Samsung yaleta simu inayofukuza mbu!

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
galaxy-pocket.jpg

Kampuni ya Samsung Tanzania, imezindua simu ya Samsung Galaxy Pocket yenye uwezo wa kufukuza mbu usiku, pindi mtumiaji anapowasha.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Belinda Lawuo ambaye ni miongoni mwa watumiaji watano waliopata fursa ya kutumia simu hiyo siku chache kabla ya uzinduzi uliofanyika juzi.

Lawuo alisema alipopata simu hiyo alifurahishwa na uwezo wake wa kufukuza mbu kupitia programu ya Mosquito Repellant.

Naye Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar alisema simu hiyo inampa mnunuzi thamani halisi ya pesa, kwani inauzwa bei nafuu, huku kukiwa na ofa mbalimbali, ikiwemo kutuma ujumbe bure mara 100 kwa mwezi na kifurushi cha intaneti.
 
Mosquito Repellant ni Android application (inayotoa utrasonic sound zenye very high pich kiasi ya kufukuza mosquito). Sidani kama hii program ina uhusiano wowote na Samsung Company (hata kama imekuja pre-installed), sababu haijatengenezwa na Samsung na simu yoyote unawezaitumia nayo kwa kudownload kupitia https://play.google.com/store/apps/details?id=com.antimosquitoh1&hl=en.

Hapo ni either Samsung wamechukulia ujiko kutoka kwa hiyo program au hii habari ina walakini.
 
nyinyi hebu acha kushangaa ujinga siku zote ili usogee kwenye ushindano wa biashara lazima pia ugundue alichonacho mwenzio so samsung kuwa na hii program ni suala la kawaida kwan mbona hata nokia anaiga baadhi ya application kutoka kwa wengine.
mimi ninaona sawa tuu tena samsung yeye ameanza kuiga kesho utasikia nokia anafuata
 
Mosquito repellent, Anti-mosquito etc.. ni Application kama application zingine zote na zinatengenezwa na developers mbali mbali kwaajili ya Operating System kadhaa ikiwemo IOS, Bada, Windows OS, Android, Maemo etc na zinafanya kazi kwa teknolojia ile ile ya kutoa sauti zenye frequency kubwa zinazofukuza mbu ,,si kwamba ni simu kwaajili ya kufukizia mbu, bali ni application ya simu inayoweza kufukuza mbu! na kwa iphone unawezadownload kupitia App Store - Mosquito Repellent au App Store - Anti Mosquito - Sonic Repeller etc...
 
Hawa Jamaa wanasifa hii app mbona ipo kitambo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hiyo ni application na sio kwamba imetengenezwa na simu. Mimi nimeipata kwenye iTunes free of charge kwa wenye iPhone, iPad, iPod. Nadhani hata SaMSUNG
 
galaxy-pocket.jpg

Kampuni ya Samsung Tanzania, imezindua simu ya Samsung Galaxy Pocket yenye uwezo wa kufukuza mbu usiku, pindi mtumiaji anapowasha.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Belinda Lawuo ambaye ni miongoni mwa watumiaji watano waliopata fursa ya kutumia simu hiyo siku chache kabla ya uzinduzi uliofanyika juzi.

Lawuo alisema alipopata simu hiyo alifurahishwa na uwezo wake wa kufukuza mbu kupitia programu ya Mosquito Repellant.

Naye Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar alisema simu hiyo inampa mnunuzi thamani halisi ya pesa, kwani inauzwa bei nafuu, huku kukiwa na ofa mbalimbali, ikiwemo kutuma ujumbe bure mara 100 kwa mwezi na kifurushi cha intaneti.

Mkulu anasemaje, maana naona yuko hatarini kukusa msaada wa net zake anazogawa?
 
Back
Top Bottom