Samwel Sitta, Harison Mwakyembe, Bernard Membe: Huu ndio ufisadi mbaya kuliko wote

cdm kwa kujifagilia hatuwawezi!!! Wewe bwana tupe mikakati yenu ya kutatua kero ubungo, tangu tumewapa jimbo, mpo busy na maandamano endelevu badala ya kushughulikia mahitaji wa wapiga kura.

mabaya tuambieni mema pia mtujuze,kimara kulikuwa na shida kubwa sana ya maji,pamoja na mabomba ya mchina kuwekwa bado maji ilikuwa kero leo hii angalau mabomba yanatoa maji kwa ufuatiliaji wa mbunge.

Not only that mambo mengi yako jikoni lakini nani asiyejua majimbo ambayo yanaongozwa na chadema serikali kuu inazuia maendeleo mengi yanayotakiwa kufanyika?

Mfano ni bajeti ya kinondoni.tumevumilia sana sasa tutaanza kuwaondoa kwenye viti wale wanaofanya maamuzi ya mwisho ili muone jitihada za wabunge.

Otherwise acha kejeli.tulipofika leo nikwakuwa chadema tupo makini vinginevyo watu mngeanza kuikimbia nchi.
 
Ha ha haaaaa Chaggas Development Manifesto (CHADEMA) ndio viongozi wenyewe hawa mlio nao kweli wa kushika dola
Nadiriki kusema kwamba mimi ni CCM lakini kwa ujinga kama huu wakuonglea ukabila ama dini ya mtu ni ujinga wa highest order kama huwezi kujenga hoja ni afadhali uachane ni hizi issue zisizokuwa na mshiko
 
Mwambene
Kubali Bosi wako Bernard Menbe ana reasoning Capacity ndogo

Wewe acha mambo ya ku-personalize mambo mpaka unaanza kutapa tapa kwamba huyu Mbopo ni Mwambene na kwa hakika unaonyesha wazi kabisa lile bifu lako la kukosa ajira Foreign Affairs bado halijaisha. Kwa taarifa yako kazi hutapata na sasa kama umeamua kukodiwa kupigana vita vya wengine basi hutafanikiwa. Hivi unataka kusema Membe na Lowassa nani ambaye reasoning capacity kubwa? Hivi kuwa mwizi na kutengeneza mbinu ya kumaliza wenzio ndiyo reasoning capacity?

Tumechoka kusikia upuuzi ule ule kila wakati. Nyie mjibadilishe majina mtakavyo lakini ukweli ni kwamba kila uchochoro mtakaopitia sisi tutaendelea kuwapigania watanzania na kuwaeleza adui yao kwa ustawi wao ni nani!
 
Samwel Sita, Ana Killango ,Harison Mwakyembe na wengine kadhaa mliokuwa mnajiita mitume kumi na wawili hamna lolote wala hapakuwa na ufisadi wowote mliokuwa mnajifanya wapiganaji wa ufisadi bali maslahi binafsi .Tulijaribu kusema kwamba sita alikuwa na hasira na lowasa kwa sababu alinyimwa uwaziri Mkuu kwa kuwekewa" kauzibe" na lowasa

Tukasema mwakyembe alikuwa kambi ya mwandosya na ana hasira kwa wanamtandao kumkosesha mtu wake Urais, Tukasema Bernard Membe alikuwa na hasira na Lowasa kwa sababu Serikali ya kwanza ya Jk alipewa Unaibu uwaziri kwa sababu Lowasa alikuwa anamwelewa vizuri Membe kuwa ana uwezo mdogo (Reasoning capacity yake ni ndogo) ,Mama kilango yeye ana hasira na lowasa kwa sababu Malecela alikosa Urais.Naamini hata leo ukifanywa uchunguzi huru itathibitika kwamba kila mmoja wenu kwenye mitume 11 alikuwa na maslahi ambayo yalikwamishwa na Lowasa ndio maana wakajiunga kummaliza mzee mwenye mvi nyingi kichwani

Haya yamethibitika baada ya sita kuteuliwa uwaziri na akakubali ,uteuzi wa Rais sio wa lazima unaweza kuukataa tena kwa lugha nzuri ambayo haitamkwaza Rais.Lakini kitendo cha Sita na Mwakyembe kukubali kimethibitisha kuwa hawa ni watu hatari kuliko hata waliokuwa wanawatuhumu ,CCM ni walewale wakizidiana wanatumia kila fursa Kumalizana ?ni mfano wa vibaka waliokwenda kuiba walipopata cheni ya dhaabu walioishika wakawaingiza wenzao mjini.walichofanya walioingizwa mjini wakaenda kuwaripoti waliowaingiza mjini polisi .Ndicho mlivyofanya pale mwlipowaripoti mafisadi wenzenu wananchi wakawapigia kelele wakajiuzulu halafu nyinyi mkaingia serikalini kuendelea kula

Sasa Rais Kamteua Mrindoko mliemtuhumu kwa Ufisadi,sita na Mwakyembe wameteuliwa na Rais na Mrindoko kateuliwa na Rais ngoma droo na bado wanaendelea kubaki kwenye serikali hiyo hiyo ya Mbayuwayu huu ndio ufisadi mbaya kuliko wote
hapo kwenye red sijapaelewa.
 
Back
Top Bottom