijengea ofisi ya bunge URAMBO-bora angejenga kituo cha afya
 
Back
Top Bottom