Samson Kipepe afariki dunia

bwana ametoa bwana ametwaa

macho yanabubujikwa na machozi mioyo imejaaa huzuni na hatusemi ila lile linalomridhi mola wetu nalo ni kushukuru kwa haya unayotupatia.

tunakuomba mwenye nguvu na mweny maamuzi juu ya maisha yetu uwape faraja na maliwazo mema wale wote waliokuwa karibu na marehemu kuanzia mama yake mkewe na watoto wake ndugu zake na waliosalia.

mwisho tunakuomba usitufitinishe kwa kifo chake na kwa yake aende apumzike bila ya kubughudhiwa

ameen
 
Unajua Wewe Ni Ki Kati Ya Watu Wa Pumbavu Sijapata Kuona Katika Maisha Yangu...hapa Watu Wanatoa Pole Za Msiba Na Kumwaga Mpendwa Wao.wewe Unajifanya Mwanamapinduzi Wa Kupambana Kila Mahali Kibaraka Wa Jm.mila Za Afrika Hatubagui Watu Ktk Misiba Au Kujifanya Wewe Ndiwe Mwanamapindizi Sana Falasi Wewe.

Sasa kuna ubaya gani? hata mimi natoka mbeya-kyela na kweli kuna mafisadi na wanafiki wengi. wewe ni wa kupuuzwa na kusamehewa!
 
Marehe Kipepe,Upumzike Kwa Amani na nawapa pole sana watu wote wa Mbeya kwa kumpoteza kijana Shupavu na mliyemtegemea.

Mungu ailaze mahali pema Roho ya marehemu Kipepe
 
Buriani kaka yetu Kipepe. He said,"I was born with nothing, and I will die with nothing. The LORD gave, and now he has taken away. May his name be praised !". JOB 1,21
 
Unajua Wewe Ni Ki Kati Ya Watu Wa Pumbavu Sijapata Kuona Katika Maisha Yangu...hapa Watu Wanatoa Pole Za Msiba Na Kumwaga Mpendwa Wao.wewe Unajifanya Mwanamapinduzi Wa Kupambana Kila Mahali Kibaraka Wa Jm.mila Za Afrika Hatubagui Watu Ktk Misiba Au Kujifanya Wewe Ndiwe Mwanamapindizi Sana Falasi Wewe.

Acha u-dikteta wako na kuanza kutukana watu hapa! Natoa pole nyingi sana kwa wafiwa; Mungu aipokee roho yake kwa amani. RIP Samson Kipepe
 
nami naungana na wanaJF kutoa pole kwa msiba wa huyu ndugu yetu ambaye inaonekana alijulikana vyema kwa wanaJF.natoa pole kwa familia ya marehemu,wazazi. mkewe,watoto,ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huu.mwenyezi MUNGU aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi amen
 
Sasa kuna ubaya gani? hata mimi natoka mbeya-kyela na kweli kuna mafisadi na wanafiki wengi. wewe ni wa kupuuzwa na kusamehewa!

Mkuu Shalom, msamehe huyu ndugu hajui alifanyalo, ukipenda mpuuze ili tuendelee kuomboleza.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMEN.
 
Pumzika kwa kwa amani kaka kipepe!Binadamu aliyeumbwa na MUNGU siku zake za kuishi duniani ni chache nazo zimejaa Taabu,Kwa kuwa tu mavumbi na mavumbini Tutarudi!
Mungu awafariji wana familia wote,jamaa na marafiki!
BWANA ALITOA NA SASA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE!
Amen!
 
Nimezipokea habari za kifo cha kada Kipepe kwa mshtuko mkubwa sana.Nilipoamka tu asubuhi majira ya saa 1.30 asubuhi kwa saa za hapa Marekani nikiwa najitayarisha kwenda kibaruani,kuwasha kompyuta na kuingia kwenye JF ghafla,nakutana na kichwa cha habari chenye habari yenye kisikitisha sana.Ukweli ni kwamba kwa kiwango fulani,hii taarifa japo ni vema kuwa nimeipata mapema,lakini imeniharibia siku yangu.Hakika nimeguswa sana!
Marehemu Kipepe tulifahamiana tangu mwaka 1998 wakati sote kwa pamoja tulipoingia kwenye uongozi wa UVCCM,mimi nikiwa Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya na yeye wakati huo alikuwa ni mchumi wa UVCCM,makao makuu.Tuligombea kwa pamoja ujumbe wa baraza kuu la UVCCM, Taifa katika uchaguzi wa mwaka 1998 mjini Dodoma.Mimi sikufanikiwa kushinda bali comrade Kipepe alishinda nafasi hiyo baada ya kutofanikiwa katika nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM dhidi ya Mh.Dr.Emaanuel Nchimbi(MB).
Tulifanya kazi wote kwa kipindi hicho chote cha miaka 5 ya uongozi wetu,alikuwa ni kijana makini sana mwenye uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja na mwenye kujiamini sana.Sifa ambazo ninaamini zilipelekea kupandishwa cheo hadi kuwa Afisa Tawala Mkuu wa UVCCM,Makao Makuu.Mara ya mwisho nilikutana naye mjini Dodoma katika kikao cha baraza kuu la UVCCM mwaka jana nilipokuwa nyumbani Tanzania,kwa likizo fupi ya majira ya kiangazi.Tuliongea masuala mengi sana yahusuyo jumuiya yetu na chama kwa ujumla.
Hakika UVCCM tumempoteza kada mahiri sana hasa katika kipindi hiki muhimu kabisa,ambapo jumuiya inakabiliwa na uchaguzi mkuu.Ni imani yangu kwamba busara,hekima,umakini,na zaidi sana, uzoefu wake mkubwa katika shighuli za UVCCM,vilikuwa bado vinahitajika sana hususani kwa uongozi mpya tunaoutarajia kuupata mwishoni mwa mwaka huu.
Nahitimisha kwa kutoa pole kwa uongozi wote wa UVCCM chini ya Mwenyekiti comrade Nchimbi,Familia,ndugu, jamaa,na marafiki wote walioguswa na msiba wa mpendwa wetu Samson.Mungu awape faraja ya kweli na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi."Ukagone Kikolo,ijo joo njila jitu twesa!!!!".Bwana alitoa na hatimaye Bwana ametwaa,Jina lake Libarikiwe"
 
Nimezipokea habari za kifo cha kada Kipepe kwa mshtuko mkubwa sana.Nilipoamka tu asubuhi majira ya saa 1.30 asubuhi kwa saa za hapa Marekani

Mzee ukisema saa 1.30 asubuhi kwa saa za hapa Marekani ni nafuu usingeandika tu hiyo sentensi au ungetupa zone zaidi ya hapo haitusaidii kitu hiyo sana sana unatuambia uko Marekani.
 
Back
Top Bottom